Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akinukuu hoja za wajumbe wa k...

Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama akinukuu hoja za wajumbe wa kikao cha Tathimini ya
Utekelezaji wa Miradi ya Kukabili na Kurejesha hali kwa maeneo
yaliyoathiriwa na tetemeko Mkoani Kagera kilichofanyika Ukumbi wa
Mikutano Ofisi ya Mkoa Machi 18, 2017 kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt.Hamisi Mwinyimvua.
Baadhi
ya wajumbe wa kikao cha Tathimini ya Utekelezaji wa Miradi ya Kukabili
na Kurejesha hali kwa maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi
wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na
Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa
kujadili na kupokea taarifa hiyo mkoani Kagera.
Mkuu
wa Wilaya ya Kagera Mhe. Deodatus Kinawilo akichangia hoja wakati wa
kikao cha Tathimini ya Utekelezaji ya Kukabili na Kurejesha hali baada
ya athari za tetemeko mkoani Kagera.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI
MKUU).
……………………….
Na. Mwandishi Wetu
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama ameupongeza uongozi wa mkoa wa Kagera kwa
hatua iliyofikiwa katika kurejesha miundombinu mbalimbali iliyoathiriwa
na tetemeko la ardhi lililotokea Septemba10 mwaka 2016 katika Mkoa wa
Kagera linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa 5.9 katika vipimo vya Richter.
Mhe.
Mhagama alionesha kuridhishwa kwake baada ya kufanya ziara Mkoani hapo
mapema wiki hii kwa lengo la kutathimini utekelezaji unaoendelea katika
kurejesha miundombinu ili wananchi waendelee kutumia huduma hizo kama
kawaida.
Katika
ziara hiyo, Waziri Mhagama alitembelea Shule ya Sekondari Nyakato,
Ihumo na Omumwani, Kituo cha Afya cha Kabyaile-Ishozi na Kituo cha
Kulelea Wazee cha Kiilima na kubaini kuwa ujenzi wa Kituo kipya cha Afya
cha Kabyaile-Ishozi ambacho kimefikia asilimi 80 ambapo kimetumia kiasi
cha shilingi 381, 506, 079.00.
“Nikiri
kwamba ukiacha baadhi ya mapungufu kwa watendaji wachache, wengi
mmetupa ushirikiano mzuri kwa kulinganisha hali ilivyokuwa kwa kuangalia
tukio lilivyotokea na hadi hatua za kukabili hatimaye kurejesha
hali.”Alisema Waziri
Aliendelea
kushukuru ushirikiano mzuri uliopo katika kutekeleza majukumu hatimaye
kufikia lengo “Kama sio ushirikiano wa pamoja kati ya Ofisi ya Waziri
Mkuu, Ofisi ya Mkoa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania huwenda tusingefika
hapa hivyo tuna kila sababu ya kupongeza juhudi hizi kwa niaba ya
Serikali hususani Ofisi ya Waziri Mkuu tumefarijika kwa ushirikiano
wenu”
Pamoja
na pongezi hizo, Waziri alimtaka Katibu Tawala wa Mkoa Kamishna Diwani
Athuman kuendelea kuzingatia taratibu za manunuzi na kila eneo
linalofanyiwa kazi kufuata taratibu, kanunuzi zilizopo kwani kwa atakaye
kiuka sheria na taratibu hakutakuwa na msamaha.”Hakutakuwa na msamaha
kwa yeyote atakayefanya uzembe lazima sheria zichukue mkondo wake hakuna
kuoneana aibu” Alisisitiza waziri.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya Mhe. Deogratius Kinawilo alipongeza kwa
kukiri kuwa kazi inayoendelea ya kurejesha hali imefanyika kwa umakini
mkubwa. “Tumefanya kazi kwa umakini mkubwa na kila mmoja alikaa kwenye
nafasi yake hivyo niendelee kuwaomba watendaji wote kufuata sheria na
kutekeleza yote yanayotupasa ili kuokoa mazingira ya wanakagera kwa
ujumla”
Waziri
mhagama alieleza pia pamoja na jitihada zote ifike mahali kile
kilichokusudiwa kitimie na miradi yote ifikapo mwezi Mei mwaka huu
imekamilika” Tuendelee kutekeleza majukumu yetu katika zoezi la
kurejesha hali ili ifikapo mwezi Mei angalau asilimia 80 iwe
imekamiliza” Alisema waziri
Ziara
hiyo ilikuwa ni moja ya utekelezaji wa maagizo ya Mhe.Rais John Pombe
Magufuli aliyoyatoa wakati wa ziara yake Januari mwaka huu na kuiagiza
Ofisi ya Waziri Mkuu kufanya tathimini za shughuli zote wakati wa
kukabili na urejesha hali baada ya kutokea kwa Tetemeko hilo.
COMMENTS