WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, DKT. PHILIP MPANGO AIPONGEZA PPF KWA KUWEKEZA KWENYE VIWANDA
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akiongea wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa 26 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiwa katika ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha, (AICC), leo Machi 23, 2017. 

“Tanzania ya Viwanda; Umuhimu na Wajibu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii”

HomeJamii

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, DKT. PHILIP MPANGO AIPONGEZA PPF KWA KUWEKEZA KWENYE VIWANDA

 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akiongea wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa 26 wa Wanachama n...

GROUP LA WHATSAPP LA AFYA YANGU LATOA MSAADA KWA WAJAWAZITO KIBAHA MKOANI PWANI
SERIKALI KUAJIRI MAAFISA UGANI KATIKA KILA KATA NCHINI
RAIS DKT MAGUFULI AMUAPISHA JAJI MKUU WA TANZANIA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO



NA ROBERT OKANDA
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameupongeza Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa kutekeleza kwa vitendo Mpango wa pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano wa kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya Uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kupitia kwenye uwekezaji wa viwanda..
Waziri ametoa pongezi hizo leo Machi 23, 2017 wakati akifungua Mkutano wa 26 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF kwenye ukumbi wa Simba wa KItuo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), jijini Arusha.
“Nimeelezwa kuwa nyinyi PPF kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na Jeshi la Magereza mmeingia kwenye makubaliano ya pamoja ya kuanzisha viwanda vikubwa na vya kisasa vya kuzalisha sukari katika eneo la Mkulazi na Mbigiri Morogoro.” Alisema Waziri Dkt. Mpango
Akifafanua zaidi kuhusu mpango wa PPF kwa ushirikiano na NSSF na Jeshi la Magereza kwenye uwekezaji mkubwa wa viwanda, Dkt. Mpango alisema, “Mimi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama ni mashuhuda wa hilo kwani tuliweza kujionea eneo la mradi la Mkulazi na ujenzi wa miundombinu tulipolitmbelea katika eneo hilo mwezi Desemba mwaka jana.” Alisema.
Akitoa hotuba ya kumkaribisha Waziri wa Fedha na Mipango, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Bw.Ramadhan Khijjah, (pichani juu), alisema, kauli mbiu ya mkutano huu wa 26 wa Wanachama na Wdau wa PPF ni “Tanzania ya Viwanda; Umuhimu na Wajibu wa Hifadhi ya Jamii”.
“PPF imedhamiria kwa dhati kabisa kuunga mkono dhamira ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ya kjuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia viwanda kama inavyoelezwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/2017 hadi 2010/21.
 Naye Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio alisema Mkutano wa mwaka huu ni wa siku mbili na umehudhuriwa na washiriki zaidi ya 800 na lengo la kuchagua kauli mbiyo iliyoelezwa hapo juu ya “Tanzania ya Viwanda; Umuhimu na Wajibu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii” ili kukuza uelewa wa Wanachama na wananchi kwa ujumla juu ya uwekezaji katika viwanda ambao Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imeanza kuifanya ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa wa miaka 5, (2016/17-2020/21 na pia kwa madhumuni ya kuongeza mapato yatokanayo na uwekezaji na kupanua wigo wa kuandikisha wanachama kutokana na ajira zitakazoongezeka.

 Baadhi ya wageni waliohudhuria mkutano huo
 Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw.Adam Mayingu (kushoto), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa GEPF, Bw. Daudi Msangi
 Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele, (kushoto), akijadiliana jambo na Meneja Kiongozi, Uandikishaji wanachama na Elimu, Mbarouk Magawa
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, akitoa hotuba ya ukaribisho
 Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa PPF
 Baadhi ya wageni waalikwa kutoka WCF
 Wajumbe wakiwa mkutanoni
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akitoa hotuba yake ya ufunguzi
 Bi.Stephanie Nandi, akiwa na mwanaye mchanga akitoa ushuhuda baada ya kufaidika na Fao la Uzazi
 Mfugaji Bw.Mrida Mshoto Marocho, akitoa ushuhuda kuhusu faida aliyopata ya bima ya Afya, baada ya kujiunga na mpango wa Wote Scheme
 Bw.Kulwa Mohammed, mmoja wa watu waliotoa ushuhuda wa jinsi alivyofaidika na Fao la Elimu. Kulwa ni Mwanafunzi wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha, (IFM)
 Mjumbe akipitia jarida la PPF lenye maelezo ya kina kuhusu shughuli mbalimbali za Mfuko
 Baadhi ya viongozi waliohudhuria mkutano huo
Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango, akimkabidhi tuzo, Kaimu Meneja Mwandamizi Rasilimali Watu wa TANESCO, Nathan K. Daimon, baada ya Shirika hilo la Umeme nchini kuwa mshindi wa jumla kwa Mashirika ya Umma yanayowasilisha michango yao kwa wakati na mingi inayofikia Bilioni 2 kwa mwaka.
 Waziri wa Afya, Mhe.Ummy Mwalimu, (kushoto), akipeana mikono na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Philip Mpango, wakati akimkabidhi vifaa vya hospitali kwa niapa ya PPF pembezoni mwa mkutano huo. PPF imetoa msaada wa vifaa hivyo vyenye thamani inayokaribia Milioni 100. Vifaa hivyo kwa mujibu wa Waziri Ummy, vitapelekwa kwenye vituo vya afya 11 kote nchini
Waziri Ummy akitoa shukrani baada ya kupokea msaada huo
Mgeni rasmi, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (kushoto), akisindikizwa na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (katikati), na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Bi.Irine Isaka, wakati akiondoka ukumbi wa Simba baada ya kufungua mkutano huo.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, DKT. PHILIP MPANGO AIPONGEZA PPF KWA KUWEKEZA KWENYE VIWANDA
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, DKT. PHILIP MPANGO AIPONGEZA PPF KWA KUWEKEZA KWENYE VIWANDA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEit76T41ud6HlWOKWbZZncyeQIXyhaKR8gJ483LLlTAv4VeaZJ1km6kBS1j04CujFabjNcXG-6vr0l6iGLRzU-LWnrCtrPW-x-8X385zyAwnbGLSh6yhfoTNfHc0guq_bpwgMq_-tscpeM/s640/5R5A6586.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEit76T41ud6HlWOKWbZZncyeQIXyhaKR8gJ483LLlTAv4VeaZJ1km6kBS1j04CujFabjNcXG-6vr0l6iGLRzU-LWnrCtrPW-x-8X385zyAwnbGLSh6yhfoTNfHc0guq_bpwgMq_-tscpeM/s72-c/5R5A6586.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/03/waziri-wa-fedha-na-mipango-dkt-philip.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/waziri-wa-fedha-na-mipango-dkt-philip.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy