JUMUIYA wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania (Tahliso) wameiangukia bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu (HESLB) kuha...

JUMUIYA wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania (Tahliso)
wameiangukia bodi ya mikopo ya
wanafunzi wa elimu ya Juu (HESLB) kuharakisha fedha za wanafunzi waliofeli baadhi ya masomo
kwa kupata alama D waliopo
vyuoni(supplementary).
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,Stanslaus
Kadugalize wakati akizungumza
na mtandao huu ambapo alisema idadi ya wanafunzi waliofeli baadhi ya masomo vyuoni ni kubwa
na mpaka sasa hawajapata fedha
za kujikimu .
Alisema fedha hizo ni kama kauli ya Naibu Waziri wa Elimu
alivyosema kuwa ifikapo ijumaa
wiki iliyopitia fedha ziwe zimefika vyuoni lakini mpaka sasa fedha hizo hazijafika jambo
ambalo linawapa wakati mgumu
wanafunzi hao.
Mwenyekiti huyo alivitaka vyuo visiweke sababu zisizo za msingi juu
ya kuwapa wanafunzi fedha zao
za kujikimu kwa wale ambao tayari fedha zimekwisha fikishwa vyuoni kwa kigezo cha
kujisajili.
“Tunatambua umuhimu wa kujisajili ila vyuo vitambue pia kwamba
wapo wanafunzi wengi
wanategemea fedha hizo hizo za bodi ya mikopo (HESLB) ili kulipia gharama za kujisajili kuweza
kukamilisha zoezi la
kujisajili hivyo vyuo viache kuweka sababu zinazopelekea usumbufu
kwa wanafunzi
“Alisema.
Kuhusu zoezi la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa
kwanza alisema sasa bodi ya
hiyo imekwisha kutoa kwa wanafunzi 29,000 kwa wale wote ambao wanasifa na hawajapata
katika upangaji wa awali
aliwashauri kutumia dirisha la rufani linalofunguliwa Novemba 13
mwaka huu ambapo rufaa hizo
itakuwa ni bure.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo hakisita kuzungumzia kuhusu zoezi
la udahili ambapo ambapo
aliitaka TCU kuingilia kati kwani bado kuna usumbufu mkubwa wa wanafunzi wanaoupata na
una hatarisha baadhi yao
kukosa nafasi ya kusoma.
Alisema vipo vyuo vimefahili wanafunzi zaidi ya idadi
wanayotakiwa mfano chuo cha
Mwenge na vyenginevyo jambo la ajabu wanapokwenda kuripoti vyuoni wanaambiwa wamekwisha
kamilisha idadi walizopangiwa.
“Sasa tunajiuliza kwanini walikubali idadi kubwa ya
wanafunzi
wathibitishe kwenye vyuo vyao? kwanini wasiweke ukomo wa
idadi kulingana na
wanayotakiwa lakini pia mpaka sasa wapo
wanasumbuliwa vyuoni
hawajapokelewa na wametoka makwao “Alisema.
“Mfano yupo mwanafunzi ametoka kwao Arusha amekwenda Mwanza
kuripoti chuo kalipa na ada
kabisa ya chuo sikitaji na alithibitisha kusoma hapo ajabu amekwenda kuripoti wana mwambia
wameshajaza idadi hivyo subiri
maamuzi ya TCU kama wataruhusu kuwapokea “Alisema.
Aliongeza kuwa vyuo visipelekee vurugu zisizo na maana yoyote
ile endapo wanafunzi hao
watakosa nafasi za masomo kwa mwaka huu kwa uzembe wa vyuo kudahili zaidi ya idadi yao
kwa hofu ya kukosa wanafunzi
.
“Lakini niwaambie sisi kama Tahliso hatutasita kuvichukulia hatua
vyuo hivyo kwa kuwalipa fidia
ya usumbufu wanafunzi ambao wamekumbana naowakati wa kufuatilia michakato hiyo
“Alisema.
(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
COMMENTS