Mwili wa aliyewahikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ukiwasili katika kiwanja cha Graduation Square MUHAS ukisindikiz...
Mwili wa aliyewahikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ukiwasili katika kiwanja cha Graduation Square MUHAS ukisindikizwa na wanataaluma April 11, 2017 ambapo mwili unatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni April 12, 2017 Jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru (kulia) akiangalia mwili wa Marehemu Profesa Maselle ukishushwa toka katika gari maalumu lililokuwa limebeba mwili huo jana, wapili kulia ni Profesa Ayubu Magimba
Mwili wa aliyewahi kuwa Mkurugenzi Hospitali ya Taifa Muhimbili Ukiwasili katika kiwanja cha Graduation SQuare Muhas ambapo taratibu za kutowa heshima za mwisho zilifanyika jana April 11, 2017 na leo April 12, 2017 mwili huo unatarajiwa kupumzishwa katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Wanataaluma mbalimbali wakiwa wanaushusha mwili wa mpendwa wao marehemu Profesa, Samuel Maselle kwa maandalizi ya kutowa heshima za mwisho jana
Baadhi ya viongozi katika meza Kuu akiwemo Profesa, Ephata Kaaya (wa tatu kushoto) wapilikushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa, Lawrence Museru na wa kwanza kushoto ni Profesa Ayub Magimba
Baadhi ya wanafamilia na wana Taaluma wa MUHAS
Kaimu Mkuu wa Shule ya Tiba (MUHAS) Dkt. Erasto Mbugi akisoma wasifu wa Marehemu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru akisoma wasifu kwa niaba ya Hospitali ya Taifa na kutoa Rambirambi kwa niaba ya wafanyakazi wa hospitali hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janab akisoma wasifu wa Marehemu Maselle kwa niaba ya Taasisi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa, Muhimbili (MOI) Dkt. Respicious Boniface akisoma wasifu kwa niaba ya Taasisi hiyo na kutowa Rambirambi kwa niaba ya wafanyakazi wake.
Ndugu wa Marehemu akishukuru kwa wote waliyojitolea kwa hali na mali kushirikiana na familia bega kwa bega kusaidia kuokoa maisha ya ndugu yao na hata mlipo sikia ndugu yetu katutoka hamkutuacha peke yetu na mmekuwa mstari wa mbele kufanikisha shughuli nzima za maandalizi ya kumsindikiza mpendwa wetu Profesa Maselle kuelelea katika nyumba yake ya milele na mmekuwa nasi mwanzo hadi kufikia tulipo fikia. nawashukuruni sana na mungu awabariki.
Sehemu ya wanataaluma mbalimbali
Baadhi ya wana taaluma wakifatilia kwa umakini yaliyokuwa yakiendelea Chuoni hapo.
Aliyewahi kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela akitowa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Mkurungezi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa, Samuel Maselle katika kiwanja cha Graduation SQuare MUHAS.
Waombolezaji wakitowa heshima za mwisho.
Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (aliyeshika mwamvuli) akitowa heshima za mwisho katika jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Hospitali hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa, Muhimbili (MOI) Dokt, Respicious Boniface akitowa heshima za mwisho katika jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Hospitaliya Taifa Muhimbili.
Wanataaluma wakiubeba mwili wa marehemu Maselle kuuweka katika gari maalumu tayari kwa kuelekea nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach.
Mwili wa Marehemu Maselle ukiingizwa jana katika Gari.
COMMENTS