Na Daudi Manongi, Maelezo DODOMA. Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO NA MAZINGIRA) imelenga kupanda miti zaidi ya mil...
Na Daudi
Manongi, Maelezo DODOMA.
Serikali kupitia
Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO NA MAZINGIRA) imelenga kupanda miti zaidi ya
milioni 280 kila mwaka katika maeneo yaliyo katika hatari za kukabiliwa na hali
ya jangwa na ukame.
Hayo yamesemwa
leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (MUUNGANO NA MAZINGIRA) Mhe. January Makamba
alipokuwa akiongea na Waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya
kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa
na Ukame Duniani inayofanyika tar 17 Juni kila mwaka.
“Ukataji wa
miti kiholela na uharibifu wa misitu unaosababishwa na utegemezi mkubwa wa binadamu wa kupata mahitaji
kutokana na mazao ya misitu pamoja na
huduma zingine muhimu, kunazidisha ukubwa wa tatizo hili”,Aliongeza Mhe.Makamba.
Aidha Waziri
Makamba amesema kuwa kutokana na athari hizi Serikali imechukua hatua
mbalimbali kukabiliana na taizo hili.
Serikali imeandaa
mkakati wa Taifa wa kupanda na kutunza miti wa mwaka 2016-2021 ambao unalenga
kupunguza kasi ya uharibifu wa ardhi kwa njia ya kupanda na kutunza miti na
kuhakikisha kwamba kila mwananchi
anahusika katika utaratibu huu.
Maelekezo hayo
ni pamoja na programu za upandaji miti,kuandaa mpango bora wa matumizi ya
ardhi,kulima kilimo kinachofuata njia za kisasa,ufugaji bora na wa kisasa na
kusisitiza matumizi ya nishati mbadala ili kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa
pamoja na kuhifadhi maji katika kipindi cha mvua.
Ametoa rai kwa
wananchi wote kushiriki kikamilifu katika kutekeleza kauli mbiu ya mwaka huu.
“Kauli mbiu ya
mwaka huu ni Ardhi ni Makazi yetu Tuitunze kwa manufaa ya baadaye hivyo wananchi wote washiriki kikamilifu
katika kuitekeleza ili kuhakikisha ardhi yetu inatunzwa kwa ajili ya kizazi
kijacho”,Aliongeza Makamba
COMMENTS