JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA HABARI UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO TAARIFA KWA UMMA ...
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA HABARI UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO
TAARIFA KWA UMMA
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mchora Katuni mashuhuri Ndg. Thaddei Thomas Marealle kilichotokea asubuhi ya tarehe 05 Januari, 2018 katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam.
Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa kifo chake Ndg. Thaddei kimeinyang’anya fani ya uchoraji na kwa ujumla tasnia nzima ya Sanaa za Ufundi mmoja wa Wasanii mahiri waliokuwa tegemeo kubwa la Maendeleo ya tasnia hiyo nchini.
Dkt. Mwakyembe ametoa pole kwa familia, uongozi wa kampuni ya WAMASA Puplications Ltd, ndugu, jamaa, marafiki na wanasanaa wote nchini na kuwaombea Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu cha msiba.
Kipindi cha uhai wake marehemu Ndg. Thaddei alifanya kazi na kampuni ya WAMASA Publications Ltd inayo chapishaji gazeti la Sani. Marehemu Thaddei atakumbukwa sana kwa katuni yake maarufu ya Sokomoko iliyokuwa ikichapishwa na gazeti la Sani.
Imetolewa na:
Octavian F. Kimario
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
07/01/2018.
COMMENTS