JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO Simu ya Upepo : “ N G O M E ” Makao Makuu ya Jeshi,...
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo : “N G O M E” Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex : 41051 DAR ES SALAAM,19 Septemba 2017
Tele Fax : 2153426
Barua pepe: ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Tovuti : www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha Askari wake aitwaye Praiveti Mussa Jumanne Muryery ambaye alikuwa katika Ulinzi wa Amani nchini DRC.
Askari huyo amefariki baada ya kushambuliwa kwa kupigwa risasi na kundi la waasi tukio ambalo limetokea tarehe 17 Septemba 2017.
Kufuatia shambulizi hilo Umoja wa Mataifa umeunda Bodi ya Uchunguzi kuchunguza tukio hilo. Aidha, Maafisa na Askari wa JWTZ wanaendelea na majukumu yao katika Operesheni hiyo.
Umoja wa Mataifa unaandaa utaratibu wa kuuleta mwili wa marehemu nchini. Mtajulishwa taratibu za mapokezi, kuaga mwili wa marehemu na mazishi.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amina.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, DAR ES SALAAM, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi : 0756 716085
COMMENTS