KITABU CHA KULETA MABADILIKO CHAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM
HomeJamii

KITABU CHA KULETA MABADILIKO CHAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii. Kampuni ya Viva Legency inayohusika na mafunzo na ushauri elekezi imekuja na kitabu kinachojulikana kama...

DKT. MWINUKA AWAPONGEZA WAHANDISI WANAWAKE TANESCO, KWA KUPEWA TUZO
BALOZI WA CHINA AFIKA OFISINI KWA SPIKA NDUGAI KUMUAGA
RAIS DKT. MAGUFULI AJICHANGANYA NA WANANCHI KUPANDA KIVUKO KWENDA KIGAMBONI NA KUFUNGUA KAMBI YA VIJANA WA CCM




Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.


Kampuni ya Viva Legency inayohusika na mafunzo na ushauri elekezi imekuja na kitabu kinachojulikana kama "SOTE TUNAWEZA" kikiwa na lengo la kusaidia harakati za mabadiliko pamoja na kukuza utamaduni wa mtanzania.


Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Viva Legency Fortunata Temu amesema kuwa kitabu cha "SOTE TUNAWEZA" kimeandikwa kwa lugha ya kiswahili na kinampa msomaji uwezo mkubwa wa kubadili fikra na kupiga hatua ya kimaendeleo.


"Kitabu cha sote tunaweza kimeandikwa kwa lugha ya kiswahili na kinampa uwezo msomaji kubadili kifikra na kupiga hatua kiamaendeleo" amesema Fortunata


Amesema kuwa katika uandishi wa kitabu hicho wametumia mifano ya watu mbalimbali kutoka Tanzania na sehemu nyingine za dunia waliofanikiwa na kusema kuwa wametumia mifano hiyo ili kumtia hamasa msomaji na kumfanya kufuata nyendo za hao watu waliofanikiwa.


Fortunata ameongeza kuwa mafanikio yanaweza kupatikana kwa kuangalia fursa zinazopatikana ndani ya jamii hivyo kuwataka watanzania kutumia lugha ya kiswahili kama fursa kwa kuhabarishana na kuelimishana .


Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , Dk.Ave Maria Semakafu ameipongeza kampuni ya Vivalegency na kusema kuwa kitabu cha "SOTE TUNAWEZA" kimekuja wakati mwafaka kwa sababu nchi yetu ipo kwenye harakati za mabadiliko kuelekea uchumi wa kati.


"Sote tunaweza kimekuja wakati mwafaka kwa sababu nchi yetu ipo kwenye harakati za mabadiliko kuelekea uchumi wa kati" amesema Dk.Semakafu.


Amesema Tanzania inachangamoto kubwa katika utamaduni wa uandishi na usomaji vitabu na kuwaomba watanzania watumie fursa ya kuandika vitabu vyenye dhima yenye kuleta maana na kuachana na utamaduni wa kuandika vitabu ambavyo havina dhima yoyote ya kubadili fikra na kuleta chachu ya maendeleo.

Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Viva Legacy (T) Bi. Fortunata Meela Temu akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa kitabu chaake cha "SOTE TUNAWEZA" leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt. Avemaria Semakafu na Mwajiri Msaidizi wa Viva Legacy (T) Ltd Bi. Neema Seleman.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Avemaria Semakafu (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa kitabu chaake cha "SOTE TUNAWEZA" leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus, na Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa VIVA lEGACY lTD (t) Bi. Fortunata Meela Temu.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Stadi Dkt. Avemaria Semakafu (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Viva Legacy Ltd (T) Bi. Fortunata Meela Temu wakiwaonyesha Waandishi wa Habari kitabu cha "SOTE TUNAWEZA" leo Jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho kimetungwa kwa lengo la kuimarisha mfumo wa utendaji na hasa kuboresha rasilimali watu.

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano baina yao na na Mkurugenzi wa Viva Legacy (T) Ltd alipokuwa akizungumzia kuhusu uzinduzi wa kitabu cha SOTE TUNAWEZA leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na: Frank Shija - MAELEZO)
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KITABU CHA KULETA MABADILIKO CHAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM
KITABU CHA KULETA MABADILIKO CHAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh9lMBa7uxJDr4LMMblCSfrMBdwpw4Q6w0T_L6vMz2FCSmnVWBe-lHnLzveDeJsihHn7RK0BloFzEvZBie-FEN8QfuH1SmSt5-h-vWQlNYCZTFynjUo4D9Ja0azVxFtL-r4n7zfvAN49Oo/s640/V1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh9lMBa7uxJDr4LMMblCSfrMBdwpw4Q6w0T_L6vMz2FCSmnVWBe-lHnLzveDeJsihHn7RK0BloFzEvZBie-FEN8QfuH1SmSt5-h-vWQlNYCZTFynjUo4D9Ja0azVxFtL-r4n7zfvAN49Oo/s72-c/V1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/12/kitabu-cha-kuleta-mabadiliko.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/kitabu-cha-kuleta-mabadiliko.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy