MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHIMIZA ELIMU KWA WATOTO WA KIKE KASKAZINI UNGUJA
HomeJamii

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHIMIZA ELIMU KWA WATOTO WA KIKE KASKAZINI UNGUJA

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi katika ufunguzi wa Madrasa y...

WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA KULINDA AMANI ILIYOPO
SERIKALI YAONDOA TOZO ZISIZO ZA LAZIMA KATIKA ZAO LA KOROSHO
UJUMBE WA KAMPUNI YA “ENGINEERING CUNSULTANTS GROUPS”-ECG







 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi katika ufunguzi wa Madrasa ya Al-Madrasatul Munawwaratul
Islamiyyah ya KilimaninTazari Zanzibar ikiwa sehemu ya ziara yake ya mkoa wa Kaskazini Unguja.






 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa Sheihiya ya Kilimani waliojitokeza kwa wingi kwenye ufunguzi wa Madrasa ya Al-Madrasatul Munawwaratul Islamiyyah ya KilimaninTazari Zanzibar ikiwa sehemu ya ziara yake ya mkoa wa Kaskazini Unguja.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki dua maalum mara baada ya zoezi la  ufunguzi wa Madrasa ya Al-Madrasatul
Munawwaratul Islamiyyah ya KilimaninTazari Zanzibar kukamilika ikiwa sehemu ya ziara yake ya mkoa wa Kaskazini Unguja.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ramani ya msikiti mkubwa unaojengwa kwa nguvu za wananchi alipotembelea Uwanja wa Jitimai uliopo Kidoti mkoa wa Kaskazini Unguja.                                         ............................................................................... 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi na walezi wa Tanzania Zanzibar waache tabia ya kuwaoza wasichana wa kike wakiwa na umri mdogo bali wawasomeshe kwa ajili ya manufaa yao ya jamii kwa ujumla.



Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati akizindua madrasa ya kisasa iliyojengwa kwenye eneo la Kilimani na kukagua ujenzi wa
vyumba vya madarasa na ujenzi wa msikiti mkubwa kuliko yote nchini Tanzania unaojengwa katika eneo la Jitimai kidoti katika Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa michango ya wananchi katika siku yake ya kwanza ya ziara ya Kikazi Kisiwani Unguja.



Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kama wazazi na walezi watasomesha watoto wa
kike elimu watakayopata itasaidia kwa kiasi kikubwa wasichana hao kufanya maamuzi sahihi na yenye tija katika jamii.


Amesisitiza kuwa pamoja na elimu kuwa ni haki ya msingi kwa mtoto wa kike hivyo ni muhimu kwa jamii nzima ya Zanzibar ihakikishe watoto wa kike wote wanapata elimu kwani watakuwa na uwezo wa kuchagua na kuandaa mustakbali wa maisha yao ya baadaye ikilinganishwa na hali ilivyo sasa kwenye baadhi ya maeneo.

Kuhusu elimu ya dini, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahimiza wazazi na walezi kuwalea watoto katika maadili mema kwa kuzingatia maandiko matakatifu ya Mtume Mohammad (S.A.W).

Amesema vijana wengi wanaolelewa kwa kufuata misingi ya bora ya dini ni vigumu kurubuniwa na kujiingiza katika matendo yasiyofaa katika jamii.



BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHIMIZA ELIMU KWA WATOTO WA KIKE KASKAZINI UNGUJA
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHIMIZA ELIMU KWA WATOTO WA KIKE KASKAZINI UNGUJA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEizOZsdyqHBxge6g0SwbTEgxjTPh72nkmZBlOGJx1qQkg8_-jhtMKvBERmHyDL4_rA0ECr_pLHpt7nK4DUuMtGxXZxOgeaWXuWgIp9fB8rQLNpGB82lqoZE5pJeGBoRMRc4pi5REsmDuwY/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEizOZsdyqHBxge6g0SwbTEgxjTPh72nkmZBlOGJx1qQkg8_-jhtMKvBERmHyDL4_rA0ECr_pLHpt7nK4DUuMtGxXZxOgeaWXuWgIp9fB8rQLNpGB82lqoZE5pJeGBoRMRc4pi5REsmDuwY/s72-c/1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/12/makamu-wa-rais-mhe-samia-suluhu-hassan.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/makamu-wa-rais-mhe-samia-suluhu-hassan.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy