SWAI WA JNIA AAGWA ASAFIRIWA ROMBO KWA MAZISHI
Mchungaji Augustino Simalenga wa Kanisa la TAG Kivule leo maeneo ya Kitunda akiombea mwili wa marehemu Jerome Swai aliyekuwa Fundi Sanifu Mkuu wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), kabla ya kusafirishwa kwa mazishi yatakayofanyika kesho wilayani  ya Rombo.
HomeJamii

SWAI WA JNIA AAGWA ASAFIRIWA ROMBO KWA MAZISHI

MCHUNGAJI SIMALENGA AWATAKA WANADAMU KUJIANDAA KABLA YA KIFO Na Mwandishi Wetu MCHUNGAJI wa Kanisa la TAG Kivule, Augustino Simaleng...

SERIKALI KUPITIA DAWASA KUJENGA MITAMBO MITATU YA KISASA YA KUCHAKATA MAJI TAKA JIJINI DAR ES SALAAM
NAIBU WAZIRI WA MADINI MHE BITEKO AUTAKA UONGOZI WA CHUO CHA MADINI DODOMA KUJITATHIMINI
MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI


MCHUNGAJI SIMALENGA AWATAKA WANADAMU KUJIANDAA KABLA YA KIFO

Na Mwandishi Wetu
MCHUNGAJI wa Kanisa la TAG Kivule, Augustino Simalenga amewataka wanadamu kujiandaa na kumrudia muumba wao kwani hawajui siku wala saa watakapokufa.

Alitoa kauli hiyo leo kwenye misa ya kumuaga marehemu Jerome Swai aliyekuwa Fundi Sanifu Mkuu wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), iliyofanyika nyumbani kwake maeneo ya Kitunda, ambapo amewataka watu kujiandaa mapema kwa kuwa hawajui watakapokwenda baada ya kifo.

“Neno la Mungu linatukumbusha kuwa tujiandae mapema, ndugu yetu Jerome ameshamaliza kazi, tunatakiwa kujitafakari sisi hatima yetu itakuwaje, kwani wapo waliolala mauti Biblia inasema hao wanapumzika wakisubiri siku atakaporudi Mwana wa Adam atakuja kuwachukua wote waliohai na wale waliokufa wakimuamini Kristu watafufuliwa kwanza ili kwa pamoja wamlaki Bwana wao mawinguni,” alisema Mchungaji Semalenga.

Alisema kila mtu atafakari maisha ya hapa duniani kwani mlango wa kutokea hapa duniani aidha ni kifo au siku Bwana atakapokuja kuchukua watu wake, hivyo ni vyema kujiandaa kwa kutafakari maisha baada ya hapa kwa sasa kuanza kujitengenezea hazina mbinguni.

“Ukisoma kitabu cha Mhubiri sura ya 3 utaona Mungu ameweka kila kitu na wakati wake, upo wakati wa kula na wakati wa kusema, wakati wa kunyamaza, wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa kila kitu kinawakati hata sisi tuliohai ni wakati wetu kuwa hai bali utafika wakati hatutaweza kuwa hai siku zote, na kila jambo lina mwanzo na mwisho, lakini mwisho wa jambo unatengenezwa wakati wa sasa kama maisha yetu ya sasa hatufikiri mwisho basi tukifika mwisho tutakuwa watu wa kujuta, watu wa kuomboleza na lakini sasa Mungu anatupa nafasi ya kuyakabili mambo yanayokuja na hatima ya maisha yetu,” alisisitiza.

Alisema katika kitabu cha Zabuni, kinasema binadamu amepewa maisha mafupi na machache, na kuishi ni miaka 70 na wachache wanaweza kuishi zaidi ya hiyo, ambapo ni tofauti na wanadamu wa kwanza waliishi miaka 100 ambayo nayo yalikuwa mafupi. Hata hivyo alisema baada ya kifo yapo maisha ya milele, ambayo mwanadamu anatakiwa kuyatafakari sasa kwa kujiwekea hazina itakayomwezesha kuishi vyema mbinguni.
Mchungaji Simalenga alisema amefanya utafiti katika huduma anazotoa lakini amegundua hakuna mwanadamu anayetaka kwenda jehanamu, hata asiyefanya ibada kwa Mungu anamatumaini ya kwenda mahala pema peponi.
“Mungu ameweka utaratibu na Mwanadamu akiuufuata ndio atafikia kwenye ule mpango ambao Mungu ameuweka, sasa kama hataki kuufuata anajikuta siku za maisha yake atajikuta mahala asipotaka kwa kilio, kujuta na kuomboleza, kwani alikuwa akipuuzia na kuona mambo ya Kimungu ni ya kiduni na watu maskini na wachini, wakati ni mambo ya msingi kuliko kitu chochote duniani,” alisema Mchungaji Simalenga.    
Naye Afisa Utumishi Mkuu wa JNIA, Bw. Priscus Mkawe alisema marehemu Swai ameacha pengo kubwa kutokana na umahiri wake katika utendaji kazi wake uliotukuka.
“Marehemu Swai alikuwa mmoja wa wafanyakazi wa kipekee aliyefanya kazi kwa bidii na kujituma na kutokana na uchapakazi wake aliwahi kuchaguliwa kuwa mfanyakazi hodari kuanzia mwaka 2001, 2003 na 2017, hivyo JNIA na TAA kwa ujumla tumempoteza mfanyakazi hodari sana,” alisema Priscus.




Msemaji wa familia ya marehemu Jerome Swai aliyekuwa Fundi Sanifu Mkuu wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Silvester Shayo (kulia) akitoa shukrani  kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Wafanyakazi wa TAA na watu wote walioshiriki kwenye msiba huo. Marehemu Swai atazikwa kesho wilaya ya Rombo.

Kaimu Mkurugenzi wa  Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka akiaga mwili wa aliyekuwa Fundi Sanifu Mkuu wa JNIA, Bw. Jerome Swai, ambaye atazikwa kesho wilayani Rombo.

Afisa Utumishi Mkuu wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Priscus Mkawe akisoma wasifu wa marehemu Jerome Swai aliyekuwa Fundi Sanifu Mkuu wa JNIA, kabla ya kuagwa nyumbani kwake Kitunda na kusafirishwa kwenda Rombo kwa mazishi yatakayofanyika kesho.

Honoratha Emmilian ambaye ni mke wa marehemu Jerome Swai aliyekuwa Fundi Sanifu Mkuu wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akilia kwa uchungu wakati wa kuuaga mwili wa mumewe nyumbani kwake Kitunda. Marehemu atazikwa kesho wilayani Rombo.

Ndugu wa marehemu Jerome Swai wakiuaga mwili wa mpendwa wao leo nyumbani kwake Kitunda, ambapo anatarajiwa kuzikwa kesho wilayani Rombo. Swai alikuwa Fundi Sanifu Mkuu wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA)

Mkurugenzi wa zamani wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Prosper Tesha (mwenye miwani mbele) akijumuika na waombolezaji kwenye msiba wa aliyekuwa Fundi Sanifu Mkuu wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Jerome Swai aliyefariki Jumatatu ya wiki hii na atazikwa kesho wilayani Rombo

Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Fundi Sanifu Mkuu wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Jerome Swai likipandishwa ndani ya basi tayari kwa safari ya kwenda Rombo kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho. Marehemu aliajiriwa mwaka 1984.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SWAI WA JNIA AAGWA ASAFIRIWA ROMBO KWA MAZISHI
SWAI WA JNIA AAGWA ASAFIRIWA ROMBO KWA MAZISHI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi2ScpcmMs1yZXLWmZJd74GweVyW9qRn8nwJ0BleT5cxPFpnYJ8X0OAg96TTDhsILs-VExwQZwOx0GvQij1ZCvYqzs2GIQ-EkDzyk_N3I2aHhYU5CMwfzx_KY7QEJZM5tkhKZAyqJCaRMs/s640/swai-1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi2ScpcmMs1yZXLWmZJd74GweVyW9qRn8nwJ0BleT5cxPFpnYJ8X0OAg96TTDhsILs-VExwQZwOx0GvQij1ZCvYqzs2GIQ-EkDzyk_N3I2aHhYU5CMwfzx_KY7QEJZM5tkhKZAyqJCaRMs/s72-c/swai-1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/02/swai-wa-jnia-aagwa-asafiriwa-rombo-kwa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/swai-wa-jnia-aagwa-asafiriwa-rombo-kwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy