LHRC YAWANOA VIONGOZI WA DINI KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA MPYA
HomeJamii

LHRC YAWANOA VIONGOZI WA DINI KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA MPYA

Mkurugenzi wa Baraza la Dini na Amani Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Godda, akihutubia wakati akifungua semina ya siku mbili ya viongozi...

IGP SIRRO APOKEA MSAADA WA MAGARI MANNE JIJINI DAR ES SALAAM
MHE WAZIRI MKUU AAGIZA KUSIMAMIWA KWA UTEKELEZAJI WA SHERIA ZA NCHI ZENYE LA KUMLINDA MTOTO WA KIKE
MAONESHO YA SABASABA 2017; BABA AMSAJILI MWANAE WA MIAKA 18 NA MPANGO WA "WOTE SCHEME" WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF


Mkurugenzi wa Baraza la Dini na Amani Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Godda, akihutubia wakati akifungua semina ya siku mbili ya viongozi wa dini kuhamasisha uhiishaji wa katiba mpya inayoendelea Hoteli ya Golden Tulip Posta jijini Dar es Salaam leo. Semina hiyo imeandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).


Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga akizungumza kuhusu umuhimu wa semina hiyo kwa viongozi wa dini.


Meneja Mipango Msaidizi wa (IRCPT), Rogers Fungo akizungumza katika semina hiyo.


Mwenyekiti wa Taifa wa Wanawake wa Baraza la Kiislam Tanzania (Bakwata), Shamim Khan (kulia), akizungumza katika semina ya siku mbili ya viongozi wa dini kuhamasisha uhiishaji wa Katiba mpya iliyofanyika Dar es Salaam leo. Semina hiyo imeandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)


Semina ikiendelea.


Wawakilishi kutoka taasisi za dini wakiwa kwenye semina.

Viongozi wa dini wakiwa kwenye semina.


Na Dotto Mwaibale
 

BARAZA la Uongozi la Dini na Amani Tanzania (IRCPT), limesema ipo haja mchakato wa Katiba Inayopendekezwa kufikia tamati kwa kuwa ina mambo ya msingi kwa Watanzania.

Mkurugenzi wa Baraza hilo, Mchungaji Thomas Godda amesema ni vema viongozi wa dini wakatimiza wajibu wao kwa kuihamasisha
Serikali imalize mchakato huo sanjari na kuhamasisha wananchi kusoma Katiba iliyopo ili kuwajengea uelewa mpana.

Ametoa kauli hiyo leo Dar es Salaam kwenye semina ya siku
mbili ya kuhamasisha uhiishaji wa Katiba Mpya kwa viongozi wa dini inayoendelea kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam ambayo imeandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Aliongeza kuwa viongozi wa dini si wanaharakati bali ni watu
wanaotoa uamuzi wao kwa hekima huku wakiaminiwa na wafuasi wao wakiwemo
viongozi wa serikali.
 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga amesema wameandaa semina hiyo kwa ajili ya viongozi wa dini
kwa kuwa ni watu wenye ushawishi mkubwa katika jamii ili kusukuma mchakato wa katiba mpya.
 

"Semina hii kwa viongozi hawa wa dini ni maazimio
yaliyofikiwa na viongozi wakuu wa dini katika mkutano wa kwanza tulioufanya ambapo
walitushauri tuendeshe semina kama hii kwa viongozi wa dini kutoka sehemu mbalimbali
nchini ili kuwajengea uelewa mpana wa kujua masuala ya Katiba,"
alisema Henga.
 

Mtoa mada katika Semina hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk.James Jese alisema kuna umuhimu wa sheria iliyopitishwa kuelekea upigaji wa kura ya maoni ya katiba mpya ifanyiwe marekebisho kwa kuwa imepitwa na wakati.
 

Mwenyekiti wa Taifa wa Wanawake wa Baraza la Kiislam Tanzania
(Bakwata), Shamim Khan, amesema Rais John Magufuli ameanza kuliongoza taifa kwa weledi mkubwa hivyo ni vema amalize pia mchakato wa kupata Katiba Mpya.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)













Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: LHRC YAWANOA VIONGOZI WA DINI KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA MPYA
LHRC YAWANOA VIONGOZI WA DINI KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA MPYA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiNedvEJD0wve7iEyQdWtuMso5ribbh3MASOwPy0sMqXxQm9-ZeIt_oXYJjm_ZSqJkWFNVsWnEMDOmRMWYFbHlgE_sfni4cUrlt5Rs-1dWU-q8vvAf-Esr1qGizQlZ8u32Qqlxm7ize0K3Q/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiNedvEJD0wve7iEyQdWtuMso5ribbh3MASOwPy0sMqXxQm9-ZeIt_oXYJjm_ZSqJkWFNVsWnEMDOmRMWYFbHlgE_sfni4cUrlt5Rs-1dWU-q8vvAf-Esr1qGizQlZ8u32Qqlxm7ize0K3Q/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/04/lhrc-yawanoa-viongozi-wa-dini-kuhusu.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/lhrc-yawanoa-viongozi-wa-dini-kuhusu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy