KAMPUNI BINAFSI ZA ULINZI KUWA NA SARE MOJA.
HomeJamii

KAMPUNI BINAFSI ZA ULINZI KUWA NA SARE MOJA.

Na Jeshi la Polisi. Kampuni binafsi za ulinzi zinazoendesha shughuli zake hapa nchini zimetakiwa kuvaa sare za aina moja ifikapo Januari...

MCHUNGAJI DR GEORDAVIE AWASIHI JAMII KUJENGA TABIA YA KUSAIDIA YATIMA
USIKU WA ZUBEIR IMANI NA ZAWADI MOHAMED WAFANA
MWIMBAJI MAARUFU WA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA AFUNGA PINGU ZA MAISHA

Na Jeshi la Polisi.
Kampuni binafsi za ulinzi zinazoendesha shughuli zake hapa nchini zimetakiwa kuvaa sare za aina moja ifikapo Januari Mosi mwakani kwa lengo la kuondoa sare ambazo zimekuwa zikifanana na zinazovaliwa na askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Agizo hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii, Mussa Alli Mussa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa kikao kilichowakutanisha wamiliki wa kampuni binafsi za ulinzi.
Kamishna Mussa amesema sare zilizokubaliwa kwa pamoja kati ya Jeshi la Polisi na wawakilishi wa kampuni binafsi za ulinzi zinatakiwa ziwe na rangi ya bluu nyeusi (Dark blue), nyeusi pamoja na mashati meupe kulingana na mazingira ya kampuni inapofanyia ulinzi.
“Kampuni zote binafsi za ulinzi hakikisheni mnajiandaa mapema kwa kuwa muda utakapofika hakuna kampuni binafsi ya ulinzi itakayoruhusiwa kufanya kazi bila ya kutumia sare hizi ambazo zitakuwa ni utambulisho rasmi wa sekta hii binafsi ya ulinzi” Alisema Mussa.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha wamiliki wa kampuni binafsi za ulinzi (TAPSCOA)  Bw. Shawiniaufoo Kimuto amesema kuwepo kwa aina moja ya sare kutasaidia kuondoa mgongano uliopo hivi sasa ambapo baadhi ya kampuni zinavaa sare zinazofanana na zinazovaliwa na vyombo vya ulinzi na usalama.
Kimuto alisema jambo hilo litasaidia kufahamika kwa urahisi kwa walinzi wa kampuni binafsi na hivyo kuwa rahisi kupata msaada pindi wanapotekeleza majukumu yao ya kulisaidia Jeshi la Polisi kuhakikisha usalama unakuwepo katika maeneo wanayofanyia kazi.

Naye Julieth Rushuli kutoka kampuni binafsi ya ulinzi ya 4JY amesema Sekta binafsi ya ulinzi imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa usalama unaimarika katika maeneo yao hivyo jamii inapaswa kuwapa ushirikiano pindi wanapotekeleza majukumu yao.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KAMPUNI BINAFSI ZA ULINZI KUWA NA SARE MOJA.
KAMPUNI BINAFSI ZA ULINZI KUWA NA SARE MOJA.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiPp8Qqn9winAMZza80jzPkDgaz55GFpl1TS5rzKvjT13curFe4EK0zDLcycVjs9LfCVTuwi-2wmaGeWO6xVsJbOpvK8zI1IzpmUxk-skUVWE2v6HTkgzQ7-toIaBXpQv7C9-2cyhPGvFY/s400/Kamishna+wa+Kamisheni+ya+Ushirikishwaji+wa+Jamii%252C+Mussa+Alli+Mussa.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiPp8Qqn9winAMZza80jzPkDgaz55GFpl1TS5rzKvjT13curFe4EK0zDLcycVjs9LfCVTuwi-2wmaGeWO6xVsJbOpvK8zI1IzpmUxk-skUVWE2v6HTkgzQ7-toIaBXpQv7C9-2cyhPGvFY/s72-c/Kamishna+wa+Kamisheni+ya+Ushirikishwaji+wa+Jamii%252C+Mussa+Alli+Mussa.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/kampuni-binafsi-za-ulinzi-kuwa-na-sare.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/kampuni-binafsi-za-ulinzi-kuwa-na-sare.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy