TANESCO YATOA MILIONI 10 KUSAIDIA MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO WALIOLAZWA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE, (JKCI)
HomeJamii

TANESCO YATOA MILIONI 10 KUSAIDIA MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO WALIOLAZWA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE, (JKCI)

 Meneja Mwandamizi  wa Shirika la umeme nchini, TANESCO, Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya, (wapili kushoto)...

DK. MENGI AKARIMU WAFARANSA SERENA HOTEL
TAARIFA KUHUSU JPC KATI YA TANZANIA NA UGANDA
UTAFITI WATOA ATHARI ZA UTEKELEZAJI WA SERA YA ELIMU BURE TANZANIA





 Meneja Mwandamizi  wa Shirika la umeme nchini, TANESCO, Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya, (wapili kushoto), na wafanyakazi wenzake, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, akikabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 10, kwa Mkurugenzi Myendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), Profesa Muhammed Janabi, (mwenye miwani), katika hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 14, 2017. Msaada huo w afedha utawezesha matibabu ya moyo kwa watoto watano waliolazwa kwenye taasisi hiyo.




NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA
la Umeme Tanzania, (TANESCO), limetoa msada wa Shilingi milioni 10 kusaidia
matibabu ya watoto wanaougua maradhi ya moyo kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI), jijini Dar es Salaam leo Novemba 14, 2017.
Akikabidhi
hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika hilo, Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam
na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya alisema, baada ya kusikia kupitia vyombo vya
habari kuwa Taasisi hiyo inahitaji msaada ili iweze kuwafanyia upasuaji watoto
ambao wazazi wao hawana uwezo wa kugharamia matibabu hayo, uongozi wa TANESCO
ulisikia maombi hayo.
Kwa
kawaida upasuaji kwa motto hugharimu kiasi cha Shilingi Milioni 2.
“Tumekuwa
na uhusiano mzuri na Taasisi yako, kwa hivyo japo hatuna uwezo mkubwa lakini Mkurugenzi
Mtendaji aliona ni vema tutoe msaada wa kuwezesha upasuaji wa watoto watano, na
leo tutakabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10.” Alisema Mhandisi
Mgaya katika hafla ya kukabidhi hundi hiuyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa JKCI, Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Aidha
Mhandisi Mgaya alisema mbali na msada huo wa fedha, TANESCO pia imeondoa tatizo
la upatikanaji wa umeme wa kutosha kwenye taasisi nhuyo kwa kuwawekea huduma
maalum ili kuhakikisha umeme unapatikana bila ya shida yoyote.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakayab Kikwete, Profesa
Mohammed Janabi, alisema ili kuenzi msada huo wa TANESCO, mmoja wa watoto
watakaofaidika na msada huo atapewa jina la TANESCO.
“Tutawaalika
katika hatua ya mwamzo kabla ya upasuaji ili muone hali halisi ya mgonjwa na
baada ya upasuaji na tutamuita TANESCO motto huyo.” Alisema Profesa Janabi
wakati akitoa shukrani zake.
Naye
Daktari bingwa wa moyo kwa watoto, Dkt. Naiz Majani alisema kwa mwaka Taasisi
hupokea wagojwa wanaohitaji upasuaji kiasi cha 200,000, kwa hivyo msada huo na
minbgine kutoka kwa wasamaria husaidia pakubwa katika kuokoa maisha ya watoto
wa Kitanzania.
“Tunawashukuru
sana kwa msada wenu na tunaomba muendelee kusaidia jamii katika kuhakikisha
watoto wa Kitanzania wanapatriwa matibabu ya moyo hata kama uwezo wao ni mdogo.”
Alisema Dkt. Majani.
Katika
hatua nyingine wafanyakazi wa TANESCO wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa
watoto waliolazwa kwenye taasisi hiyo wanaosubiri kufanyiowa upasuaji.


 Mhandisi Mgaya na Profesa Janabi, wakimsikilzia Mwenyekiti wa TUICO, Tanesco, Bw.Hassan J.M Athumani, wakati akitoa shukrani.
 Profesa Janabi (kulia), akimkabidhi jarida la taasisi hiyo, Mhandisi Mgaya
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, (kulia), akisalimiana na Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto, Dkt. Naiz Majani.
 Bi. Muhaji akikabidhi msada wa maji, na mahitaji mengine, kwa muuguzi wa zamu wa wodi ya watoto wanaougua maradhi ya moyo, Bi. Joyce Mtanga
 Mwenyekiti wa TUICO Tanesco, Bw. Hassan J.M Athjumani, (kulia), akikabidhi maji kwa mzazi wa mtoto aliyelazwa JKCI akisubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo.










Mtoto Mrisho Haidari(Miezi 7), ambaye anasumbuliwa na maradhi ya moyo akiwa wodini akisubiri kufanhyiwa upasuaji.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TANESCO YATOA MILIONI 10 KUSAIDIA MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO WALIOLAZWA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE, (JKCI)
TANESCO YATOA MILIONI 10 KUSAIDIA MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO WALIOLAZWA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE, (JKCI)
https://i.ytimg.com/vi/BoDoFfb6A34/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/BoDoFfb6A34/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/11/tanesco-yatoa-milioni-10-kusaidia.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/11/tanesco-yatoa-milioni-10-kusaidia.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy