WAZIRI LUKUVI AELEZA MABORESHO YALIYOFANYIKA KATIKA SEKTA YA ARDHI
HomeJamii

WAZIRI LUKUVI AELEZA MABORESHO YALIYOFANYIKA KATIKA SEKTA YA ARDHI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya kazi; Mhe. William Lukuvi ametaja maboresho kadhaa yaliyofanyika katika Wizara ya Ardhi. Mhe. L...

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AFANYA MKUTANO NA WAHARIRI ILI KUONGEZA UELEWA WA MIFUMO MIPYA KUHUSU UAGIZAJI WA MBOLEA KWA PAMOJA
WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AZINDUA KITABU KATIKA UFUNGUZI WA SHEREHE ZA KUADHIMISHA MIAKA 10 YA CHUO KIKUU ARDHI
KONGAMANO LA WASOMI WANATAALUMA KUFANYIKA LEO HOTELI YA LANDMARK UBUNGO DAR ES SALAAM


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya kazi; Mhe. William Lukuvi ametaja maboresho kadhaa yaliyofanyika katika Wizara ya Ardhi.
Mhe. Lukuvi aliyasema hayo alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwl. Nyerere; Mzee Joseph Butiku alipofika ofisini kwake leo, katika kanda ya ofisi ya Ardhi - Dar es Salaam.
Akieleza Maendeleo yanayofanyika sasa katika eneo la Urasimishaji; Mhe Lukuvi alieleza kuwa zoezi la Urasimishaji sasa linaendelea kwa kasi, na kutolea mfano wa Jiji la Mwanza kuwa zoezi hilo linafanyika kwa mafanikio makubwa. Alisema; “Mpaka sasa viwanja 35,000 vimeshapimwa na Hati 12,000 kutolewa  katika wilaya za Ilemela na Nyamagana.
Mhe. Lukuvi alisema baadhi ya maeneo mengine ambayo yamefanya zoezi la Urasimishaji kwa kiwango cha kuridhisha ni pamoja na Kimara na Makongo ambapo Wananchi wenyewe wamekuwa wahusika wakuu katika kuhakikisha kuwa wamezingatia miongozo waliopewa na Wizara kufanikisha zoezi hilo, ikiwepo kuzingatia kuainisha miundombinu muhimu kama  njia za barabara, maji , umeme n.k.
Akiendelea kufafanua jinsi eneo la Upimaji wa viwanja lilivyoboreshwa. Mhe. Waziri ameeleza kuwa sasa kuna kampuni 48 za upimaji ambazo zimesajiliwa na kuidhinishwa na Wizara, na zinazoendelea  sasa na kufanya upimaji wa viwanja katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha, Mhe . Lukuvi ameeleza kuwa katika maeneo ya Vijijini pia kasi ya  upangaji wa Matumizi bora ya Ardhi imekuwa ya kuridhisha, tofauti na miaka ya zamani.  Hatahivyo alieleza kuwa changamoto zipo, hususani katika mkoa wa Morogoro; katika maeneo ya Mvomero, Kilombero na mengineyo lakini Serikali inaendelea na jitihada za kufanya taratibu za upangaji wa Matumizi bora ya Ardhi na kufanya upimaji wa maeneo kwa kasi kubwa zaidi katika maeneo hayo.  
Vile vile Mhe. Lukuvi amesema katika kuboresha ulinzi wa Hati za Ardhi; Hati sasa zipo katika taratibu za kuandaliwa na kutolewa Kielektroniki. Alisema, Hati hizo za Kielektroniki zitathibiti mianya yote ya ulaghai  na rushwa, matendo ambayo yamekuwa yakifanywa kwa muda mrefu na matapeli mbalimbali na kusababisha vilio kwa Wananchi wengi. Pia kwa Mfumo huo wa Kielektroniki kila Mmiliki wa Ardhi, atalazimika kuwajibika ipasavyo katika kulipa Kodi ya Pango la Ardhi.
Naye Mzee Butiku amempongeza Mhe. Lukuvi katika juhudi zake za kuendelea kuboresha huduma zinazofanywa na Wizara hiyo na kumsihi kuendelea na jitihada hizo. Alisema; “Nikilinganisha hali iliyokuwepo Wizarani nyakati za nyuma na sasa, maboresho ni makubwa, endelea na juhudi unazozifanya”.
(NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI)



 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya kazi, Mhe. William Lukuvi akionyesha muonekano wa Hati ya Kielektroniki inavyotarajiwa kuwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwl. Nyerere; Mzee Joseph Butiku alipofika ofisini kwake leo, katika kanda ya ofisi ya Ardhi - Dar es Salaam.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya kazi, Mhe. William Lukuvi akionyesha moja ya ramani za Mipango Miji kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwl. Nyerere, Mzee Joseph Butiku alipofika ofisini kwake leo, katika kanda ya ofisi ya Ardhi - Dar es Salaam
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya kazi, Mhe. William Lukuvi akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwl. Nyerere, Mzee Joseph Butiku na msaidizi wake walipofika ofisini kwake leo, katika kanda ya ofisi ya Ardhi - Dar es Salaam.
Na kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI LUKUVI AELEZA MABORESHO YALIYOFANYIKA KATIKA SEKTA YA ARDHI
WAZIRI LUKUVI AELEZA MABORESHO YALIYOFANYIKA KATIKA SEKTA YA ARDHI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjihDfLDp_7xDUu1gLmLhiSJX9SwEr2_TtVC1JyYY82TFg4H0Pf9R2fnZPi3xGb_KidO-ufIOVtPZx1hKa13M7awA_HU2Mq6jWwuVSs1rtYkiLINtlwtvr0ik0Lz8Gwtc4-8ZQYuFiDT6A/s640/picha+a.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjihDfLDp_7xDUu1gLmLhiSJX9SwEr2_TtVC1JyYY82TFg4H0Pf9R2fnZPi3xGb_KidO-ufIOVtPZx1hKa13M7awA_HU2Mq6jWwuVSs1rtYkiLINtlwtvr0ik0Lz8Gwtc4-8ZQYuFiDT6A/s72-c/picha+a.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/waziri-lukuvi-aeleza-maboresho.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/waziri-lukuvi-aeleza-maboresho.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy