WASAFIRI WATAHADHARISHWA KUPATA CHANJO YA HOMA YA MANJANO
HomeJamii

WASAFIRI WATAHADHARISHWA KUPATA CHANJO YA HOMA YA MANJANO

Waziri wa Viwanda,Biashara naUwekezaji Mhe. Charles Mwijage kulia akipokea cheti cha chanjo cha kimataifa kijulikanacho kama cheti cha hom...

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA BALOZI WA UFARANSA NA MKURUGENZI MKAZI WA WFP
MATUKIO PICHA; WAZIRI MIPANGO ALIPOWASILISHA MAPENDEKEZO YA SERIKALI YA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA NA YA KIWANGO NA UKOMO WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2018/2019
KAMPUNI BINAFSI ZA ULINZI KUWA NA SARE MOJA.




Waziri wa Viwanda,Biashara naUwekezaji Mhe. Charles Mwijage kulia akipokea cheti cha chanjo cha kimataifa kijulikanacho kama cheti cha homa ya manjano kutoka kwa Afisa Afya Bw. Fadhili Kilamile mara baada ya kupata chanjo hiyo leo kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Zungu wa kwanza kulia akisubiria kupewa cheti cha chanjo cha kimataifa kijulikanacho kama cheti cha homa ya manjano kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengocha Afya Mipakani Bw. Remidius Kakulu kushoto mara baada ya kupata chanjo hiyo leo kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma.
MbungewaVitiMaalumjimbo la SingidaMhe. Martha Mlatawa kwanza kuliaakiandikiwacheti cha chanjo cha kimataifakijulikanachokamacheti cha homayamanjanokutokakwa Afisa Afya Agnes Shirima katikatimarabaadayakupatachanjohiyoleokwenyeviwanjavyabungemjini Dodoma aliyesimamani Afisa Habari wa WizarayaAfya Bi. Catherine Sungura.

…………………………

Na.Catherine Sungura, WAMJW

Dodoma


Watanzania hususan wale wanaosafiri nje ya nchi zile zenye ugonjwa wa homa ya manjano wanatakiwa kujitokeza kwenye vituo vilivyoainishwa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kwa ajili ya kupata chanjo hiyo pamoja na kubadilisha vyeti vipya.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakati alipofika kupata huduma ya chanjo ya homa ya manjano ambayo inatolewa bungeni hapa

Waziri Mwijage amesema duniani ugonjwa huu upo na zipo nchi nyingi ambazo zimepoteza wananchi wake kwa kuugua ugonjwa huo“Suala hili ni muhimu sana kwa afya zetu,pamoja na kwamba nchi yetu haina mgonjwa wa homa ya manjano

Aidha amesema maambukizi ya ugonjwa huu endapo mtu ataupata gharama za matibabu yake ni ghali sana na inaweza kupelekea kupoteza maisha,hivyo ni vyema kujitokeza kwa wingi kupata chanjo hiyo pamoja na kubadilisha kadi zao kwani usiweke reheni maisha yako

Hata hivyo aliwatahadharisha wafanyabiashara,wanafunzi wale wanaosafiri au kusoma nje ya nchi ni vyema wahakikishe wanapata chanjo hiyo kuliko kupewa kadi kwa njia nyingine kwani kadi hizi zimeboreshwa na zina alama za siri ambazo nchi za kimataifa zina uwezo wa kusoma alama zetu.

Naye Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe.Mussa Zungu ameipongeza Wizara ya Afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto kwa kubadilisha kadi hizi mpya kwa kuepukana na vyeti vingi ambavyo vilikua vinanunuliwa mtaani bila kupata huduma za kupata chanjo,hivyo ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanapata chanjo hizo kwani ilikua ni hatari sana hususan nchi zile zenye milipuko wa homa za manjano na hivyo kupata vyeti ambavyo ni halali

Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto limeongeza muda wa kubadilisha vyeti vya zamani hadi mwisho wa mwezi huu na baada ya hapo vyeti vya zamani havitatambulika tena.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WASAFIRI WATAHADHARISHWA KUPATA CHANJO YA HOMA YA MANJANO
WASAFIRI WATAHADHARISHWA KUPATA CHANJO YA HOMA YA MANJANO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhHjEsUoVZB9-t34BO31GALLDrIuimXEhrqiAR8GkAUioRA0FbAT_XUNe-9BeW-FKyXM9KfZ6WhLY1bBs_5CW4e9jOvS8bxI81g3iiNSJz0cIluTG7XWp1GPKy2lTQmbcDo7GgMeDhYGl4/s640/ZA-3.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhHjEsUoVZB9-t34BO31GALLDrIuimXEhrqiAR8GkAUioRA0FbAT_XUNe-9BeW-FKyXM9KfZ6WhLY1bBs_5CW4e9jOvS8bxI81g3iiNSJz0cIluTG7XWp1GPKy2lTQmbcDo7GgMeDhYGl4/s72-c/ZA-3.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/05/wasafiri-watahadharishwa-kupata-chanjo_5.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/wasafiri-watahadharishwa-kupata-chanjo_5.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy