SERIKALI: MATUMIZI YA DOLA NCHINI HAYAATHIRI KUSHUKA KWA THAMANI YA SHILINGI
HomeJamii

SERIKALI: MATUMIZI YA DOLA NCHINI HAYAATHIRI KUSHUKA KWA THAMANI YA SHILINGI

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Vwawa Mhe. Japhet Hasunga (C...

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA PASAKA KANISA LA MTAKATIFU YOSEPH
WAZIRI MKUU AWAOMBA VIONGOZI WA DINI WAPIGANIE NA KUILINDA AMANI
KAMISHNA WA OPERESHENI WA ZIMAMOTO AZINDUA MAFUNZO YA UZAMIAJI MAJINI KINA KIREFU



Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Vwawa Mhe. Japhet Hasunga (CCM)


Serikali imesema kuwa kushuka au kupanda kwa thamani ya shilingi nchini hakusababishwi na bidhaa na huduma mbalimbali kutozwa kwa dola bali kunatokana na misingi ya shughuli mbalimbali za kiuchumi (Macroeconomic fundamentals) pamoja na hali halisi ya uchumi wa nchi zinazofanya biashara na Tanzania.


Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Vwawa Mhe. Japhet Hasunga (CCM), aliyetaka kujua mikakati ya Serikali katika kuimarisha thamani ya shilingi ya Tanzania na kupiga marufuku matumizi ya fedha za kigeni nchini.


Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji aliainisha kuwa nakisi ya urari wa biashara, mfumuko wa bei na tofauti ya misimu (seasonal factors) ni sababu kuu zinazosababisha kushuka na kupanda kwa thamani ya shilingi nchini.
Dkt. Kijaji aliliambia Bunge kuwa ili kuimarisha thamani ya shilingi Benki Kuu inaendelea kuthibiti mfumuko wa bei ili usitofautiane sana na wabia wa biashara nchini.


“Benki Kuu imethibiti biashara ya maoteo (speculation) katika soko la fedha za kigeni ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa miamala ya fedha za kigeni inafanywa na benki kwa ajili ya shughuli za kiuchumi tu na sio biashara ya maoteo, hali hii itasaidia upatikanaji wa fedha za kigeni katika soko la rejareja ili kupunguza shinikizo la kuporomoka kwa thamani ya shilingi.”Alisema Dkt Kijaji.


Dkt. Kijaji alifafanua kuwa pamoja na hatua zinazochukuliwa na Benki Kuu ufumbuzi wa kudumu wa kutengamaa kwa thamani ya shilingi nchini hutegemea zaidi kupungua kwa nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa, huduma na uhamisho wa mali nchi za nje.
Imetolewa na:


Benny Mwaipaja
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
11/9/2017
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SERIKALI: MATUMIZI YA DOLA NCHINI HAYAATHIRI KUSHUKA KWA THAMANI YA SHILINGI
SERIKALI: MATUMIZI YA DOLA NCHINI HAYAATHIRI KUSHUKA KWA THAMANI YA SHILINGI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhMUwTsbBBNGxUrT5fcUIgEzHq1yxvb4IDBBakTKIkCrYeYq_YGKHnZUQvISDspWkQR69QT8u8VZ5vLKBWxJ1TdpnyWt14QoJ3jJxQGsaNmxv2XhclE0Qnwbb7z6ZKfqNzIRQxthr-9EleU/s640/IMG_03750.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhMUwTsbBBNGxUrT5fcUIgEzHq1yxvb4IDBBakTKIkCrYeYq_YGKHnZUQvISDspWkQR69QT8u8VZ5vLKBWxJ1TdpnyWt14QoJ3jJxQGsaNmxv2XhclE0Qnwbb7z6ZKfqNzIRQxthr-9EleU/s72-c/IMG_03750.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/serikali-matumizi-ya-dola-nchini.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/serikali-matumizi-ya-dola-nchini.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy