BODI YA MAZIWA TANZANIA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KUONGEZA IDADI YA NG'OMBE WA MAZIWA KUFIKIA MILIONI 1.5

Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) (wa pili kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari katika moja ya mikutano yake na V...




Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) (wa pili kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari katika moja ya mikutano yake na Vyombo vya Habari.
Na Ismail Ngayonga MAELEZO


BODI ya Maziwa Tanzania (TDB) imeandaa Mpango Mkakati  wa ushirikiano na Sekta Binafsi ili kuongeza idadi ya ng’ombe wa maziwa kufikia Milioni 1.5 hatua inayolenga kuongeza wa soko la uzalishaji wa mazao ya maziwa katika nchi za Ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Nchini, Nelson Kilongozi wakati wa mahojiano katika kipindi maalum cha TUNATEKELEZA kinachorushwa hewani na Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) na kuratibiwa na Idara ya Habari (MAELEZO).
Kilongozi alisema taasisi hiyo imeandaa mkakati huo wa miaka 5 kuanzia mwaka 2018-23 ili kuhakikisha kuwa viwanda vya Tanzania vinakuwa na uwezo mkubwa wa kusindika maziwa na kushindana na nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya katika uuzaji na usambazaji wa mazao ya maziwa katika ukanda wa Jumuiya hiyo.
“Kwa sasa Tanzania ina jumla ya Ng’ombe wa maziwa 782,000 kati ya ng’ombe Milioni 28 waliopo, hivyo hawatoshelezi mahitaji yetu, lengo letu ni kushirikiana na sekta binafsi ili kuhakikisha kuwa tasnia ya maziwa inaleta tija inayokusudiwa” alisema Kilongozi.
Kwa mujibu wa Kilongozi alisema uzalishaji wa maziwa nchini kwa sasa ni lita Bilioni 2.1 kwa mwaka ambapo asilimia 70 yanatokana na ng’ombe wa asili, ambapo hata hivyo imekuwa ni vigumu kutoa elimu kwa wafugaji wake kutokana na changamoto ya kuhama mara kwa mara kwa ajili ya kutafuta malisho.
 Aliongeza kuwa kuwa mpaka sasa kuna jumla ya viwanda 82 vyenye uwezo wa kusindika lita laki 652,000, na hivyo Bodi hivyo imejipanga katika kuhakikisha kuwa inaongeza hamasa kwa wawekezaji kwa ajili ya kujenga viwanda vidogo na vya kati ili kulinda ubora wa maziwa ya Tanzania.
“Changamoto iliyopo sasa ni kukosekana kwa vituo vya ukusanyaji wa maziwa pindi yanapozalishwa kwa kuwa vituo hivyo havina vifaa vya kupoozea maziwa pindi yanazalishwa kabla ya kufikishwa kiwandani” alisema Kilongozi.
Alisema Bodi hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa wafugaji kuzingatia kanuni za ufugaji bora ikiwemo kuwa na mbegu bora zenye uwezo wa kuzalisha kiasi kikubwa cha cha maziwa ili waweze kujiongezea kipato sambamba na kuimarisha afya.
Akifafanua zaidi Kilongozi alisema Bodi hiyo pia imeendelea kuhamasisha wananchi kujenga tabia ya kunywa maziwa kwa, ambapo kwa mwaka huu wataanzisha Programu maalum ya uhamasishaji unywaji wa maziwa katika mikoa 6 nchini.
Aliitaja Mikoa hiyo kuwa ni Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Iringa, Njombe na Mbeya, ambapo pamoja na mambo mengine program hiyo imelenga pia kukabiliana na magonjwa ya udumavu yanayowakabili watoto wadogo katika mikoa mbalimbali nchini.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: BODI YA MAZIWA TANZANIA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KUONGEZA IDADI YA NG'OMBE WA MAZIWA KUFIKIA MILIONI 1.5
BODI YA MAZIWA TANZANIA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KUONGEZA IDADI YA NG'OMBE WA MAZIWA KUFIKIA MILIONI 1.5
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhlwc5e6BiWKnr3hc0qMBesvw8qPbQ9Bh4BWT_HBXiQlk3qi-W0S0kxjaam0wwQwIEPIY_w970WHR2HcCKTxDpCH3S-2hahgtNGRWHhWlEa4KH2FBv3yLP2ZgwyaYsBVWSC9NmIMIRKat0/s640/TDB.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhlwc5e6BiWKnr3hc0qMBesvw8qPbQ9Bh4BWT_HBXiQlk3qi-W0S0kxjaam0wwQwIEPIY_w970WHR2HcCKTxDpCH3S-2hahgtNGRWHhWlEa4KH2FBv3yLP2ZgwyaYsBVWSC9NmIMIRKat0/s72-c/TDB.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/04/bodi-ya-maziwa-tanzania-kushirikiana-na.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/bodi-ya-maziwa-tanzania-kushirikiana-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy