WAZIRI MPINA AAGIZA MIKATABA YA WAWEKEZAJI WA VITALU VYA RANCHI YA TAIFA VYENYE JUMLA YA HEKTA 68238 KUVUNJWA MARA MOJA
HomeBiashara

WAZIRI MPINA AAGIZA MIKATABA YA WAWEKEZAJI WA VITALU VYA RANCHI YA TAIFA VYENYE JUMLA YA HEKTA 68238 KUVUNJWA MARA MOJA

Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye Kofia) akiwa kwenye picha pamoja na Viongozi wa Wilaya ya Mvomero na Viongozi ...

WATATU WALAMBA MAMBILIONI TA TATUMZUKA JUMAPILI JACKPOT
ALICHOKIZUNGUMZA DKT. NDUGULILE BAADA YA KUWATEMBELEA WANAWAKE WAJASILIAMALI WA MANISPAA YA MBOZI MKOANI SONGWE.
MWENYEKITI WA BODI YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA (TPC), DK. HARUN KONDO ATOA SALAMU ZAKE KWA MAADHIMISHO YA SIKU YA POSTA DUNIANI


Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye Kofia) akiwa kwenye picha pamoja na Viongozi wa Wilaya ya Mvomero na Viongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania alipotembelea ranchi ya Dakawa jana.


Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye Kofia) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Muhamed Utaly kulia akitoa maelezo ya kuhusu eneo la hekta 20000 zilizoshindwa kuendelezwa na mwekezaji Mtibwa Sugar kwa lengo la ufugaji. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo bwana Stan Rau hapo jana.

Meneja wa ranchi ya Mifugo ya Mkata, Iddi Sadalah akimuonyesha Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye Kofia) banda la Mbuzi linalokadiriwa kuchukua mbuzi 800 kwa wakati mmoja katika ranchi ya Mkata jana.




……………….


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina ameagiza Mtendaji Mkuu wa Ranchi za Mifugo za Taifa, Profesa Philemoni Wambura kuvunja mikataba ya wawekezaji wa vitalu vyenye jumla ya hekta 68,238 kwenye ranchi ya Mkata na Dakawa ndani ya mwezi mmoja baada kushindwa kuviendeleza vitalu vya ranchi na kushindwa kulipia kwa muda mrefu.Mpina ameyasema hayo jana wakati alipotembelea katika ranchi ya Mkata na Dakawa kwa lengo la kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika katika ranchi hizo.


Amezitaja kampuni za wawekezaji ambazo zilizomilikishwa vitalu zinatakiwa kuvunja mkataba kwa kushindwa kuendeleza upande wa ranchi ya Mkata katika Wilaya ya Kilosa kuwa ni pamoja na Kadolo Farm Company Ltd kitalu namba 418 yenye hekta 4005,Bagamoyo Farm kitalu namba 419 yenye hekta 3672.96, A to Z Animal Feeds Company Ltd kitalu namba 420 yenye hekta 3692.97 na Ereto Livestock Keepers kitalu namba 422 yenye hekta 4020.54.


Katika Wilaya ya Mvomero kampuni zilizoshindwa kuendeleza vitalu ni pamoja na kampuni ya Overland kitalu namba 415 yenye hekta19446.28, Katenda yenye hekta 2500, Mollel yenye hekta 2500 na Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa (Mtibwa Sugar) chenye hekta 20000 walizomilikishwa toka mwaka 1999 na kushindwa kukiendeleza na kukilipia kwa miaka 18.


Mpina amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kilosa kumaliza mara moja migogoro inayoendelea baina ya wakulima na wafugaji. Aidha Waziri Mpina amemtaka Diwani wa kata yaTwatwatwa, Katibu Tawala wa Halimashauri ya Wilaya ya Kilosa pamoja na jamii ya wafugaji kumaliza migogoro inayowasumbua kwa muda mrefu kwa njia ya mazungumzo kabla ya kukimbilia muhimili wa mahakama bila sababu yoyote.


Mpina amesema kama vyombo vya Serikali vingetumika vizuri kuanzia ngazi ya kijiji kungepunguza migogoro ya wakulima na wafugaji katika wilaya hiyo. Wilaya ya Kilosa ni miongoni mwa Wilaya zinaongoza kwa kuwa na migogoro mingi baina ya wakulima na wafugaji hapa nchini.


Kwa upande mwingine, Waziri Mpina amezitaka Halimashauri zote nchini kutotunga sheria kandamizi dhidi ya wafugaji. Akitolea mfano, wa sheria ndogo ya Halimashauri ya Mvomero ya kutoza faini ya shilingi 25, 000/=kwa kila mfugo kuingia katika Wilaya hiyo bila kufuata taratibu badala ya shilingi elfu kumi iliyoelekezwa katika Sheria ya Magonjwa ya Wanyama namba 17 ya Mwaka 2003.


Kwa upande wake, Katibu Mkuu Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) Magembe Makoye amesema upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya wafugaji kutasaidia kuondoa migogoro baina ya pande hizo na kuendelezwa kwa ranchi hizo za taifa kutawasaidia wafugaji kupata shamba darasa litakalo wasaidia kufuga kwa kisasa na kupata mbegu bora za mifugo.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MPINA AAGIZA MIKATABA YA WAWEKEZAJI WA VITALU VYA RANCHI YA TAIFA VYENYE JUMLA YA HEKTA 68238 KUVUNJWA MARA MOJA
WAZIRI MPINA AAGIZA MIKATABA YA WAWEKEZAJI WA VITALU VYA RANCHI YA TAIFA VYENYE JUMLA YA HEKTA 68238 KUVUNJWA MARA MOJA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjPTAujp7ejtiROoXLDjv4F36XyJLs_9oKLCOaEyCkDrEzO5Df-gfV8Eww02Fb45gY2xqHfOfCm5N4rh8WkgXbvcrhWNYKc6mRFlBVWTivu7KEPWHe-L0FRAufSyO5ze1i6Wl0DkyXuJq1h/s640/a.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjPTAujp7ejtiROoXLDjv4F36XyJLs_9oKLCOaEyCkDrEzO5Df-gfV8Eww02Fb45gY2xqHfOfCm5N4rh8WkgXbvcrhWNYKc6mRFlBVWTivu7KEPWHe-L0FRAufSyO5ze1i6Wl0DkyXuJq1h/s72-c/a.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/12/waziri-mpina-aagiza-mikataba-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/waziri-mpina-aagiza-mikataba-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy