MRADI WA ORIO MUARUBAINI WA TATIZO LA UMEME MKOANI KATAVI
HomeJamii

MRADI WA ORIO MUARUBAINI WA TATIZO LA UMEME MKOANI KATAVI

 NA SAMIA CHANDE, KATAVI Mradi wa Orio uliotekelezwa kwa ushirikiano wa  Serikali ya Uholanzi na Tanzania  kupitia Shirika la Umeme Tan...

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA MIMI NA WEWE MKOA WA MJINI MAGHARIBI
WAZIRI MUHONGO AKUTANA NA RAIS WA KAMPUNI YA TBEA YA CHINA
RAIS DKT MAGUFULI NA RAIS MUSEVENI WA UGANDA WASAINI TAMKO LA PAMOJA LA UTEKELEZAJI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA LA HOIMA-TANGA

 NA SAMIA CHANDE, KATAVI
Mradi wa Orio uliotekelezwa kwa ushirikiano wa  Serikali ya Uholanzi na Tanzania  kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) umesaidia kujenga kituo cha kuzalisha umeme chenye uwezo wa Megawati 2.5 ambazo zimesaidia  kumaliza tatizo la umeme Wilaya ya  Mpanda na Mkoa wa Katavi kwa ujumla.
Kwa mujibu wa Meneja wa TANESCO Mkoani  Katavi, Mhandisi Julius Sabu, kituo hicho kimesaidia kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme Mkoani humo, na kutoa umeme wa uhakika na wenye ubora.
“Kituo hicho kinahudumia Wilaya za Tanganyika, Mpanda mjini, maeneo ya Starlike na Kakese”. Aliainisha Mhandisi Sabu.
Lakini pia Kituo kimepunguza gharama za uzalishaji umeme ukilinganisha na Kituo cha zamani.
Wakaazi wa Wilaya ya Tanganyika wameishukuru Serikali na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kwa kuwaletea umeme kwani umekuwa mkombozi katika shughuli zao za kiuchumi, kama vile kuchomelea, "saloon",  na biashara ya maduka.
“Nawashauri Wananchi wenzangu, sasa ni wakati wa kuchangamkia fursa hii inayotokana na kupata umeme wa uhakika katika kukuza shughuli zetu za kiuchumi.” Alisema Mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Maneno Mtogwa mkazi wa Wilaya ya Tanganyika.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Katavi ametoa rai kwa Wananchi wa Wilaya za Tanganyika, Mpanda Mjini, maeneo ya Kakese na Starlike kujitokeza kwa wingi kwenye madawati ya huduma kwa Wateja na Ofisi za TANESCO ili kupatiwa huduma kwani TANESCO imejipanga kuwahudumia Wananchi popote walipo na kwa viwango vya hali ya juu.
 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Katavi Mhandisi Julius Sabu kiwa anakagua mashine kwenye kituo cha kuzalisha umeme cha Mpanda mkoani Katavi




 Kituo cha kufua umeme cha Mpanda Mkoani Katavi
Vijana wa Wilaya ya Tanganyika wakiwa wanachomelea mageti
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MRADI WA ORIO MUARUBAINI WA TATIZO LA UMEME MKOANI KATAVI
MRADI WA ORIO MUARUBAINI WA TATIZO LA UMEME MKOANI KATAVI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjszftzdTkOJyMnTwCvcAnkX-Ff0bOPsRnYWZOZ52m0IRf9Gtl-VNqjWSMD1jmDxfjqt_UswKSz8BhNSIgpTeXKEE1dc2yNEdWhjprlPy-QZTF-vVMT5uOyE6cz4Yjc0GK1a4oHsuYzriL_/s640/3.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjszftzdTkOJyMnTwCvcAnkX-Ff0bOPsRnYWZOZ52m0IRf9Gtl-VNqjWSMD1jmDxfjqt_UswKSz8BhNSIgpTeXKEE1dc2yNEdWhjprlPy-QZTF-vVMT5uOyE6cz4Yjc0GK1a4oHsuYzriL_/s72-c/3.png
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/02/mradi-wa-orio-muarubaini-wa-tatizo-la.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/mradi-wa-orio-muarubaini-wa-tatizo-la.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy