MAWAZIRI UGANDA WAVUTIWA NA UCHIMBAJI MDOGO WA DHAHABU MKOANI GEITA
HomeBiashara

MAWAZIRI UGANDA WAVUTIWA NA UCHIMBAJI MDOGO WA DHAHABU MKOANI GEITA

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel wa kwanza kulia akiwaongoza Mawaziri kutoka Uganda kwenda kukagua shughuli za uchimbaji mdogo...

TIGO YACHANGIA KATIKA UKUAJI WA TEKNOLOJIA NA HUDUMA ZA KIFEDHA KWA NJIA YA MTANDAO NCHINI
KAMPUNI YA TRUMARK YAHITIMU MAFUNZO YA UBORESHAJI UFANISI TOKA NETHERLANDS
MBEGU BORA ZA MIGOMBA, VIAZI LISHE NA MIHOGO KUWAKOMBOA WAKULIMA MKOANI KAGERA





Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel wa kwanza kulia akiwaongoza Mawaziri kutoka Uganda kwenda kukagua shughuli za uchimbaji mdogo Lwamgasa Wilayani Geita.

NA MAGESA JUMAPILI
MAWAZIRI wa nne wa Wizara za Madini, Uchumi, Mambo ya Ndani na Nje wa Serikali ya Jamhuri ya Uganda wamewasili Mkoani Geita kujifunza namna Serikali ya Tanzania ilivyofanikiwa kuwezesha na kuendeleza Wachimbaji Wadogo wa Dhahabu ili kukuza Sekta hiyo nchini kwao.
Akizungumza kwa niaba ya Mawaziri wengine baada ya kuwasili katika Mgodi wa Busolwa Mine Waziri wa Nchi na Maendeleo ya Madini wa Uganda Mheshimiwa Lokeris Peter amesema kuwa wamekuja Tanzania kujifunza mbinu za kuendeleza Sekta ya Madini hususan Uchimbaji Mdogo kwa kuwa Tanzania imekuwa ikifanya shughuli hii kwa muda mrefu na kupata mafanikio makubwa. Mheshimiwa Peter ameongeza kuwa wamekuja Geita kwa kuwa ni kuna migodi mingi mikubwa na midogo hivyo wamekuja kujifunza namna wanavyochimba, kuuza, kuunganisha wachimbaji katika vikundi na namna wanavyothibiti utoroshaji wa madini ili nao wakawaendeleze wachimbaji wa dogo nchini Uganda kwa nia ya kupata maendeleo kama Tanzania.
Awali akizungumza katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Stanslaus Nyongo Naibu Waziri wa Madini amesema kuwa Tanzania tumepata maendeleo makubwa ya kuweza kuendeleza wachimbaji wadogo, kati na wakubwa hivyo Mawaziri wanne na Wanasheria kutoka Uganda wamekuja nchini kuona ni jinsi gani Serikali ya Tanzania ilivyofanikiwa kuendeleza na kusaidia uchimbaji wa madini mdogo, kati na mkubwa. Amesema "wametembelea nchi nyingine za Afrika lakini bado wameona kuna umuhimu wa kufika Tanzania kwasababu kila nchi waliyofika waliona Tanzania ni mfano kwa Afrika hivyo wamekuja kujifunza na kuona namna nchi inavyoneemesha wananchi wake kupitia sekta ya madini baada ya mabadiliko ya sheria ya madini ya mwaka 2010 kwenda Sheria mpya ya mwaka 2017 na mabadiliko yake na sera za nchi kwa jumla ". Ameongeza kuwa wamekuja Geita kwasababu kuna madini na wachimbaji wadogo wengi zaidi ili waone jinsi wachimbaji wadogo wanavyowezeshwa kupata mitaji ya kufanya shughuli za uchimbaji.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ameipongeza Serikali ya Uganda kwa kuona umuhimu wa kuja kujifunza Geita na kutambua jinsi Sekta ya madini inavyoweza kuleta mageuzi ya uchumi wa nchi. Ametoa wito kwa wachimbaji wadogo mkoani hapa kujiunga katika vikundi ili kuunganisha nguvu, mitaji na uzoefu wao kwa pamoja na walete vifaa vya kisasa na kuwa na uchimbaji wa kisasa wenye tija ili mitaji yao ipanuke na kupata faida ili kuongeza ajira nyingi kwa watanzania.
Wakiwa Mkoani Geita Mwaziri hao pamoja na wataalamu wao wametembelea Wilaya ya Geita ambapo wamejionea shughuli za uchimbaji mdogo na kati katika migodi ya Busolwa mine uliopo kata ya Nyarugusu,Kadeo Mine na Kituo cha mfano cha Serikali kwa ajili ya kufundishia masuala ya uchimbaji wa madini kilichopo eneo la Lwamgasa Wilayani Geita.

Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita aliyevaa miwani na Koti la kijivu akimpokea Waziri wa Madini wa Uganda Mheshimiwa Lokeris Peter baada Mkoani Geita na ujembe wa Mawaziri wanne na wanasheria kwa ajili ya kujifunza namna Serikali ya Tanzania inavyowawezesha wachimbaji wadogo, Kati na Wakubwa katika Shughuli zao.

Mwaziri kutoka nchini Uganga pamoja na wataalamu wa madini wakifuatilia kwa karibu shughuli za uchimbaji mdogo zinavyofanyika katika Mgodi wa KADEO Limited uliopo kata ya Lwamgasa walipokwenda kujifunza uchimbaji Mdogo.



Mmiliki wa Mgodi wa KADEO Mine Limited ndugu Kadeo akitoa maelezo kwa Mawaziri na wataalmu wa madini walipotembelea Mgodi wa KADEO Mine kujifunza shughuli za uchimbaji mdogo wa Dhahabu Kata ya Lwamgasa Geita.


Naibu Waziri wa Madini Mheshimiwa Stanslaus Nyongo akizungumza na wadau wa madini na wanachama wa chama cha wachimbaji wadogo wa madini katika Mgodi wa Busolwa Mine wakati wa zaiara ya mwaziri waane kutoka Uganda ya kujifinza uchimbaji mdogo wa Madini.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAWAZIRI UGANDA WAVUTIWA NA UCHIMBAJI MDOGO WA DHAHABU MKOANI GEITA
MAWAZIRI UGANDA WAVUTIWA NA UCHIMBAJI MDOGO WA DHAHABU MKOANI GEITA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhPdyU0os65aYAAJRRP8x4eL5CKxiu3MEt96grkZ9I3bQ97zpoYr7FQw66tWzH5FKuaTSIhu55h__1A8x2dKZxBO7meHNCz9TgibOe7Pf624hp-uIzOfjBESGDlv77A9ftroBqXXXr0z1oT/s640/PIC+NA.3.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhPdyU0os65aYAAJRRP8x4eL5CKxiu3MEt96grkZ9I3bQ97zpoYr7FQw66tWzH5FKuaTSIhu55h__1A8x2dKZxBO7meHNCz9TgibOe7Pf624hp-uIzOfjBESGDlv77A9ftroBqXXXr0z1oT/s72-c/PIC+NA.3.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/12/mawaziri-uganda-wavutiwa-na-uchimbaji.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/mawaziri-uganda-wavutiwa-na-uchimbaji.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy