SERIKALI YATUMIA BILIONI 85 KUPELEKA MAWASILIANO VIJIJINI
HomeJamii

SERIKALI YATUMIA BILIONI 85 KUPELEKA MAWASILIANO VIJIJINI

Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Dua Nkurua, akitoa maoni kuhusu ufikishaji wa mawasiliano vijijini kwa viongozi wa Wizara ya ...

TRA YASHINDA TUZO YA UTUNZAJI BORA WA MAHESABU KWA TAASISI ZA UMMA
CHUO KIKUU ARDHI CHAKAMILISHA UJENZI NA UWEKAJI VIFAA BANDARI YA TANGA
MAKAMU WA RAIS, SAMIA SILUHU HASSAN AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA MAENEO TENGEFU YA VIWANDA VYA USINDIKAJI VYAKULA



Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Dua Nkurua, akitoa maoni kuhusu ufikishaji wa mawasiliano vijijini kwa viongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (hawapo pichani) katika kikao na Kamati hiyo mjini Dodoma. Kushoto kwake ni Mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Bhagwanji Meisuria na Katibu wa Kamati hiyo Bw. Richard Masuke.


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akifafanua jambo katika kikao na Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Moshi Kakoso na Naibu Katibu Mkuu wa Mawasiliano wa Wizara hiyo Eng. Angelina Madete.


NA WUUM, DODOMA
SERIKALI imesema kuwa imetumia shilingi Bilioni 85 kupeleka mawasiliano vijijini kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kuzipatia ruzuku kampuni za simu za mkononi ili kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata huduma za mawasiliano.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwenye Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu mjini Dodoma.
“Mfuko huu unaendelea kuhakikisha kuwa mawasiliano bora yanafika katika maeneo mengi nchini hususan vijijini na kwenye maeneo ambayo hayana mvuto wa kibiashara ambapo Takwimu zinabainisha kuwa, tayari mawasiliano yamefikishwa kwenye kata 443, vijiji 1,939 kuanzia mwezi Machi 2013 hadi Julai mwaka huu”, amefafanua Naibu Waziri Ngonyani.
Ameongeza kuwa tayari Mfuko umetiliana saini mkataba na kampuni za simu za mkononi mwezi Agosti mwaka huu kuhakikisha kuwa zinapeleka mawasiliano kwenye kata nyingine 75 na vijiji 154.
Aidha, ametanabaisha kuwa hadi hivi sasa asilimia 94 ya wananchi wanapata huduma ya mawasiliano nchini na kuongeza kuwa, Serikali kupitia mkataba wake na Kampuni ya Simu ya Halotel imefikisha mawasiliano kwenye jumla ya vijiji 3,069 kati ya vijiji 4,000 tangu walipoanza utekelezaji wa jukumu hilo mwezi Novemba, 2015 na wanatarajia kukamilisha kazi hiyo ifikapo mwezi Novemba mwaka huu.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu Mhe. Moshi Kakoso, amezitaka kampuni za simu za mkononi zinazopeleka mawasiliano vijijini na maeneo yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara ambazo zinapatiwa ruzuku na Serikali kuhakikisha kuwa zinatoa taarifa sahihi kwa Mfuko huo ikiwemo hatua zilizofikiwa za ujenzi na usimikaji wa minara na uwepo wa mawasiliano kwenye vijiji husika.
Amewataka UCSAF kujitangaza na kuweka mabango yao kwenye minara yote nchini iliyojengwa kupitia ruzuku ya Serikali ili kuwawezesha wananchi kutambua uwajibikaji wa Serikali katika kufikisha mawasiliano kwa wananchi wake.
Naye, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Eng. Angelina Madete, amesema kuwa Wizara kupitia UCSAF itahakikisha kuwa kila mwananchi anafikiwa na mawasiliano kuendana na jukumu la msingi la Mfuko huo la kufikisha mawasiliano kwa wote.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Eng. Peter Ulanga, amewahakakikishia wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu kuwa Taasisi yake itashirikiana na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuhakiki kazi zilizofanywa na kampuni za simu za mkononi za ujenzi na usimikaji wa minara na uwepo wa mawasiliano kwenye vijiji mbalimbali nchini.



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Eng. Angelina Madete akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuhusu miradi ya maendeleo ya mawasiliano vijijini katika kikao kilichofanyika mjini Dodoma.


Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu maeneo ya vijijini yaliyofikiwa na mawasiliano katika kikao na Kamati hiyo mjini Dodoma. Kulia ni Mhe. Dua Nkurua na Mhe. Rita Kabati wajumbe wa Kamati hiyo.


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Moshi Kasoso, akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Kamati hiyo katika kikao kilichowakutanisha na uongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Edwin Ngonyani.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SERIKALI YATUMIA BILIONI 85 KUPELEKA MAWASILIANO VIJIJINI
SERIKALI YATUMIA BILIONI 85 KUPELEKA MAWASILIANO VIJIJINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhS7KIBoCzJTVQ-BtOjvJGEK2UKCoLXbK9W8AEI5In3DUrO0so2Ugi3Z_Fqbijj7akcbPDhnBded8zqG1awzmhfGCg9fcztIfA8meq9-EDtiAaGLXo7zZWr1EcRpM2dgTOE6fc3kyeu92lN/s640/4.JPEG.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhS7KIBoCzJTVQ-BtOjvJGEK2UKCoLXbK9W8AEI5In3DUrO0so2Ugi3Z_Fqbijj7akcbPDhnBded8zqG1awzmhfGCg9fcztIfA8meq9-EDtiAaGLXo7zZWr1EcRpM2dgTOE6fc3kyeu92lN/s72-c/4.JPEG.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/08/serikali-yatumia-bilioni-85-kupeleka.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/serikali-yatumia-bilioni-85-kupeleka.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy