SERIKALI YAITAMBUA RASMI MITANDAO YA KIJAMII (BLOGGERS)
HomeJamii

SERIKALI YAITAMBUA RASMI MITANDAO YA KIJAMII (BLOGGERS)

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas, akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa M...







Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas, akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi.
Meneja Mwandamizi wa Amana Huduma za Bima na Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili, akizungumza katika mkutano huo kuhusu masuala mbalimbali ya benki hiyo ambayo ni moja ya mdhamini wa mkutano huo.
Mwanahabari na Blogger  Frederick Katulanda, akiuliza swali.
Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi, akiwaelekeza jambo mablogger
Mablogger wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.


Mablogger kazini


Blogger Baraka kutoka Bukoba akiuliza swali.
Mwezeshaji wa mkutano huo Maxsence  Mello akitoa mada.
Meza kuu. Kutoka kulia ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo, Kranty Mwantepele.Meneja Mwandamizi wa Amana Huduma za Bima na Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili,Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas, Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi pamoja na Katibu wa muda wa TNB, Khadija Kalili.


Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi, akizungumza kwenye mkutano huo.


Bloggers wakifuatilia mada.
Blogger Mroki Mroki akiwa kazini wakati wa mkutano huo.

Mgeni rasmi akihutubia.
Mwendeshaji wa mtandao wa FullShangwe, John Bukuku akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Maofisa wa Kitengo cha Uhusiano wa Benki ya NMB wakibadilishana mawazo. Kushoto ni Doris na Joyce Nsekela.
Blogger kutoka mkoani Arusha, Tumaniel Seria, akiuliza swali. Kushoto ni William Malecela mmiliki wa mtandao wa Mwananchi na (katikati) ni mmiliki wa Blog ya Michuzi, Issa Michuzi.




Mmiliki wa mtandao wa Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda akichangia jambo.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Picha ya pamoja.

Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imetangaza rasmi kuitambua mitandao ya Kijamii (Bloggers) kuwa chombo cha habari nchini.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas Dar es Salaam leo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN).

"Serikali sasa inaitambua rasmi mitandao ya kijamii kuwa ni chombo cha habari kama ilivyo vyombo vingine nchini hivyo nawaomba wakuu wa vitengo vya habari serikalini kushirikiana na wanamitandao hiyo katika kutoa taarifa mbalimbali" alisema Abbas.

Abbas alivitaka vyombo vya habari hasa magazeti pale wanapotumia picha kutoka mitandao ya kijamii kueleza chanzo cha picha hiyo tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo picha zao zinatumika bila ya kutaja chanzo.

Katika hatua nyingine Abbas alisema Bloggers haina tofauti na vyombo vingine hivyo ni vema wanapotoa habari zao kuzingatia sheria na weredi wa kazi vinginevyo sheria itawakumba kama ilivyo kwa magazeti na vyombo vingine. 

Abass aliwataka wanamitandao hao kujiunga na TBN ili iwe rahisi kutatuliwa changamoto walizonazo kuliko kila mmoja kuwa kivyake.

Wanamitandao hao  wakizungumzia changamoto waliyonayo walimwambia mkurugenzi huyo kuwa  wamekuwa wakibaguliwa na maofisa habari wa serikalini ikiwa pamoja na kunyimwa 'Press Card' jambo linalokwamisha utendaji wao wa kazi.


Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SERIKALI YAITAMBUA RASMI MITANDAO YA KIJAMII (BLOGGERS)
SERIKALI YAITAMBUA RASMI MITANDAO YA KIJAMII (BLOGGERS)
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgzgBpYwr-xVQFdfDfz2-NaaYCSG6mr8xTFe4dRHqv_MpFXYI_h65AW0fnyDG3szTRpADZGg5Y1WES42w42WX4Kq6tZwKYj9FkjppXRkdihmBGXLaxlPqriUkzjKGcQRUIZQJe2eH17eBNp/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgzgBpYwr-xVQFdfDfz2-NaaYCSG6mr8xTFe4dRHqv_MpFXYI_h65AW0fnyDG3szTRpADZGg5Y1WES42w42WX4Kq6tZwKYj9FkjppXRkdihmBGXLaxlPqriUkzjKGcQRUIZQJe2eH17eBNp/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/12/serikali-yaitambua-rasmi-mitandao-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/serikali-yaitambua-rasmi-mitandao-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy