DKT. MAHIGA AHUTUBIA CHUO KIKUU CHA MAMBO YA NJE CHA CHINA
HomeJamii

DKT. MAHIGA AHUTUBIA CHUO KIKUU CHA MAMBO YA NJE CHA CHINA

Wziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Chuo cha Mambo ya...

MUHAS MLOGANZILA WAZINDUA HUDUMA ZA KUSAFISHA DAMU KWA WAGONJWA WA FIGO JIJINI DAR
SPIKA NDUGAI AKUTANA NA WANA KWAYA KUTOKA KONGWA
KAMATI YA KATIBA NA SHERIA YA BUNGE YAKUTANA NA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA NCHINI



Wziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Chuo cha Mambo ya Nje cha China kabla ya wawili hao hawajaelekea kwenye ukumbi kuhutubia wanafunzi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augastine Mahiga akihutubia wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China. Dkt. Mahiga alieleza ushirikiano wa Tanzania na China ulipoanza hadi leo na kuwasihi wanafunzi hao waangalie namna ya kuuimarisha kutokana na nafasi zao. 


Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China wakisikiliza Hotuba ya Dkt. Mahiga. Wanafunzi hao ambao walikuwa wadadisi sana walifurahi sana kutokana na elimu ya siku moja waliopata kutoka kwa Mbobezi wa masuala ya Diplomasia.

Dkt. Mahiga akiendelea na hotuba yake huku Mkuu wa Chuo akisikiliza kwa makini. Mkuu huyo alikiri kuwa kutokana na hotuba hiyo amejifunza vitu vingi sana.

Ujumbe uliomsindikiza Waziri Mahiga, kutoka kulia ni Bw. Benedict Msuya, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Gerald Mbwafu, Katibu wa Waziri na Kanali Remigius Ng'umbi, Mwambata Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China.

Mstari wa Mbele kutoka kushoto ni Kamishna msaidizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Malmeltha Mtagwaba, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Thomas Kashililah, Naibu Katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji kutoka Wizara ya Vwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha wa Zanzibar, Bw. Khams Omar na Balozi wa Tnzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki wakifuatilia hotuba hiyo.

Mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China akiuliza sawali kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

Picha ya Pamoja. Ziara katika kampuni ya magari ya Foton Motors Group
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa kampuni ya Foton Motors Group kabla ya kuanza kutembelea kampuni hiyo kujionea shughuli zake.

Baadhi ya aina ya magari yanayotengenezwa na kampuni ya Foton Motors Group.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa ndani ya moja ya magari yanayotengenezwa na kampuni ya Foton Motors Group.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa ndani ya karakana ya Foton Motors Group kuangalia shughuli za uzalishaji wa magari zinavyofanyika.

Baada ya kuona shughuli za kampuni hiyo, Waziri Mahiga alifanya mazungumzo rasmi na viongozi wa kampuni hiyo ambapo walimuomba awasaidie ili waweze kuwekeza nchini Tanzania. Kampuni hiyo inataka kufungua kiwanda cha kuunganisha magari yao kwa lengo la kuuza Tnzania na soko la Afrika. Walisema kampuni yao inatengeneza magari ya aina yote makubwa, madogo, mabasi na malori ndio inayoongoza kwa mauzo nchini China kwa kipindi cha miaka 13 sasa.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea zawadi ya mfano wa moja ya magari yanayotengenezwa na kampuni ya Foton Motors Group. Mazungumzo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya China Merchant

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya China Merchant inayowekeza kwenye mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Makamu wa Rais huyo pamoja na mambo mengine alielezea kufurahishwa kwake na uamuzi wa Serikali kuidhinisha rasmi utekelezaji wa mradi huo.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DKT. MAHIGA AHUTUBIA CHUO KIKUU CHA MAMBO YA NJE CHA CHINA
DKT. MAHIGA AHUTUBIA CHUO KIKUU CHA MAMBO YA NJE CHA CHINA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhfojPBoV2_xTnJnEGJY79aHlJ19QKmTlbvOoK5-BgoUqdyKYmI6zy60AT4UkVTFLt6WKggdko7FqOqKQ9SkUAQ4J1AAnEM_HiaN6ZkKxFHV69bBbdv-8u8SGPmCpP-vAEDNbs0P75EbxGC/s640/DSCN8309.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhfojPBoV2_xTnJnEGJY79aHlJ19QKmTlbvOoK5-BgoUqdyKYmI6zy60AT4UkVTFLt6WKggdko7FqOqKQ9SkUAQ4J1AAnEM_HiaN6ZkKxFHV69bBbdv-8u8SGPmCpP-vAEDNbs0P75EbxGC/s72-c/DSCN8309.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/12/dkt-mahiga-ahutubia-chuo-kikuu-cha.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/dkt-mahiga-ahutubia-chuo-kikuu-cha.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy