Na Robert Okanda Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imevipiga stop kutoa huduma ya kuuza mafuta vituo kadhaa jijini Dar es Salaam kwa k...
Na Robert Okanda
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imevipiga stop kutoa huduma ya kuuza mafuta vituo kadhaa jijini Dar es Salaam kwa kosa la kutoa huduma hiyo pasipo kutumia mashine maalum zilizounganishwa na pampu za nishati wanazouza kwa wateja kinyume na agizo la serikali jijini Dar es Salaam leo.
Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere aliambatana na maafisa waandamizi kuendesha zoezi hilo kwa baadhi ya vituo ilhali Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alisimamia zoezi hilo kwa upande Kigamboni na kukemea vikali wale wafanyabiashara wemye tabia ya kukwepa mapato ya serikali kwa kutozingatia agizo la serikali ifikapo Tarehe 30 Agosti Mwaka jana wawe wameshafunga mashine hizo kwenye pampu za kutoa huduma hiyo ili watoapo huduma na kurudisha mikonga ya pampu hizo risiti ya huduma itolewe moja kwa moja kwenye mashine hizo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa zoezi la kufungia vituo mbalimbali, Kamishna Kichere amesema kuwa zoezi hilo ni la nchi nzima na kwa yeyote atakayeshindwa kutii sheria kwa bila shuruti alazamishwa kutii sheria hiyo kwani vituo vyote vinatakiwa kutoa huduma bila kuwepa kulipa kodi.
"Tuliwapa muda wafunge mashine hizo lakini mpaka sasa hawajatekeleza agizo hilo hivyo hatuna budi kuvifunga hivyo vituo mpaka pale watakapotekeleza matakwa ya serikali," amesema Kamshna Kichere. Tumebaini baadhi yao wamefunga mashine hizo kwa baadhi ya pampu ilhali nyingine hawajazifunga hivyo kuendelea kutudanganya kwa kuamini kwamba wamezingatia sheria wakati kiuhalisia wanaedelea kukwepa kulipa kodi.
Naye Kamishna wa Mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Elijah Mwandumbya amesema wafanyabiashara hawana budi kuzingatia sheria za nchi na kutoa huduma kwa kutumia mashine hizo kwani mpaka sasa hakuna malalamiko yaliyotolewa na wafanyabiashara wachache waadilifu wanaoutumia mashine hizo.
Ameongeza kuwa sheria kali zitachukuliwa dhidi ya wafanyabiashara wote ambao vituo vyao vya mafuta vimefungwa na wasithubutu kutoa huduma bila kutimiza masharti ya kuunganisha huduma hizo na pampu za vituo vya pia wawashirikishe TRA ili waruhusiwe kuendelea kutoa huduma hiyo.
![]() |
![]() |
Wafanyakazi wa Kampuni ya Yono Auction Mart Limited wakifunga moja ya vituo vilivyobainika kutoa huduma pasipo kuubnganishwa na mashine za kielekroniki Dar leo. |
![]() |
Wafanyakazi wa Kampuni ya Yono Auction Mart Limited wakifunga moja ya vituo vilivyobainika kutoa huduma pasipo kuubnganishwa na mashine za kielekroniki Dar leo. |
COMMENTS