Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde amegawa mashine 31 za aina mbalimbal...
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde amegawa mashine 31 za aina mbalimbali kutoka kampuni ya HiTECH International kwa vikundi 31 katika jimbo lake la Dodoma Mjini.
Mashine alizozitoa Naibu Waziri ni pamoja na mashine za kutotolea vifaranga (incubators- mayai 1056 na mayai 528) mashine za matofali (umeme na manual), mashine za Popcorn zenye matairi, vyerehani, mashine za kutengeneza chaki (chaki 50,000-80,000 kwa siku), mashine za kunyonyolea kuku mpaka kuku 500 kwa siku.
Mavunde ametoa mashine hizo zenye thamani ya milioni 55.8 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake katika uvhaguzi wa mwaka 2015 kuwezesha wananchi ili wajikomboe kiuchumi lakini pia kuunga mkono mpango wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
COMMENTS