Mbunge wa jimbo la Mtama,Mhe Nape Nnauye akiwasili katika kikao kati yake na wazee Maarufu wa Kata ya Mtama na Majengo A, kilichofanyika...
Mbunge wa jimbo la Mtama,Mhe Nape Nnauye akiwasili katika kikao kati yake na wazee Maarufu wa Kata ya Mtama na Majengo A, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki kijiji cha Majengo A huku akiwa ameongozana na Katibu Msaidizi wa Wilaya ya Lindi Vijijini, Shaibu Bakari Ngatiche.

Mbunge wa jimbo la Mtama,Mhe Nape Nnauye akizungumza na Wazee maarufu wa Kata ya Mtama na Majengo A, katika kikao chao kilichofanyika katika ukumbi wa Kanisa la Katoliki, Mtama Lindi Vijijini. Mhe. Nape alizungumza mambo mengi pamoja na kuwaomba Wana Mtama kusameheana kwa mambo yote mabaya yaliyokuwa yametokea na kuanza ukurasa mpya wa kujenga undugu wa kupendana na kushirikiana katika mampo mbalimbali. Amewaomba kuziweka kando itikadi zao za kisiasa na badala yake wakae kwa umoja wao wafikirie namna ya kuliletea maendeleo jimbo la Mtama.
"Ndugu zangu,Wazee wangu siasa kwa sasa zimekwisha, niwaombe tu,itikadi zetu za kisiasa tulizokuwa nazo tuziweke kando, tuanze upya kwa pamoja kuijenga Mtama yetu ili ipige hatua katika suala zima la Maendeleo. Na mie kwa vile nimepata nafasi ya kuhakikisha jimbo la Mtama linapata maendeleo, basi nitahakikisha yale yote niliyowaahidi wakati wa kampeni ndani ya miaka mitano niwe nimemaliza ama kuyakupunguza kwa kiasi kikubwa", alisema Nape. (Picha na MichuziJr).

Baadhi ya wazee wakimsikiliza Mbunge wa jimbo la Mtama Mhe. Nape Nnauye alipokuwa akizungumza nao mambo mbalimbali ya kuhakikisha jimbo la Mtama na Kusini kwa ujumla inaanza kupiga hatua kimaendeleo.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lindi vijijini, Mohamed Nanyali akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wakati akimkaribisha Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Nape Nnauye ili kuzungumza na wapiga kura wake kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo Wazee maarufu wa jimbo hilo.

Baadhi ya akina Mama waliofika kumsikiliza Mbunge wao.

Mmoja wa Wananchi wa jimbo la Mtama akielezea moja ya changamoto ndani ya jimbo hilo, ambalo amemuomba Mhe. Nape alifanyie kazi.

Mh. Nape akiwa katikati ya Wazee Maarufu wa jimbo la Mtama wakisubiri chakula cha pamoja.
COMMENTS