KIONGOZI wa chama cha ACT-Wazalendo, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe, ameachiliwa kwa dhamana baa...
KIONGOZI wa chama cha ACT-Wazalendo, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe, ameachiliwa kwa dhamana baada ya kukamatwa na polisi mapema asubuhi Oktoba 31, 2017 akiwa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupewa dhamana ya polisi, Mhe. Zitto aliwaambia waandishi wa habari kuwa kukamatwa kwake kumehusishwa na matamshi yake ya hivi karibuni kuhusu takwimu za uchumi wa nchi, wakati akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani kata ya Kijichi jijini Dar es Salaam.
"Lakini pia nimehojiwa kuhusiana na makosa ya kimtandao (Cyber crime) kwa hivyo tunasubiri kama watapeleka kesi mahakamani tukayazungumze huko, lakini tulitarajia kukamatwa kwangu maana Rais alisema nikamatwe na ingekuwa ajabu kama nisingekamatwa." Alisema Zitto.
Moi jana tu Oktoba 30, 2017, Serikali kupitia maafusa wa Benki Kuu ya Tanzania, na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, walikosoa vikali takwimu za Mhe. Zitto ambazo kiujumla zinaeleza kuporomoka kwa uchumi ambapoaliuita uchumi wa nchi umesinyaa.
Hata hivyo maafisa hao wa serikali waliwaambia waandishi wa habari kuwa takwimu hizo ni potofu na kwamba uchumi wa nchi unafanya vizuri.
COMMENTS