RAIS MAGUFULI AONGOZA KUMUAGA SAMUEL SITTA NA ATUMA RAMBIRAMBI KIFO CHA MBUNGE HAFIDH ALI TAHIR
HomeSiasa

RAIS MAGUFULI AONGOZA KUMUAGA SAMUEL SITTA NA ATUMA RAMBIRAMBI KIFO CHA MBUNGE HAFIDH ALI TAHIR

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa aliyekuwa Spika...

WANACHAMA 681 KUTOKA UMOJA WA VIJANA WA CCM VYUO NA VYUO VIKUU MKOA WA DAR ES SALAAM WATUNUKIWA VYETI VYA KUHITIMU MASOMO YAO
BULEMBO ATINGA IGUNGA NA NZEGA MKOANI TABORA LEO, ATAKA MADIANI KUFANYAKAZI KWA KARIBU NA MABALOZI
WARIDE: ASISITIZA UBUNIFU KWA WATENDAJI WA CCM NA SERIKALI.





RAIS MAGUFULI AONGOZA KUMUAGA SAMUEL SITTA NA ATUMA RAMBIRAMBI KIFO CHA MBUNGE HAFIDH ALI TAHIR
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016
 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 11 Novemba, 2016 amewaongoza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samuel John Sitta aliyefariki dunia tarehe 07 Novemba, 2016 katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani.
Mwili wa Marehemu Samuel John Sitta umeagwa katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam ambapo Viongozi wengine waliojumuika kuuaga mwili huo ni pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Mawaziri wakuu wastaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Frederick Tluway Sumaye, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Katipwa Wambali na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Baada ya kuagwa katika viwanja vya Karimjee, mwili wa Marehemu Samuel John Sitta umesafirishwa kwenda Dodoma ambako Wabunge, Viongozi wa Mkoa na wananchi watapata fursa ya kuuaga katika Viwanja vya Bunge na baadaye jioni utasafirishwa kwenda Tabora ambako maziko yatafanyika kesho Jumamosi huko Urambo.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Dimani Zanzibar Mhe. Hafidh Ali Tahir kilichotokea majira ya saa 9 usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.Mhe. Hafidh Ali Tahir amefariki dunia muda mfupi alipofikishwa hospitali baada ya kuugua ghafla.
"Nimeshtushwa sana na kifo cha Mhe. Hafidh Ali Tahir na ninakuomba Mhe. Spika Job Ndugai unifikishie salamu za pole kwa Familia ya Marehemu, Wabunge, Wananchi wa Jimbo la Dimani, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote walioguswa na msiba huu.
"Tutamkumbuka Mhe. Hafidh Ali Tahir kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika utumishi wa umma, katika michezo na akiwa mwakilishi wa wananchi, kwa hakika tumepoteza mtu muhimu sana" amesema Rais Magufuli na kumuombea Marehemu apumzishwe mahali pema peponi. Amina.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
11 Novemba, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akimfariji Mama Margareth Sitta, Mjane wa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016.

 Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakitoa heshima  za mwisho kwa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016
  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akimpa pole binti wa  aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akimpa pole Mhe. John Sitta, mtoto wa  aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016

 ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akiwapa pole wanafamilia  wa  aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016.
 ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akiwapa pole wanafamilia  wa  aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016
 ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akiwapa pole wanafamilia  wa  aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Nobemba 11, 2016
 ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akiwapa pole wanafamilia  wa  aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016
 ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akiwapa pole wanafamilia  wa  aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016
 ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akiwapa pole wanafamilia  wa  aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS MAGUFULI AONGOZA KUMUAGA SAMUEL SITTA NA ATUMA RAMBIRAMBI KIFO CHA MBUNGE HAFIDH ALI TAHIR
RAIS MAGUFULI AONGOZA KUMUAGA SAMUEL SITTA NA ATUMA RAMBIRAMBI KIFO CHA MBUNGE HAFIDH ALI TAHIR
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjblt_DMD7F_aj-_-EzVyqoZMUPvldhkhljpRjnWFOLyx6ofXykQpxn4UFXtpP8tuTG5oDxfYIV2FoDqjeBSFeq8jjcNpBaPNRf4W_3SR8V_JE39SltexWh4JAFSHKjbPsXiWpR7wdYzHA/s640/a10.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjblt_DMD7F_aj-_-EzVyqoZMUPvldhkhljpRjnWFOLyx6ofXykQpxn4UFXtpP8tuTG5oDxfYIV2FoDqjeBSFeq8jjcNpBaPNRf4W_3SR8V_JE39SltexWh4JAFSHKjbPsXiWpR7wdYzHA/s72-c/a10.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/11/rais-magufuli-aongoza-kumuaga-samuel.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/11/rais-magufuli-aongoza-kumuaga-samuel.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy