WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DOKTA PHILIP MPANGO ATETA NA MKURUGENZI MKUU WA UNIDO, BW. LI YONG
HomeJamii

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DOKTA PHILIP MPANGO ATETA NA MKURUGENZI MKUU WA UNIDO, BW. LI YONG

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akimlaki Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughuli...

WAZIRI DKT. MWAKYEMBE ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA MARIALLE
RAIS DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI MZEE KINGUNGE NA WAGONJWA WENGINE WALIOLAZWA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI
RATIBA RASMI YA MAZISHI YA MAREHEMU PERAS MKE WA MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU





Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akimlaki Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo ya viwanda (UNIDO), Bw. Li Yong, nje ya ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu J.K. Nyerere, Jijini Dar es Salaam. leo Machi 9, 2018.

NA BENNY MWAIPAJA-WFM
WAZIRI wa Fedha na Mipango,Dkt.Philip Mpango amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo ya viwanda (UNIDO), Bwana Li Yong ambapo wawili hao wamezungumzia namna Tanzania na UNIDO zinavyoweza kuimarisha zaidi ushirikiano ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa viwanda ifikapo 2015.
Katika mazunguzmo hayo Dkt. Mpango amesema Serikali ya Tanzania inathamini sana mchango wa kitaalamu unaotolewa na shirika hilo, hasa katika mipango ya maendeleo ya kiuchumi, na kuwataka kuendelea kuiunga mkono Serikali hasa katika kusaidia uboreshaji wa miundombinu mbalimbali ili kuinua sekta ya viwanda.
‘Katika miaka mitano ya kwanza ya mpango wa maendeleo wa Taifa, mojawapo ya agenda ni kuboresha miundombinu, nishati ya umeme, teknolojia ya mawasiliano na rasilimali watu ambapo vyote kwa pamoja vitatufikisha katika malengo tuliyokusudia’alisema Dkt.Mpango.
Aidha Dkt. Mpango amesema sekta ya viwanda ni sekta muhimu, hivyo Serikali inahitaji kushirikiana kwa pamoja na wadau mbalimbali ili iweze kufikia malengo iliyojiwekea katika miaka mitano ya kwanza ya mpango wa maendeleo wa Taifa.
"Mpango wa maendeleo wa sasa unalenga kuifanya nchi yetu iwe nchi ya uchumi wa kati, kwa kujenga mazingira mazuri ya biashara na kuzalisha wataalamu wa viwandani" Alisisitiza Dkt. Mpango
Alisema kuwa pamoja na mikakati hiyo ya kuendeleza viwanda bado sekta hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ikwemo ya uzalishaji mdogo wa bidhaa za viwandani, uzalishaji wa bidhaa ambazo hazikidhi ubora wa kimataifa na uchache wa wataalamu katika usimamizi wa shughuli za viwandani, hivyo Serikali inahitaji kuungwa mkono na sekta binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuinua uchumi wa nchi kupitia sekta ya viwanda.
Kwa upande wake Bwana Li Yong, amesema ili kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali, ni lazima kusimamia vyema maono na mikakati ya kimaendeleo na kuongeza kuwa anatarajia kujifunza vitu vingi kipindi atakchokuwepo hapa Tanzania, hasa katika hatua ambayo nchi imefikia katika uendelezaji wa viwanda.
Li Yong alisisitiza umuhimu wa kuishirikisha sekta binafsi na kupanga mipango thabiti itakayoiwezesha sekta hiyo kukuza uwekezaji kwa kuweka mazingira bora ya uwekezaji na ufanyaji biashara na kuahidi kuwa Shirika lake liko tayari kufanikisha azma hiyo ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto) akimwongoza mgeni wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo ya viwanda (UNIDO), Bw. Li Yong, kufanya naye mazungumzo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu J.K. Nyerere, Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kushoto) akiongoza ujumbe wa Wizara ya Fedha na Mipango wakati wa mazungumzo na mgeni wake ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo ya viwanda (UNIDO), Bw. Li Yong (wa tatu kulia), mazungumzo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu J.K. Nyerere, Jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na mgeni wake ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo ya viwanda (UNIDO), Bw. Li Yong (kulia), mazungumzo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu J.K. Nyerere, Jijini Dar es Salaam.(PICHA WFM)

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DOKTA PHILIP MPANGO ATETA NA MKURUGENZI MKUU WA UNIDO, BW. LI YONG
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DOKTA PHILIP MPANGO ATETA NA MKURUGENZI MKUU WA UNIDO, BW. LI YONG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEigZKHfLlHeXZ_p3eqV990j9WpM-INzVNWpvu7tnNXOVDDt72RW57rVwI6k4IwDN2UIIxjbUblVNUchieREJuxDLW-54FoHBF6czufoStZmt9UNFdk50K6QF6VG9xanEXRs7rOgcgcHsPk/s640/IMG_2464.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEigZKHfLlHeXZ_p3eqV990j9WpM-INzVNWpvu7tnNXOVDDt72RW57rVwI6k4IwDN2UIIxjbUblVNUchieREJuxDLW-54FoHBF6czufoStZmt9UNFdk50K6QF6VG9xanEXRs7rOgcgcHsPk/s72-c/IMG_2464.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/waziri-wa-fedha-na-mipango-dokta-philip.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/waziri-wa-fedha-na-mipango-dokta-philip.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy