Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira pamoja na wachungaji, wakiinua mikono wakati wa ibada ya Kuli...
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira pamoja na
wachungaji, wakiinua mikono wakati wa ibada ya Kuliombea Taifa Kinziga,
Salasala Jijini Dar es Salaam.
Mwimbaji
Alfonsina Samweli wa kanisa la Assemblies of God la Kinziga Salasala
Jijini Dar es Salaam akimpa Mkono Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Luhaga Mpina, baada ya kumkabidhi kabrasha lenye
DVDs zenye nyimbo za Injili wakati wa ibada ya Kuliombea Taifa.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina
akikata Utepe katika CD kuashiria kuzinduliwa kwa Abum ya Nyimbo za
Injili za mwimbaji Alfonsina Samweli.
Sehemu
ya waumini wa kanisa la Assemblies of God la Salasala wakisikiliza
hotuba ya Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano na
Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Hayupo Pichani wakati wa ibada maalumu ya
kuiombea Taifa iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)
Na Evelyn Mkokoi – Salasala DSM.
NAIBU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga
Mpina amesema Serikali ya awamu ya Tano inaongozwa na Nguvu za Mungu
katika kuwatumikia wananchi wake na si vinginevyo.
Pia
amesema Serikali ya awamu ya Tano kamwe haitayumbishwa wala kuyumba
katika kutenda yaliyomema kwa maendeleo ya nchi kwa kuogopa maneno ya
watu ya kuwakatisha tamaa.
Akizungumza
Dar es Salaam jana wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la Kusifu na Kuabudu
na kuliombea Taifa la Kanisa la Tanzania Assemblies of God lililopo
katika eneo la Kinzugi Salasala, alisema Serikali itaendelea kusimamia
misingi yake bila kuogopa maneno ya watu wanaoyoikatisha tamaa kwani
Sheria na Katiba za nchi zinatokana na maneno yaliyopo katika vitabu
vya Mungu.
Alisema
watumishi wa Mungu wanatakiwa kuwaombea viongozi katika kutenda kazi
zao kwani uongozi waliokuwa nao ni uchaguzi kutoka kwa Mungu na sio kwa
nguvu za mtu yeyote.
"
Uongozi unatokana na Mungu,Mimi Mpina sikujua kama ningekuwa Waziri
nilimaliza siku mbili sikujua kama niliteuliwa kuwa Naibu Waziri kipindi
hicho nilikuwa shambani nikafatwa na kuambia kuwa nimechaguliwa
,nikasema ni uweza wa Mungu,"alisema na kuongeza kuwa
"Utawala
wa awamu ya tano tunemtanguliza mbele Mungu,tunaomba muendelee
kutuombea tutekeleze majukumu yetu licha ya kuwepo kwa vikwazo
mbalimbali katika kutekeleza majukumu yetu,"alisema Mpina
Aidha
aliziomba familia za wakristo kuwa mfano wa kuigwa katika utunzaji wa
mazingira kwani bila kuwepo kwa mazingira safi magonjwa yatapata nafasi
katika jamii.
"Familia
za Kikristo lazima ziwe mfano wa kuigwa katika utunzaji wa mazingira,
hizi faini tunazowapiga watu kutokana na ukiukwaji wa sheria za
mazingira kwa uchafuzi wa Mazingira, sio kama tunawaonea bali
kuwakumbusha wajibu wao "alisema.
Kwa
Upande wake,Mchungaji wa Kanisa la Assembly of God , Deusi Sabuni
alisema watahakikisha wanaendele kufanya Maombi kuiombea serikali ya
awamu ya tano na viongozi wake.
Alisema
roho za uadui zilizopo na watu kusema vibaya na kuwakatisha tamaa
kusiwavunje mioyo kwa kusikiliza maneno ya watu katika kuleta maendeleo
ya nchi kwa manufaa ya taifahili na watu wake."Makanisa na Misikiti
tupo pamoja nanyi katika kuwaombea na kama serikali hii ikiendelea hivi
ndani ya miaka mitatu nchi yetu itabadilika,"alisema Mch.Sabuni.
Ibada
maalum ya Kuliombea Taifa, kusifu pamoja na kuimba, ilienda sambamba na
uzinduzi wa Ablum ya nyimbo za injili za mwimbaji Alfonsina Samweli
pamoja na mnadawa kuuza DVDs zenye nyimbo za injili.
COMMENTS