HomeJamii

WAZIRI MKUU AKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA ITALIA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji kutoka Italia ili waje kuwekeza kwenye viwanda na usindikaji bidhaa za mifugo ...

BOHARI YA DAWA (MSD) YAPONGEZWA KWA USAMBAZAJI WA DAWA NCHINI
ZIARA YA NAIBU WAZIRI MHANDISI MASAUNI NA WAZIRI BARANDAGIYE WA BURUNDI KATIKA KAMBI ZA WAKIMBIZI NDUTA NA MTENDELI MKOANI KIGOMA
KANUNI ZA MAADILI YA TAALUMA YA MAWASILIANO KWA UMMA KUANDALIWA




WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji kutoka Italia ili waje kuwekeza kwenye viwanda na usindikaji bidhaa za mifugo na uvuvi kwa sababu ni eneo wanalolimudu vizuri.

“Tumedhamiria kujenga Tanzania ya viwanda, tunawakaribisha wawekezaji kutoa Italia ili waje kuwekeza kwenye viwanda vya usindikaji mazao ya mifugo pamoja na uvuvi kwa sababu tunatambua kuwa ninyi mmebobea katika eneo hilo,” alisema.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Februari 28, 2017) alipokutana na Balozi wa Italia nchini Tanzania, Bw. Roberto Mengoni kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.

“Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda ili kuongeza ajira na kuondoa umaskini miongoni mwa wananchi wake. Tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye maeneo mbalimbali,” alisema Waziri Mkuu.

Kwa upande wake, Balozi Mengoni alimweleza Waziri Mkuu kwamba katika muda wa miezi nane ambayo ameishi hapa nchini, amebaini kuwa Tanzania ni nchi yenye fursa nyingi za kiuchumi. “Ni soko kubwa ambalo halijaguswa (untapped market) hasa kwenye masuala ya viwanda na uwekezaji.

Hata hivyo, Balozi huyo alikiri kwamba bado wananchi wengi wa Italia wanahitaji kupatiwa elimu zaidi juu ya fursa zilizopo hapa nchini. “Hadi leo kuna Waitaliano ambao hawajui kuwa Mlima Kilimanjaro uko Tanzania. Wengi wanajua uko Kenya, kwa hiyo elimu zaidi inahitajika katika suala zima la kutangaza utalii wa Tanzania,” alisema.

Alisema tangu afike nchini, wawekezaji kutoka Italia wameonesha nia ya kuwekeza kwenye nishati jadidifu, kiwanda cha kutengeneza nguo za michezo (sports wear) na kwamba wafanyabiashara wengine zaidi wanatarajia kuja hapa nchini.

Ili kutoa uelewa mpana kwa wafanyabiashara na raia wa Italia, ubalozi kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) tumeandaa mkutano mkubwa kuhusu biashara na uwekezaji utakaotoa maelezo kuhusu fursa zilizopo Tanzania katika nyanja mbalimbali.

“Mkutano huu utakaofanyika Mei 6, mwaka huu, utawalenga zaidi wafanyabiashara na utajikita kwenye maeneo makuu sita ambayo ni viwanda vya usindikaji, viwanda vya nguo (textiles), ngozi na mazao yake, miundombinu, nishati na utalii,” alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekutana na Balozi wa Japan hapa nchini, Bw. Masaharu Yoshida ambapo katika mazungumzo yao wamejadiliana mambo mbalimbali yakiweo ya miundombinu, elimu na nishati.




Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU AKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA ITALIA
WAZIRI MKUU AKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA ITALIA
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/03/waziri-mkuu-akaribisha-wawekezaji.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/waziri-mkuu-akaribisha-wawekezaji.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy