KANUNI ZA MAADILI YA TAALUMA YA MAWASILIANO KWA UMMA KUANDALIWA
HomeJamii

KANUNI ZA MAADILI YA TAALUMA YA MAWASILIANO KWA UMMA KUANDALIWA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicolaus William(kushoto) na Rais wa Chama cha Uhusiano wa Umma ...

JARIDA LA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU LA MWEZI SEPTEMBA, 2016
MAHAFALI YA 13 YA KIDATO CHA NNE SHULE YA SEKONDARI BWAWANI YAFANA MKOANI PWANI
WAKAZI WA DAR WABOMOLEWA NYUMBA 150, LEO KUTUA KWA MKUU WA WILAYA KUPELEKA KILIO CHAO


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicolaus William(kushoto) na Rais wa Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST)  Bw.Loth Makuza (kulia) wakionyesha Katiba ya chama hicho kwa wanataaluma ya mawasiliano kwa umma waliyohudhuria uzinduzi wa chama hicho (hawapo pichani)   leo jijini Dar es Salaam.
NA ANITHA JONAS – WHUSM
Idara ya Habari Maelezo pamoja na Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) wametakiwa  kuungana kwa pamoja na kuandaa Kanuni za Maadili ya Taaluma ya Mawasiliano kwa Umma kwa kuzingatia maslai ya taifa.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicolaus William alipokuwa akizindua chama cha PRST chenye lengo la kuongeza ueledi kwa wanataaluma ya mawasiliano kwa umma nchini .
“Ningependa kuona chama hichi kinakuwa mstari wa mbele katika kutoa mafunzo mbalimbali kwa wanataaluma wake kama lilivyolengo kuwa chama kitajikita zaidi katika kuongeza weledi kwa wanatansia pamoja na kuleta mabadiliko ya kiutendaji katika sekta ya mawasiliano nchini kwa kulingana na mahitaji ya soko,” Bw.William.
Akiendelea kuzungumza katika uzinduzi huo Naibu Katibu Mkuu huyo alisisitiza kuwa ni vyema wadau wote wa taaluma ya mawasiliano kwa umma watambue umuhimu wa chama hichi kwani wao ndiyo wenye dhamana ya kukikuza, kukiendeleza na kukijengea misingi imara itakayodumu na kuleta tija ndani ya taifa.
Kwa upande wa Mwakilishi wa Msemaji Mkuu wa Serikali kutoka Idara ya Habari Maelezo, Jonas Kamaleki alieleza kuwa serikali inaunga mkono jitihada za kuanzishwa kwa PRST na iko tayari kutoa ushirikiano wakati wote.
“Serikali ingependa chama hichi kuwa na mikakati madhubuti na utekelezaji  wenye tija na hata kuwa mfano kwa Afrika Mashariki bila ya kujali kuchelewa kwa kuanzishwa kwake,”Bw.Kamaleki.
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Shule ya Habari na Mawasiliano kwa Umma Dkt.Dietrick Kaijanangoma alitoa nasaha kwa Maafisa Uhusiano wa taasisi mbalimbali nchini ya kuwataka kuwa wabunifu na kufanya tafiti ndogo na kubwa kwa ajili ya kuimarisha taasisi zao na zaidi kujifunza kwenda na wakati kwa kutambua mahitaji ya umma.
Pamoja na hayo nae Rais PRST Bw.Loth Makuza alitoa shukrani kwa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania  Awamu ya Tatu Mhe.Benjamin William Mkapa kwa kuanzisha sekta ya habari nchini
Halikadhalika Bw.Makuza alitoa ombi kwa taasisi mbalimbali kuunga mkono uanzishwaji wa chama hicho  pamoja na wanataaluma kujitokeza kwa wingi na kujiunga na chama utaratibu wa kujiunga unapatikana kupitia tovuti ya www.prst.or.tz.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nicolaus William (wa tatu kushoto) akikata utepe wa Katiba ya Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) kuashiria kuzinduliwa kwa chama hicho leo jijini Dar es Salaam,aliyeshika Katiba hiyo (kulia) ni Rais wa PRST, Loth Makuza.

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nicolaus William (wa nne kushoto) akimkabidhi cheti Innocent Mungy kilichotolewa na uongozi wa chama Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST)  kwa kutambua mchago wake katika kuanzishwa kwa chama hicho mara baada ya uzinduzi wake jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya viongozi wa Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nicolaus William (aliyeketi wanne kushoto) mara baada ya uzinduzi wa chama hicho leo jijini Dar es Salaam na  watatu kutoka kulia) ni Rais wa PRST, Loth Makuza.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KANUNI ZA MAADILI YA TAALUMA YA MAWASILIANO KWA UMMA KUANDALIWA
KANUNI ZA MAADILI YA TAALUMA YA MAWASILIANO KWA UMMA KUANDALIWA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhJPOiUEBkYsz9_Ooi2kbovQx3VUlq267pzrc-x7BBd5tLjMnkJRqlIhcR8tF6x7YgEJNepNSZuitPSYA6ZJe_RAhsCXFnvOfzlVQzqdwKj3udYWMW5oy3tXIFREZYrtqo_quhzxT3sT-wS/s640/PIX+2.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhJPOiUEBkYsz9_Ooi2kbovQx3VUlq267pzrc-x7BBd5tLjMnkJRqlIhcR8tF6x7YgEJNepNSZuitPSYA6ZJe_RAhsCXFnvOfzlVQzqdwKj3udYWMW5oy3tXIFREZYrtqo_quhzxT3sT-wS/s72-c/PIX+2.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/12/kanuni-za-maadili-ya-taaluma-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/kanuni-za-maadili-ya-taaluma-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy