WAZIRI MKUU AKUTANA NA WAKURUGENZI WA KAMPUNI YA NAMERA NA JOC
HomeJamii

WAZIRI MKUU AKUTANA NA WAKURUGENZI WA KAMPUNI YA NAMERA NA JOC

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa .amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa JOC, Qin Mengwei (Kulia). na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera ...

VIDEO: GUMZO LA LAKE FM KWENYE GULIO LA MTAA JIJINI MWANZA.
DARAJA LA MAGARA KUANZA KUJENGWA MWEZI JULAI
BOTI YA MV MKONGO YASAFIRISHWA KUELEKEA UTETE PWANI





Waziri Mkuu Kassim Majaliwa .amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa JOC, Qin Mengwei (Kulia). na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi (kushoto mwenye miwani nyeusi) . Wakurugenzi hao wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa. Nchini Tanzania. Waziri Mkuu amekutana na viongozi hao leo, Februari 12, 2018 Ofisini kwake jijini Dar es Salaam







WAZIRI MKUU. Kassim Majaliwa. amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa viwanda vikubwa viwili vya kuchakata pamba cha Namera Group of Industries,na JOC. Wakurugenzi hao wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu huu.Waziri Mkuu amekutana na viongozi hao leo, Februari 12, 2018 Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa viwanda vikubwa viwili vya kuchakata pamba ambao wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu huu.Viongozi hao ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi na Mkurugenzi Mtendaji wa JOC Bw. Qin Mengwei ambao kwa pamoja wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa.

Waziri Mkuu amekutana na viongozi hao leo (Jumatatu, Februari 12, 2018) jijini Dar es Salaam na amesema kwamba wakulima waliitikia wito wa Serikali wa kufufua zao hilo, hivyo mwaka huu wanatarajia kupata mavuno mengi.Waziri Mkuu amewataka viongozi hao wajiandae kununua pamba nyingi kwa sababau mwaka huu wakulima wamelima pamba ya kutosha baada ya Serikali kuwahamasiha waongeze uzalishaji kwa kuwa kuna soko la uhakika.

Amesema hatua hiyo imekuja baada ya Rais Dkt. John Magufuli kutoa maelekezo ya uhamasishaji wa kilimo hasa mazao makuu ya biashara, tayari tija imeanza kuonekana ambapo zao la korosho limepata mafanikio makubwa na sasa linafuatia zao la pamba.

Waziri Mkuu amesema Serikali inashiriki kikamilifu katika usimamizi wa zao la pamba kuanzia hatua za maandalizi ya shamba kwa wakulima kuelekezwa kulima kitaalam, upatikanaji wa pembejeo hadi masoko, hivyo amewaalika viongozi hao kushiriki katika mkutano utakaowakutanisha wafanyabiashara wote wa zao hilo.

“Mimi mwenyewe mwezi huu nitakuwa na ziara ya kikazi mkoani Mwanza, kwa hiyo tarehe 21, Februari, nimeitisha mkutano wa wafanyabiashara wote wa pamba nchini iwe ni wanaosokota nyuzi, kuchambua pamba au kukamua mbegu za pamba, ili mradi wanajihusisha na pamba nanyi naomba muwepo”.

Waziri Mkuu amesema Serikali imefurahishwa na uamuzi wao wa kutaka kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu huu kwani ni faraja kwa Taifa kwa sababu wakulima walipunguza uzalishaji baada ya kukosa soko la uhakika.Kwa upande wao, Bw. Pardesi na Bw. Qin wamemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba kampuni zao zinauwezo wa kununua pamba yote inayozalishwa nchini na kuichakata katika viwanda vyao na kutengeneza nyuzi na nguo zitakazouzwa nchini kwa bei nafuu.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, FEBRUARI 12, 2018.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU AKUTANA NA WAKURUGENZI WA KAMPUNI YA NAMERA NA JOC
WAZIRI MKUU AKUTANA NA WAKURUGENZI WA KAMPUNI YA NAMERA NA JOC
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhJveBJQfowaRDfdz8Wt1MQSAh-5Gx44pPY7hxIXb3KSEVTHZRzJc0tGjMIzAS18I5rI4CKYqoedPpRVVwTBKLrpl797AEzgdINp-RBLQA0Z3QS7mFXKT-LmwgZ1m7mw0ZK0PxmZSKmAVt9/s640/PMO_7716-768x598.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhJveBJQfowaRDfdz8Wt1MQSAh-5Gx44pPY7hxIXb3KSEVTHZRzJc0tGjMIzAS18I5rI4CKYqoedPpRVVwTBKLrpl797AEzgdINp-RBLQA0Z3QS7mFXKT-LmwgZ1m7mw0ZK0PxmZSKmAVt9/s72-c/PMO_7716-768x598.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/02/waziri-mkuu-akutana-na-wakurugenzi-wa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/waziri-mkuu-akutana-na-wakurugenzi-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy