WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA WABUNGE KUAGA MWILI WA MBUNGE WA DIMANI- HAFID HALLY TAHIR
HomeSiasa

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA WABUNGE KUAGA MWILI WA MBUNGE WA DIMANI- HAFID HALLY TAHIR

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na wabunge wakiwa wamesimama kimya kwa dakikika moja kwa heshima ya mbunge wa Dimani, Hafi...

KITI CHA UMEYA CHAIVURUGA CHADEMA MBEYA MJINI
RAIS MAGUFULI AONGOZA KUMUAGA SAMUEL SITTA NA ATUMA RAMBIRAMBI KIFO CHA MBUNGE HAFIDH ALI TAHIR
MATUKIO BUNGENI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO






WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA WABUNGE KUAGA MWILI WA MBUNGE WA DIMANI- HAFID HALLY TAHIR

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na wabunge wakiwa wamesimama kimya kwa dakikika moja kwa heshima ya mbunge wa Dimani, Hafidh Ally Tahir, bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. Hafidh alifariki dunia usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
 
 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mbunge wa Dimai Hafidh Ally Tahir, bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. 
 
 
 



Spika wa Bunge, Job Ndugai akitoa heshima za mwisho kwa mbunge wa Dimani, marehemu Hafidh Ally Tahir kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Novemba 11, 2016. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa mbunge wa Dimani, Hafidh Ally Tahir kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Novemba 11, 2016. Mbunge huyo alifariki dunia mjijini Dodoma usiku wa kuamkia leo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (wapili kulia) na Katibu wa Bunge, Dkt.Thomas Kashililah wakisubiri kupokea mwili wa Mbunge wa Dimani, marehemu Hafidh Ally Tahir kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma ambako ulisafirishwa kwenda Zanzibar kwa Mazishi Novemba 11, 2016. 
 
 
 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai na Kiongozi wa  Upinzania bungeni, Freeman Mbowe (kulia) wakishuhudia wakati mwili wa mbunge wa Dimani, Hafidh Ally Tahir ukipandishwa kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa Dodoma ili kusafirishwe kwenda Zanzibar kwa mazishi Novemba 11, 2016.


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza wabunge kuuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Dimani, Zanzibar Mheshimiwa Hafidh Ally Tahir.

Bw. Tahir amefariki saa 9 alfajiri ya kuamkia leo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na mwili wake kuagwa katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar kwa mazishi.

Akizungumza katika tukio hilo, Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, familia ya marehemu na wabunge wote.“Tumepokea taarifa za msiba huu kwa mshtuko mkubwa. Leo tupo katika wakati mgumu sana. Tumeondokewa na viongozi wengi,” amesema.

Amesema wafiwa wanatakiwa kuishi kwa upendo. “Tumuombee marehemu, tuiombee familia iwe na moyo wa utulivu katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.”

Bw. Hafidh alizaliwa Oktoba 30, 1953 na aliwahi kuwa Mkuu wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (1970-1978) na amekuwa mbunge tangu 2005 hadi mauti yanamkuta.Enzi ya uhai wake, alishiriki kikamilifu katika masuala ya michezo; alikuwa mwamuzi wa soka mwenye beji ya FIFA na kocha msaidiizi wa timu ya soka ya Bunge.

Hadi jana, Bw. Hafidh alishiriki katika shughuli mbalimbali ikiwemo uchaguzi wa kupata viongozi wa Tawi la Umoja wa Wabunge WanaYanga mjini Dodoma ambapo yeye alichaguliwa kuwa Katibu.




IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, NOVEMBA 11, 2016.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA WABUNGE KUAGA MWILI WA MBUNGE WA DIMANI- HAFID HALLY TAHIR
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA WABUNGE KUAGA MWILI WA MBUNGE WA DIMANI- HAFID HALLY TAHIR
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhgosKOuoZ69JRSUHjzTMh9sDFg4Ko01jOMScNvKtPhyCLJUpXuTZo4sUAp8XdAeBtg7E2dPW_NrSJEqzQ4LZTV3WGtDpel4XFQ0bzYJY9KZU4nzSDX61FyQbkwFrblJUVMJCgvz-x5vPIy/s640/RG1A2081.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhgosKOuoZ69JRSUHjzTMh9sDFg4Ko01jOMScNvKtPhyCLJUpXuTZo4sUAp8XdAeBtg7E2dPW_NrSJEqzQ4LZTV3WGtDpel4XFQ0bzYJY9KZU4nzSDX61FyQbkwFrblJUVMJCgvz-x5vPIy/s72-c/RG1A2081.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/11/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-aongoza.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/11/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-aongoza.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy