SERIKALI YASISITIZA UWAZI SHUGHULI ZA MADINI
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (katikati) akizungumza jambo wakati wa mkutano na Balozi wa Canada nchini, Ian Myles (kulia) na Mshauri masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii kwenye Tasnia ya Uziduaji kutoka Serikali ya Canada, Jeffrey Davidson (kushoto).

HomeJamii

SERIKALI YASISITIZA UWAZI SHUGHULI ZA MADINI

Kampuni za Madini nchini zimetakiwa kufanya shughuli zake kwa uwazi sambamba na kufuata Sheria za nchi ili kuepuka migongano. Wito huo ...

MBUNGE MSTAAFU ABBAS MTEMVU AFUNGUA MKUTANO WA VICOBA NA BENKI YA KIISLAMU YA AMANA PTA DAR ES SALAAM
WAZIRI MHAGAMA ARIDHISHWA NA JITIHADA ZA KUREJESHA MIUNDOMBINU MKOANI KAGERA
KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI AJITAMBULISHA KWA RAIS WA ZANZIBAR, DKT. ALI MOHAMMED SHEIN


Kampuni za Madini nchini zimetakiwa kufanya shughuli zake kwa uwazi sambamba na kufuata Sheria za nchi ili kuepuka migongano.
Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam Januari 29, 2018 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila kwenye mkutano na Balozi wa Canada nchini, Ian Myles aliyeambatana na Mshauri masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii kwenye Tasnia ya Uziduaji kutoka Serikali ya Canada, Jeffrey Davidson.
Ujumbe huo ulimtembelea Katibu Mkuu Msanjila kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali kwenye Sekta ya Madini ikiwemo suala la Sheria ya Madini, masuala ya uwajibikaji kwa jamii (CSR) yanayofanywa na kampuni mbalimbali zikiwemo za kutoka nchini Canada na matarajio ya Serikali kwa kampuni (wawekezaji).
Profesa Msanjila alisisitiza kuwa kampuni zinazofanya shughuli zake nchini zinalazimika kufuata taratibu na sheria za nchi ili kujijengea mazingira rafiki ya utekelezaji wa shughuli husika.
Alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha Sekta ya Madini inanufaisha Taifa kwa ujumla sambamba na wawekezaji na alibainisha kwamba lengo hilo litafikiwa ikiwa kampuni husika zitatekeleza wajibu wake kwa uwazi kulingana na matakwa ya sheria.
“Kampuni zinazojihusisha na shuguli za madini zinapaswa kufanya shughuli zake kwa usahihi na uwazi,” alisisitiza Profesa Msanjila.
Aidha, Profesa Msanjila alisisitiza kuwa kampuni zinazojihusisha na shughuli za madini nchini, zinapaswa kupata taarifa sahihi kutoka kwa Wataalam waliopo Serikalini ili kupata mwelekeo sahihi wa dhamira ya Serikali.
“Kampuni zinatakiwa kupata taarifa sahihi kutoka kwa vyanzo sahihi ili kufanya shughuli zake kwa usahihi,” alisisitiza Profesa Msanjila.
Profesa Msanjila vilevile alizungumzia dhamira ya Serikali ya kuhakikisha madini yanayochimbwa nchini yanaongezwa thamani kabla hayajasafirishwa nje ili kukuza uchumi wa Taifa.
“Madini yakiongezwa thamani hapa nchini, faida ni nyingi ikiwemo ajira na pia mapato yataongezeka kwani tutakuwa tumeelewa thamani halisi ya madini husika, kabla hayajasafirishwa,” alisema.
Ili kufikia dhamira hiyo, Profesa Msanjila alisema Serikali ipo kwenye mazungumzo na kampuni zilizoonyesha nia ya kujenga viwanda vya kuyeyusha na kusafisha madini (smelting and refining).
Mbali na hilo, Profesa Msanjila alizungumzia suala la uwezeshaji wachimbaji wadogo wa madini ambapo alisema Serikali imedhamiria kuhakikisha kwamba wananufaika ipasavyo na shughuli zao sambamba na mchango wao kwenye pato la Taifa kuonekana.
Alielezea jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika kuwawezesha wachimbaji wadogo ikiwemo uanzishaji wa vituo vya mafunzo vya mfano (centre of excellence) ambavyo alivitaja baadhi yake kuwa ni Kituo cha Tanga, Geita na Mtwara.
Kwa upande wake Balozi Myles alisema ni muhimu Serikali, Wawekezaji na Jamii kwa ujumla kushirikiana na pia kuwa na lengo la wazi la namna ya kunufaika kutokana na Sekta ya Madini.
Naye Davidson aliahidi kuzungumza na kampuni za Canada kuelezea matarajio ya Serikali kwao kwa namna mbalimbali ikiwemo suala la sheria, uwajibikaji kwa jamii, mazingira na michango mbalimbali ya kampuni kwa maendeleo ya jamii.
“Nitawakumbusha kwamba wanawajibika si kwa wanahisa wao peke yake bali pia kwa jamii wanapofanyia shughuli zao,” alisema Davidson.
Mkutano wa Katibu Mkuu wa Madini na Balozi wa Canada nchini ulihudhuriwa na watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Madini akiwemo Kamishna wa Madini ambaye pia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kamisheni ya Madini, Profesa Shukrani Manya.


Watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Madini na Ubalozi wa Canada nchini Tanzania wakifuatilia majadiliano kwenye mkutano wa Katibu Mkuu Madini na Balozi wa Canada (hawapo pichani). Kushoto ni Kamishna wa Madini ambaye pia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kamisheni ya Madini, Profesa Shukrani Manya na kulia ni Kamishna wa Biashara Ubalozi wa Canada nchini, Anita Kundy. Wengine ni Maafisa kutoa Wizara ya Madini.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (kulia) akimsikiliza Mshauri masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii kwenye Tasnia ya Uziduaji kutoka Serikali ya Canada, Jeffrey Davidson (katikati). Kushoto ni Balozi wa Canada nchini, Ian Myles (kulia)

Mshauri masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii kwenye Tasnia ya Uziduaji kutoka Serikali ya Canada, Jeffrey Davidson (kushoto) akizungumza wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (katikati). Kulia ni Balozi wa Canada nchini, Ian Myles.


Balozi wa Canada nchini, Ian Myles (kushoto) akizungumza wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (kulia). Katikati ni Mshauri masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii kwenye Tasnia ya Uziduaji kutoka Serikali ya Canada, Jeffrey Davidson.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (wa pili kulia) mara baada ya kumalizika kwa mkutano na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Ian Myles (katikati). Kulia ni Kamishna wa Madini ambaye pia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kamisheni ya Madini, Profesa Shukrani Manya. Kutoka kushoto ni Mshauri masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii kwenye Tasnia ya Uziduaji kutoka Serikali ya Canada, Jeffrey Davidson na Kamishna wa Biashara Ubalozi wa Canada nchini, Anita Kundy.




Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SERIKALI YASISITIZA UWAZI SHUGHULI ZA MADINI
SERIKALI YASISITIZA UWAZI SHUGHULI ZA MADINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi57iQrvYw3Px_1uEs7UWxOwaUCO_khyVo9ZkhfJWjwwdAbtrPLSQFw1CHqut1pC40Wc4LDczdTAuFxYMJQ-oMwofkrc76ywNnuIuN0kcbltxpbp6Ocx7GvZkXkVonS0ETLwe3F2qdlkTA/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi57iQrvYw3Px_1uEs7UWxOwaUCO_khyVo9ZkhfJWjwwdAbtrPLSQFw1CHqut1pC40Wc4LDczdTAuFxYMJQ-oMwofkrc76ywNnuIuN0kcbltxpbp6Ocx7GvZkXkVonS0ETLwe3F2qdlkTA/s72-c/1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/01/serikali-yasisitiza-uwazi-shughuli-za.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/01/serikali-yasisitiza-uwazi-shughuli-za.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy