Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Fedha (TRA), Anna Mndeme kulia akipokea tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za um...
Naibu
Mkurugenzi wa Idara ya Fedha (TRA), Anna Mndeme kulia akipokea tuzo
ya utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za umma kutoka kwa Mwakilishi
wa Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw .Shogolo
Msangi katikati wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo kwa
wawasilishaji bora wa mapato kwa mwaka 2015 yaliyofanyika nje kidogo ya
jiji la Dar es Salaam wa kwana kushoto ni Mwenyekiti wa NBAA Prof.
Isaya Jairo.
Mkurugenzi
wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rioba akipokea
tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za umma baada kuwa mshindi
wa pili kutoka kwa kwa Mwakilishi wa Mhasibu Mkuu wa Serikali, Shogolo
Msangi wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo kwa
wawasilishaji bora wa mapato kwa mwaka 2015 yaliyofanyika nje kidogo ya
jiji la Dar es Salaam.
Afisa
Mkuu wa Mapato kutoka kampuni ya kutengeneza cement (Tanga Cement Plc) Pieter De Jager akiwa na tuzo ya washindi wa
jumla kwenye mashindano ya wawasilishaji bora wa mapato kwa mwaka 2015
yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mhasibu Mkuu wa Serikali, Shogolo
Msangi (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa
uwasilishaji bora wa mapato wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo
kwa mwaka 2015 iliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. (Picha Na Ally Daud-Maelezo)
Na Ally Daud-MAELEZO
MAMLAKA
ya Mapato Tanzania (TRA) imeshinda tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu
kwa taasisi za umma zilizoandaliwa na Bodi ya Ukaguzi na Wahasibu
(NBAA) kwa mwaka 2015.
Akipokea
tuzo hiyo Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Fedha (TRA) Bi. Anna Mndeme
amesema kuwa wamepata tuzo hiyo kutokana na kuwasilisha vizuri mahesabu
ya mwaka wa fedha yaliyowasilishwa kufuatana na viwango vya
uwasilishwaji vinavyozingatiwa na Bodi ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA).
“Tumefanya
vizuri na tumepata tuzo kwa kushika nafasi ya kwanza kutokana na
kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha yaliyowasilishwa kufuatana
na viwango vya uwasilishwaji vinavyozingatiwa na Bodi ya Ukaguzi na
Wahasibu (NBAA)” alisema Bi. Mndeme.
Aidha
Bi. Mndeme amesema kuwa tuzo hiyo ni chachu kwa TRA itayofanya
waendelee kujituma zaidi katika ukusanyaji na utunzaji wa mapato ili
kusaidia nchi kupata huduma bora za jamii kwa maendeleo ya taifa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA Bw. Richard
Kayombo amesema kuwa huo ni uthibitisho kwamba TRA inafanya kazi kwa
ueledi na uwazi kupelekea kupata tuzo ya heshima.
Katika
mashindano hayo Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) wameibuka washindi
wa pili huku kampuni inayotengeneza Sementi (Tanga Cement Plc)
wakiibuka kuwa washindi wa jumla kwenye tuzo hizo .
COMMENTS