NA K-VIS BLOG/Mashirika ya Habari KOREA Kaskzini, imetengeneza tetemeko la ardhi lenye ukumbwa wa 6.3 vipimo vya Richa, l...
NA K-VIS BLOG/Mashirika ya Habari
KOREA Kaskzini, imetengeneza tetemeko la ardhi lenye ukumbwa wa 6.3 vipimo vya Richa, likiwa ni kubwa kuliko lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, 2016 ambalo lilikuwa na uzito wa 5.7 vipimo vya Richa.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa, wabaya wake Korea Kusini tayari wamesema, Korea Kaskazini imefanya jaribio la sita la kombora la Nyuklia na wala sio tetemeko la Ardhi. Tetemeko hilo limetokea mchana wa Septemba 2, 2017 kwa saa za huko ambayo ni sawa na majira ya asubuhi Septemba 3, 2017 kwa saa za Bongo
Kwa mujibu wa Mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa ya Marekani, (USGS), tetemeko hilo limekwenda umbali wa kilomita 10 chini ya ardhi limetokea eneo la Kaunti ya Kilju ambako mitambo ya majaribio ya makombora ya nyuklia huko Punggye-ri imejengwa.
Korea Kusini imeitisha kikao cha baraza la usalama la nchi hiyo, kujadili tetemekeo hilo la “kutengeneza”.
Habari nyingine zinasema, Katika eneo hilo hilo pametokea tetemeko lingine lenye ukubwa wa kipimo cha 4.6 kipimo cha richa.
Habari nyingine zinasema, Katika eneo hilo hilo pametokea tetemeko lingine lenye ukubwa wa kipimo cha 4.6 kipimo cha richa.
COMMENTS