NAIBU WAZIRI DKT. MARY MWANJELWA AWATAKA TFRA KUONGEZA UFANISI KATIKA UTENDAJI WA KAZI ZAO
HomeJamii

NAIBU WAZIRI DKT. MARY MWANJELWA AWATAKA TFRA KUONGEZA UFANISI KATIKA UTENDAJI WA KAZI ZAO

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa ameiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) kuongeza ufanisi katika ute...

WAZIRI MKUU MHE. MAJALIWA AWASILI TORONTO CANADA
KESI YA MAUAJI YA KANUMBA INAYOMKABILI LULU YAANZA KUUNGURUMA LEO.
TIB CORPORATE BENKI YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA DAR ES SALAAM


Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa ameiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi zao ili kuleta mabadiliko makubwa kwa wakulima.

Akiongea katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Uthibiti wa Mbolea (TFRA) jana na kuwahusisha Watumishi wote wa Taasisi hiyo, Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi hao kuwa na malengo na mpango kazi ambao kila mtu atautekeleza  na atapimwa kutokana na mpango kazi huo.

 Hata hivyo Dkt. Mwanjelwa amewapongeza  kwa namna wanavyotekeleza majukumu yao kwa sasa, hususan katika zoezi la uagizaji wa mbolea kwa mfumo wa pamoja (Bulk Procurement System) ambao umechangia kwa kiasi kikubwa mbolea hiyo kumfikia mkulima kwa bei nafuu.Pamoja na pongezi hizo Naibu Waziri, Dkt. Mwanjelwa ameitaka  TFRA  kuongeza bidii katika utendaji wao wa kazi na kuhakikisha kuwa wanaondoa kero zinazowakabili Wakulima.

Aidha ameitaka Mamlaka ya Uthibiti wa Mbolea kuhakikisha kuwa mambo matatu muhimu yanazingatiwa ambayo ni upatikanaji wa mbolea (Availability) ufikishaji wa mbolea karibu zaidi kwa Wakulima (Accessibility) na kwa bei ambayo wakulima wanaweza kumudu kuinunua (Affordability) .“Mhakikishe mbolea inakuwepo nchini kote na wakulima wanapohitaji inapatikana na iwe kwa gharama ambayo Mkulima anaweza akanunua. “Amekaririwa, Naibu Waziri.

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa mamlaka hiyo bwana Lazaro Kitandu amemshukuru Naibu waziri kwa kuwatembelea na kuwatia moyo katika utendaji kazi wao na kumhakikishia kwamba TFRA imejipanga vizuri kupambana na changamoto za baadhi ya wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu hasa katika kuzingatia bei elekezi ya mbolea.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akizungumza viongozi pamoja na wafanyakazi katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Uthibiti wa Mbolea (TFRA)
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akipata maelezo kuhusu sampuli ya mbolea aina ya DAP kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mbolea (TFRA) Bwana Lazaro Kitandu  alipotembelea ofisi hiyo.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: NAIBU WAZIRI DKT. MARY MWANJELWA AWATAKA TFRA KUONGEZA UFANISI KATIKA UTENDAJI WA KAZI ZAO
NAIBU WAZIRI DKT. MARY MWANJELWA AWATAKA TFRA KUONGEZA UFANISI KATIKA UTENDAJI WA KAZI ZAO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjd5OxADglDoGRAWYNNKrSWMvQyA3wtleLHk6kv6vAf_TH2FEv59DB0JcNrQuLUBL7AW7POeWN5Xv45zyNEWxsD6MRdUax58GTVy6Q2V5_7AHtcq-v_f_kwxg1tQF2XEYwMsCfivSJzOf2E/s640/01.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjd5OxADglDoGRAWYNNKrSWMvQyA3wtleLHk6kv6vAf_TH2FEv59DB0JcNrQuLUBL7AW7POeWN5Xv45zyNEWxsD6MRdUax58GTVy6Q2V5_7AHtcq-v_f_kwxg1tQF2XEYwMsCfivSJzOf2E/s72-c/01.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/10/naibu-waziri-dkt-mary-mwanjelwa-awataka.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/naibu-waziri-dkt-mary-mwanjelwa-awataka.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy