RAIS DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI MZEE KINGUNGE NA WAGONJWA WENGINE WALIOLAZWA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI
HomeJamii

RAIS DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI MZEE KINGUNGE NA WAGONJWA WENGINE WALIOLAZWA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Simu: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz T...

SERIKALI NA WADAU KUENDELEA KUZUIA MAAMBUKIZI MAPYA YA VIRUSI VYA UKIMWI
WAANDISI WA BAM INTERNATIONAL WASHAURI WASICHANA WAPENDE MASOMO YA SAYANSI
MWADHAMA KADINALI POLYCARP PENGO AUKANA WARAKA WA PASAKA WA MAASKOFU, SIRI YAFICHUKA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 06 Januari, 2018 amewajulia hali baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam wakiwemo Mzee Kingunge Ngombale Mwiru na Mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti.
Katika wodi ya Mwaisela, Mhe. Rais Magufuli amemjulia hali Mzee Kingunge Ngombale Mwiru ambaye anatibiwa majeraha baada ya kushambuliwa na mbwa wake, nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Ibrahim Mkoma wa hospitali hiyo amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa hali ya Mzee Kingunge inaendelea vizuri.
Mzee Kingunge amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kwenda kumuona hospitalini hapo na amemueleza kuwa sasa anajisikia nafuu baada ya kupata matibabu.
Pamoja na kumpa pole na kumuombea apone haraka Mhe. Rais Magufuli amesema anatambua mchango mkubwa wa Mzee Kingunge katika siasa na maendeleo ya nchi.
Katika wodi ya Sewahaji, Mhe. Rais Magufuli amemjulia hali Bw. Richard Kajumulo ambaye ni Kaka wa Mbunge wa Muleba Kusini Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka, Bw. Said Abeid Salim, Bi. Amina Ismail Shirwa, Mzee Hamad Lila na amempa pole Naibu Katibu Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Zainab Chaula aliyefiwa na Mama yake mzazi wakati Mhe. Rais akiwa wodini humo.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amewajulia hali mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti ambao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa matibabu ya moyo.
Maria na Consolata wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kwenda kuwaona na kuwapa pole na pia wameongoza sala ya kumuombea Mhe. Rais Magufuli na nchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi amesema matibabu kwa Maria na Consolata ambao ni wanafunzi mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki Ruaha (RUCU) yanakwenda vizuri.
Aidha, Prof. Janabi amesema taasisi hiyo imefanikiwa kutoa matibabu kwa wagonjwa wa moyo 1,400 katika mwaka uliopita na kwamba inashika nafasi ya tatu barani Afrika kwa utoaji wa huduma bora za matibabu ya moyo.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewashukuru na kuwapongeza madaktari wa hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kazi kubwa wanayofanya kutibu wagonjwa na amesema Serikali itaendelea kutatua changamoto zinazowakabili ili kuboresha huduma zaidi.
“Nawashukuru sana madaktari na wafanyakazi wote, mnafanya kazi kubwa ya kuwatibu wagonjwa, pia mmeboresha hospitali na inaonekana ni safi, mimi niwaahidi kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira yenu ya kazi ili muendelee kutoa huduma nzuri” amesema Mhe. Rais Magufuli.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliyelazwa kwa ajili ya matibabu katika Wodi ya Mwaisela iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliyelazwa kwa ajili ya matibabu katika Wodi ya Mwaisela iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali watoto wawili Mapacha walioungana Maria na Consolata ambao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya Matibabu.







Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akisali pamoja na watoto wawili Mapacha walioungana Maria na Consolata ambao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya Matibabu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi pamoja na wafanyakazi wengine wa Taasisi hiyo mara baada ya kutembelea wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wapishi wanaofanya kazi ndani ya Hospitali ya Muhimbili wakati akitoka kuona wagonjwa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Kaka wa Profesa Anna Tibaijuka (KUSHOTO) ajulikanye kwa jina la Richard Kajumulo ambaye amelazwa katika Wodi ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na manesi wanaohudumia wagonjwa katika Wodi ya ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Nasoro Rashid aliyelazwa katika Wodi ya ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali mzee Hamadi Lila aliyekuwa akilia kwa furaha mara baada ya kumuona Rais alipofika katika wodi ya Sewahaji. (PICHA NA IKULU)
































Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI MZEE KINGUNGE NA WAGONJWA WENGINE WALIOLAZWA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI
RAIS DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI MZEE KINGUNGE NA WAGONJWA WENGINE WALIOLAZWA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI
https://lh6.googleusercontent.com/tPd9N05msNoQg6PlHcnSJsRwXQiLSY-8DmLUeWhGw8GjjyIGcfHimzbI4WRop4ABuuR5b_MFPLDIiZclewLcG5kPq2Ku5g-RiJbZqmeqgl-XLE0ybIovDpO3dsHS6L3zCXQPAviAZCp4q6Pzfg
https://lh6.googleusercontent.com/tPd9N05msNoQg6PlHcnSJsRwXQiLSY-8DmLUeWhGw8GjjyIGcfHimzbI4WRop4ABuuR5b_MFPLDIiZclewLcG5kPq2Ku5g-RiJbZqmeqgl-XLE0ybIovDpO3dsHS6L3zCXQPAviAZCp4q6Pzfg=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/01/rais-dkt-magufuli-amjulia-hali-mzee.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/01/rais-dkt-magufuli-amjulia-hali-mzee.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy