TUNATAKA MAAFISA HABARI NCHINI WAWE NA UELEWA WA MASUALA YA SIASA NA UCHUMI - DKT. HASSAN ABBAS
HomeJamii

TUNATAKA MAAFISA HABARI NCHINI WAWE NA UELEWA WA MASUALA YA SIASA NA UCHUMI - DKT. HASSAN ABBAS

Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma. Mkurugenzi wa Idara ya Habari ya MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas amesema ...

WAHITIMU IFM WAASWA KUJIEPUSHA NA RUSHWA NA UFISADI
SUZA AND ZUMC FORGE ACADEMIC PARTINERSHIP
WAZIRI MAVUNDE AGAWA MASHINE 31 KWA WANANCHI WA DODOMA MJINI

Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari ya MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas amesema Maafisa Habari na Mawasiliano hapa nchini wanatakiwa kuwa na uelewa wa masuala mbalimbali ikiwemo Uchumi, siasa na jamii katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.


Dkt. Abbas ameyasema hayo leo, Mjini Dodoma alipokuwa akifungua mafunzo ya Itifaki na Mawasiliano ya Kimkakati kwa Maafisa Habari na Mawasiliano kutoka Taasisi za Umma na Sekta Binafsi yaliyoandaliwa na Idara ya Habari MAELEZO kwa kushirikiana na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Washauri wa Kidiplomasia wa Kiuchumi (Economic Diplomacy Consultants).


"Itifaki ni moja ya eneo ambalo Afisa Habari yoyote anatakiwa kulijua kwa undani kutokana na jukumu alilonalo la kusimamia matukio mbalimbali yanayotokea katika Taasisi yake," alisema Dkt. Abbas.


Ameendelea kwa kusema, kuna kipindi Afisa Habari anapata wageni ambao ni wakuu wa nchi na kushindwa kujua namna ya viongozi hao wanavyotakiwa kukaa kutokana na vyeo vyao.Aidha, amesema kuwa mafunzo hayo ni muendelezo wa mafunzo mengine mengi ambayo Maafisa hao watakuwa wakiyapata kila wakati ili kuwapa uelewa katika maeneo mbalimbali ya masuala ya uchumi, siasa, jamii na katika sekta yenyewe ya mawasiliano. 


"Itafika kipindi tutajifunza hata vyeo vya jeshi namna vinavyokuwa pamoja na majina ya vyeo vyao ambapo itarahisisha katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Maafisa Habari," alisema Dkt. Abbas.
Mafunzo hayo ya Maafisa Habari na Mawasiliano ni ya siku mbili ambayo yameanza leo Novemba 23 na yanatarajia kumalizika kesho Novemba 24, 2017.
Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akifungua mafunzo kuhusu Mawasiliano ya Kimkakati na Itifaki kwa Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali na Sekta Binafsi (hawapo pichani) yanayofanyika kwa siku mbili mjini Dodoma.

Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akiongea na Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali na Sekta Binafsi wakati ufunguzi wa mafunzo yanayofanyika kwa siku mbili mjini Dodoma. (Picha zote na Frank Mvungi- Maelezo Dodoma)
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TUNATAKA MAAFISA HABARI NCHINI WAWE NA UELEWA WA MASUALA YA SIASA NA UCHUMI - DKT. HASSAN ABBAS
TUNATAKA MAAFISA HABARI NCHINI WAWE NA UELEWA WA MASUALA YA SIASA NA UCHUMI - DKT. HASSAN ABBAS
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhe78jPs7yQECFKgWfnMc8tJUvg6skysPneNjoD8pCW-7wawWlUbgfTThKLXp89HwI4FgTs_ewfkrZwPdrxa7O6JdMzlXfEwLebf1Dfhs43mSTPDtqnUu2_JcBBqqcEK4fBj5ezrN9nmXbL/s640/PICHA+1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhe78jPs7yQECFKgWfnMc8tJUvg6skysPneNjoD8pCW-7wawWlUbgfTThKLXp89HwI4FgTs_ewfkrZwPdrxa7O6JdMzlXfEwLebf1Dfhs43mSTPDtqnUu2_JcBBqqcEK4fBj5ezrN9nmXbL/s72-c/PICHA+1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/11/tunataka-maafisa-habari-nchini-wawe-na.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/11/tunataka-maafisa-habari-nchini-wawe-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy