Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani ambaye amelazwa katika hospitali ya K...
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven
Ngonyani ambaye amelazwa katika hospitali ya Kairuki, Mikocheni jijini
Dar es salaam akitibiwa Januari 2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Mbunge wa Jimbo la
Korogwe Vijijini, Mhe. Steven Ngonyani (Profesa Majimarefu) aliyelazwa
katika Hospitali ya Kairuki akipatiwa matibabu.
Akiwa
hospitalini hapo leo (Jumatatu, Januari 2, 2017), Waziri Mkuu amesema
amefurahi baada ya kumkuta Mbunge huyo anaendelea vizuri na kwamba afya
yake inaridhisha.
Waziri
Mkuu ametumia fursa hiyo kumtakia afya njema Mhe. Ngonyani. Amesema
anaamini hivi karibuni atapona na kuruhusiwa kutoka hospitali.
Kwa upande wake Mbunge huyo ambaye amelazwa katika hospitali ya Kairuki iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam, amemshukuru Waziri Mkuu kwa kwenda kumjulia hali.
Pia amesema anaendelea vizuri na anatarajia kwenda nchini India kwa matibabu zaidi mara taratibu zitakapokamilika.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
JUMATATU, JANUARI 2, 2017.
COMMENTS