Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii YALI Regional Leadership Centre ya Nchini imedhamiria kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vija...
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii
YALI
Regional Leadership Centre ya Nchini imedhamiria kutoa elimu ya
ujasiriamali kwa vijana Tanzania Bara na Visiwani kwa kumualika moja ya
waandamizi wa masuala ya ujasiriamali kutoka nchini Jordan Laith Al
Qassam ili kutoa mafunzo mbalimbali kwa kuhakikisha wanapata nafasi za
kujiajiri na kuongeza pato la taifa.
Akizugumza kabla ya kuanza semina hiyo,Muà ndaaji wa Semina hiyo
Fabian Shayo amesema kuwa mafunzo hayo yajulikanayo kama Blue Ocean
Strategy yatahusisha zaidi masuala ya ujasiriamali hususani kwa vijana
na mkufunzi Al Qassama ambaye amebobea katika masuala hayo atatoa elimu
kwa vijana waliojitokeza.
Shayo amesema Blue Ocean Strategy imeweza kusaidia watu wengi
hususani vijana katika masuala ya ujasiriamali na hata kuanzisha
makampuni duniani kote pia imeweza kutengeneza soko la kibiashafa na
kukuza faida.
Mkufunzi wa mafunzo hayo, Al Qassama ambaye ni mmoja ya waandamizi
wa kiwanda cha Jordan ICT na kukiwezesha kuwa moja ya makampuni makubwa
duniani amesena kuwa vijana wengi wanaamini kuwa fedha ndiyo kila kitu
na kushindwa kuelewa kuwa mawazo yanaweza kuwa msaada kwao.
Blue Ocean Strategy itaendeshwa katika vipindi vitatu tofauti kwa
bara na visiwani kwa ajili ya kuwapatia elimu vijana kwa watakaoleta
mabadiliko na maendeleo kwenye sekta ya ujasiriamali kupata fursa za
ajira na kukuza kiwango cha maendeleo ya kiuchumi katika taifa.
Katika ukanda wa Afrika Mashariki, Vijana waliowahi kushiriki
semina hiyo(Alumni)
wametumia fursa hii kuwasaidia vijana wenzao ili
kuweza kuangalia wanakwamuka vipi kiuchumi kwa kupitia njia ya
ujasiriamali.
Mwenyekiti wa kamati ya uandaaji wa mafunzo hayo, Fabian Shayo
akizungumza na waandishi wa habari juu ya mikakati yao ya kusaidia
vijana kujikwamua kiuchumi kwa kutumia sera ya ujasiriamali. Kulia ni
Mkufunzi Laith Al Qassam na kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya fedha
Fortunatus Eklklesiah.
Mkufunzi Laith Al Qassam akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na mafunzo hayo ya ujasiriamali kwa vijana na nini wanatakiwa
kufanya ili kuondoa dhana ya kuajiriwa au kuamini fedha zinaweza kufanya
kila kitu. Kulia ni Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano, Khalila Mbowe
na kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya uandaaji wa mafunzo hayo, Fabian
Shayo.
Mkufunzi wa Semina hiyo Laith Al Qassam akitoa mafunzo ya
ujasiriamali kwa vijana waliojitokeza yaliyoendeshwa na YALI Regional
Leadership Centre kwa ukanda wa Afrika Mashariki.
COMMENTS