MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MAKAO MAKUU YA KAMISHENI YA KISWAHILI YA AFRIKA MASHARIKI
HomeJamii

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MAKAO MAKUU YA KAMISHENI YA KISWAHILI YA AFRIKA MASHARIKI

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwaonyesha wajumbe walioshiriki Kongamano la kwanza la Kimataifa la Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika M...

DALILI KWAMBA BADO UNA UCHOVU WA LIKIZO NA NAMNA YA KUKABILIANA NAZO
RAIS DKT. MAGUFULI AMUPISHA NAIBU WAZIRI WA MADINI MHE. DOTTO MASHAKA BITEKO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
IGP SIRRO AONGOZA MAOFISA NA ASKARI POLISI SHEREHE YA KUUKARIBISHA MWAKA 2018



Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwaonyesha wajumbe walioshiriki Kongamano la kwanza la Kimataifa la Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki mpango mkakati wa miaka mitano wa Kamisheni hiyo (kulia) Mtendaji Mkuu wa Kamisheni Prof. Kenneth Simala na (kushoto) Rais Mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida wakikata utepe kama ishara ya kufungua Ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa ofisi ya Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki mjini Zanzibar.  Kushoto (kwake) ni Waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Afrika mashariki, Balozi Dkt. Augustine mahiga, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe (kulia0 kwake) na viongozi wengine.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa ofisi ya Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki mjini Zanzibar.  Kushoto (kwake) ni Waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Afrika mashariki, Balozi Dkt. Augustine mahiga, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe (kulia kwake) na viongozi wengine. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa Kongamano la kwanza la Kimataifa la Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki lililobeba mada isemayo Kuleta Mabadiliko katika jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kutumia Kiswahili lilianza leo mjini Unguja, Zanzibar. 



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida wakipeana ishara ya kushukuru mara baada ya Balozi wa Japan kukabidhi miradi miwili mikubwa,mmoja ukiwa ni ujenzi wa uzio wa shule ya Msingi ya Muyuni na wa pili ni mradi wa uboreshaji  wa mazingira ya elimu katika wilaya ya ya kusini uliojumuisha ujenzi wa shule ya awali katika kijiji cha Kajengwa na Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Kizimkazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuelezea  Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida namna Pomboo wanavyovutia utalii katika mkoa wa kusini wakati akimkabidhi zawadi ya sanamu ya Pomboo mara baada ya ufunguzi wa Ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )



Maryam Kidiko na Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar.

KUANDALIWA kwa kongamano la kwanza la Kimataifa la Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki ni miongoni mwa juhudi za kuendeleza lugha ya Kiswahili katika ukanda huo na Duniani kwa jumla.
Hayo ameyasema Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki huko katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip iliopo Malindi Mjini Zanzibar.
Alisema kongamano hilo lililowashirikisha wataalamu wa lugha ya Kiswahili wa nchi wananchama wa Afrika Mashariki lina umuhimu mkubwa katika historia ya maendeleo ya Kiswahili duniani pamoja na kupanga mikutano na kubadilishana utalaamu .
Hivyo Alieleza kuwa ni muhimu kwa kamisheni kusimamia kwa makini hadhi ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano ikitambuwa kwamba ukanda wa Afrika Mashariki ni sehemu ya Dunia yenye lugha tofauti.
Samia alisema uratibu na uendelezaji wa Maendeleo na matumizi ya Kiswahili utaimarisha mchakato na utengamano wa Jumuiya kwa maendeleo endelevu. “Utengamano wa Jumuiya sio tukio bali ni mchakato ambao unapaswa kuendeshwa na watu wenye kuelewa vizuri matumizi endelevu ya Kiswahili “Alisema Makamo wa Rais.
Hata hivyo alielezea kuwa mafanikio kamili yanategemea mkabala wa mawasiliano na ushiriki wa raia wote katika maendeleo endelevu ya Jumuiya . Alisema Kiswahili ni kiungo muhimu kati ya wana Afrika Mashariki katika kujenga utambuzi na kubaini changamoto pamoja na fursa zinazofungamana na maendeleo.
Alitaka kongamano hilo kuonyesha namna ambavyo Kiswahili kinaweza kufanikisha utangamano na malengo ya kuimarisha maendeleo ya nchi wanachama Afrika Mashariki. Waziri Samia alionyesha kkufurahishwa kwake na nchi wanachama kutenga bajeti kila mwaka kwa lengo la kuimarisha na kuendeleza shughuli za Kamisheni hiyo.
Nae Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe alisema baadhi ya Nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ambazo zilikuwa nyuma katika kutumia lugha ya Kiswahili wamepiga hatua na kimeweza kusaidia katika kuharakisha maendeleo yao.
Aliitaka Kamisheni hiyo kushirikiana na Wadau mbali mbali ili iweze kuleta maendeleo kupitia lugha ya Kiswahili.
Kwa upande wa Waziri wa Habari Utalii , Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma alisema Serilkali ya Zanzibar inathamini kuwepo Makao Makuu ya Kamisheni Zanzibar na ameahidi itaendelea kuunga mkono kutokana na umuhimu wa lugha hiyo.
Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Profesa Kenneth Simala alisema Kamisheni itafanya juhudi ya kuziunganisha nchi wanachama na asasi za kiraia kukikuza Kiswahili.
Sambamba na hayo alisema Zanzibar imeweza kutowa mchango mkubwa katika Nchi za Afrika Mashariki kupitia lugha ya Kiswahili katika kukuza lugha hiyo.
Kauli mbiu ya Kongamano hilo la siku mbili ni ‘KULETA MABADILIKO KATIKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUPITIA KISWAHILI.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MAKAO MAKUU YA KAMISHENI YA KISWAHILI YA AFRIKA MASHARIKI
MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MAKAO MAKUU YA KAMISHENI YA KISWAHILI YA AFRIKA MASHARIKI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEirMZtmakC5t6_u6en9KHUCQcE_jd36LIt_lG9QOZdq5P9cjMVyidvhe0IiZNSpRRDO4w3jSRivXZEmdZ2sdCT5VQWwEO9oZVsYjNXUAwpnyVojzPpn7QNjpAIae5RLwLCHXk4AmhSc1fI/s640/04-1-1024x686.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEirMZtmakC5t6_u6en9KHUCQcE_jd36LIt_lG9QOZdq5P9cjMVyidvhe0IiZNSpRRDO4w3jSRivXZEmdZ2sdCT5VQWwEO9oZVsYjNXUAwpnyVojzPpn7QNjpAIae5RLwLCHXk4AmhSc1fI/s72-c/04-1-1024x686.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/makamu-wa-rais-samia-suluhu-hassan.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/makamu-wa-rais-samia-suluhu-hassan.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy