WAZIRI LUKUVI APIGA MARUFUKU WATHAMINI WANAOFANYA UTHAMINI NJE YA SERIKALI
HomeJamii

WAZIRI LUKUVI APIGA MARUFUKU WATHAMINI WANAOFANYA UTHAMINI NJE YA SERIKALI

Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, William Lukuvi leo amezindua rasmi bodi ya wathamini ambayo imeundwa kwa mujibu wa she...

WAZIRI MAHIGA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABOLOZI WA CUBA, ZAMBIA NA BURUNDI
WAZIRI MKUU AZUNGUMZA NA MABALOZI, AWATAKA WAKATAFUTE WAWEKEZAJI
HABARI NJEMA KWA WANA UKEREWE, KUPATA UMEME JUNI 2018


Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, William Lukuvi leo amezindua rasmi bodi ya wathamini ambayo imeundwa kwa mujibu wa sheria ya uthamini na usajili wa wathamini ya mwaka 2016 ambayo imeanza kutumika rasmi Januari mwaka huu. 

Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri Lukuvi amesema kwa mujibu wa sheria wajumbe wa bodi ni lazima kutoka katika taasisi mbalimbali ikiwemo Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, ofisi ya rais TAMISEMI, vyuo vikuu, vyama vya kitaluma vya wathamini, ofisi ya mwanasheria mkuu, taasisi ya mabenki, na bodi ya wakaguzi na wahasibu(NBAA) na kuongeza kuwa kwa muundo huo bodi inahitaji mpana mkubwa wa uwakilishi ili kutekeleza majukumu yake kwa urahisi. 

Pia amesema kuwa serikali iliona umuhimu wa kuwa na chombo madhubuti kwa ajili ya kusimamia taaluma ya uthamini baada ya kuonekana kuwa kumekuwa na ongezeko la udanganyifu katika kazi ya uthamini hasa kwenye miradi ya serikali na ya mikopo katika mabenki baada ya Kazi hiyo ya uthamini kuwa chini ya Baraza la wapima ardhi na wathamini (NCPS). 

Aidha ameweka wazi kwamba tasnia ya uthamini ni ya muhimu sana kwa ustawi wa uchumi kwa ujumla kwani Kazi za wathamini zunahusiana na ukadiriaji wa Mali kwa malengo mbalimbali ikiwemo kuweka rehani za mikopo kwenye mabenki, kodi za ardhi na majengo, mahesabu ya makampuni binafsi na taasisi za serikali hivyo kama Kazi hiyo haitafanywa kwa umakimi na uadilifu inaweza kuchangia kuanguka kwa uchumi na hata watu kupoteza mali sambamba na kusababisha migogoro ya ardhi. 

Pia amebainisha masuala ambayo yanatakiwa kufanyiwa Kazi kwa haraka ili kufuta dosari zilizopo na kusema kuwa ni kudhibiti kazi ya uthamini kufanywa na watu wasiosajiliwa na bodi na wale wasio ma taaluma ya uthamini, kudhibiti udanganyifu wa thamani kwa ajili ya uthamini kwa ajili ya fidia, kodi na mikopo ya benki, kutoa na kusimamia mafunzo ya Mara kwa Mara kwa wathamini pamoja na kuandaa viwango na miongozo ya uthamini. 

Pia Waziri ametoa onyo kwa wathamini wanaotumia udanganyifu pindi wanapofanya tathimini pamoja na wale wanaofanya kazi ya uthamini nje ya kazi au miradi ya serikali na kuwaomba wathamini wote kujisajili kwenye bodi ya wathamini ili watambulike na kupata usajili unaotambulika. 

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya usajili wa wathamini Dkt.Cletus E.Ndjovu amesema kuwa bodi ya wathamini ni muhimu sana katika suala la maendeleo na kuahidi kwamba watafanya kazi kwa weledi na kwa kufuata sheria ya bodi ya uthamini bila kumwonea mtu aibu ili kuleta heshima katika taaluma ya uthamini.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI LUKUVI APIGA MARUFUKU WATHAMINI WANAOFANYA UTHAMINI NJE YA SERIKALI
WAZIRI LUKUVI APIGA MARUFUKU WATHAMINI WANAOFANYA UTHAMINI NJE YA SERIKALI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjqXSqf_Q6zDK5Rp5zqojvFLnR5Zexr304EWvGBXT7fEyPemKNT8sv7fL3AloOv7D_fQlJrSbt2ofoasCZlI7Ouw0a1fHcHZB-gATUcvobyV5ez_pyOJH1uY5ZEb2ceSAruWcn4ni52slCq/s400/MMG_2917.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjqXSqf_Q6zDK5Rp5zqojvFLnR5Zexr304EWvGBXT7fEyPemKNT8sv7fL3AloOv7D_fQlJrSbt2ofoasCZlI7Ouw0a1fHcHZB-gATUcvobyV5ez_pyOJH1uY5ZEb2ceSAruWcn4ni52slCq/s72-c/MMG_2917.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/02/waziri-lukuvi-apiga-marufuku-wathamini.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/waziri-lukuvi-apiga-marufuku-wathamini.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy