TANESCO YAKABIDHI MRADI WA UMEME KWENYE SHULE YA MSINGI GARAGAZA HUKO KIBAHA
HomeJamii

TANESCO YAKABIDHI MRADI WA UMEME KWENYE SHULE YA MSINGI GARAGAZA HUKO KIBAHA

  Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), mkoa wa Pwani, Mhandisi Martin Madulu, (kushoto), akipena mikono na Afisa Elimu, (Ta...

RAIS MAGUFULI ATEUA WENYEVITI WAWILI WA BODI.
MATUKIO MBALIMBALI YLIYOJIRI JIJINI DODOMA MEI 15 2018
UFUNGUZI WARSHA YA MAAFISA HABARI ATAWAS


 Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), mkoa wa Pwani, Mhandisi Martin Madulu, (kushoto), akipena mikono na Afisa Elimu, (Taaluma), mkoawa Pwani, Bw.Shirley Membi Swai, wakati wa makabidhiano ya mradi wa uwekaji umeme katika shule ya Msingi Galagaza, kata ya Msangeni, Kibaha kwa Mfipa mkoani Pwani, Aprili 7, 2017. Mradi huo una thamani ya Shilingi Milioni 10. Anayeshuhudia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Shaaban Langweni





NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limekabidhi mradi wa umeme kwenye majengo ya shule ya msingi Galagaza iliyoko, kata ya Msangani wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.
Akikabidhi mradi huo wenye thamani ya Shilingi Milioni 10, wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo leo Aprili 7, 2017, Meneja wa TANESCO, Mkoani Pwani, Mhandisi Martin Madulu, alisema “mradi ulihusisha utandazaji nyaya za umeme (wiring installation), ufungaji wa power circuit- breaker, taa, pamona na ufundi kwenye majengo yote ya shule ikiwemo ofisi ya walimu”. Alifafanua meneja huyo. Akifafanua zaidi, Mhandisi Madulu alisema, “tumeona tuwaunge mkono shule kwenye level ya msingi kwani ni maandalizi mazuri kwa wataalamu wa baadaye kwani sasa mazingira yatakuwa mazuri kwa kusoma, pia mazingira yatakuwa mazuri kwa walimu kuandaa masomo yao na tunaamini italeta matokeo chanya.” Alisema.
Alisema, TANESCO imeamua kusaidia shule hiyo katika harakati za shirika kurudisha sehemu ya faida kwa wananchi, lakini pia kuhamasisha umma kutumia umeme.
“Ni fursa kwenu kutumia vizuri umeme huu, ili muweze kufanya vizuri zaidi katika masomo yenu, tunategemea kiwango cha ufaulu kitaongezeka kwani hivi sasa mnaweza kutumia fursa mbalimbali za kupata elimu kama matumizi ya kompyuta, ambazo zinahitaji uwepo wa umeme.” Alifafanua. Akipokea mradi huo, Afisa Elimu (Taaluma) wa Mkoa wa Pwaniambaye alimwakilisha Afisa Elimu wa Mkoa huo, Shirley Membi Swai, aliishukuru TANESCO kwa msaada huo na kuwataka wanafunzi na walimu kutumia vizuri uwepo wa umeme shuleni hapo kuongeza ufaulu wa wanafunzi kwani sasa mazingira ya kusoma ni mazuri zaidi.

Huu ni mchango mkubwa sana katika maendeleo ya elimu nchini, msaada huu umekuja kwa muda muafaka kwani hivi sasa, serikali tayari imeanza kufundisha TEHEMA katika shule na kufundisha kwa kutumia mtandao (digital learning na tayari umeshaanza hapa nchini, ambapo wanafunzi na walimu wameanza kutumia kompyuta ndogo (tablets).” Alisema. Pia nawashukuru TANESCO kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwapatia wanafunzi elimu bure, msaada huu unaongeza chachu ya kufanikisha azma hiyo ya serikali.
Mhandisi Martin Madulu, akitoa hotuba yake
 Bw.Shirley Membi Swai, akitoa hotuba yake
 Afisa Uhusiano wa TANESCO, Salama akizungumza wakati wa utangulizi wa hafla hiyo.
 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Galagaza
 Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Galagaza, Shaaban Lagweni, akiwatambulisha walimu wenzake.
Sehemu ya majengo yaliyowekewa umeme na TANESCO kama msaada.
 Wanafunzi wakipiga makofi kushangilia hotuba.
 Mwalimu Echi Mkopi, akisoma risala.
 Kwaya ya shule ikiburudisha.
 Mgeni rasmina uongoziwa TANESCO wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananfunzi.
 Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), mkoa wa Pwani, Mhandisi Martin Madulu (kushoto), akimuonyesha Afisa Elimu (Taaluma), Shirley Membi Swai, moja ya vifaa vilivyofungwa na TANESCO katika mradi huo.

Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO mkoa wa Pwani waliohudhuria hafla hiyo wakibadilishana mawazo.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TANESCO YAKABIDHI MRADI WA UMEME KWENYE SHULE YA MSINGI GARAGAZA HUKO KIBAHA
TANESCO YAKABIDHI MRADI WA UMEME KWENYE SHULE YA MSINGI GARAGAZA HUKO KIBAHA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEisQgRNARRbxzjDGRud8saDrVTV8NgzvkJ7PEbPHCxzNQgwpj04hO-ljOaQtPSfEJK8pze2mUohLeQxqYwM6v-70vMluA-kpbFnkAqZV5zcPRVofjVxm_IFz3IBoQok0_7Dv62XZvXZRsU/s640/pix1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEisQgRNARRbxzjDGRud8saDrVTV8NgzvkJ7PEbPHCxzNQgwpj04hO-ljOaQtPSfEJK8pze2mUohLeQxqYwM6v-70vMluA-kpbFnkAqZV5zcPRVofjVxm_IFz3IBoQok0_7Dv62XZvXZRsU/s72-c/pix1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/04/tanesco-yakabidhi-mradi-wa-umeme-kwenye.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/tanesco-yakabidhi-mradi-wa-umeme-kwenye.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy