Na Lilian Lundo – MAELEZO Serikali inaendelea na operesheni ya kukagua viwanda vinavyotengeneza pombe zilizo kwenye vifungashio vya mi...
Na Lilian Lundo –
MAELEZO
Serikali inaendelea
na operesheni ya kukagua viwanda vinavyotengeneza pombe zilizo kwenye
vifungashio vya mifuko ya plastiki maarufu kama “viroba” ili kujiridhisha kama viwanda hivyo
vimesitisha uzalishaji wa pombe hizo pamoja na kuzuia utokaji wa pombe ambazo
bado zipo katika maghala.
Hayo yamesemwa na
Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Manchale Heche
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wakati wa operesheni hiyo ambayo
inaendelea Jijini Dar es Salaam.
“Zoezi linaendelea
kama lilivyoanza jana ambapo tunakagua viwanda vinavyozalisha viroba, na mpaka
sasa tumeshatembelea viwanda vitatu ambavyo ni kiwanda cha Kibo Spirit
kinachotengeneza pombe ya kiroba aina ya Double Panch, Kiwanda che Blue Nile
kinachotengeneza viroba vya Kitoko na
Rivella pamoja na kiwanda cha True Bell kinachotengeneza viroba vya Bonanza na
Suke,” alifafanua Heche.
Aliendelea kwa kusema
kuwa lengo la operesheni ni kukagua viwanda vyote vinavyozalisha pombe aina ya
viroba ili kujiridhisha ikiwa viwanda hivyo vimetekeleza agizo la Serikali la
kusimamisha uzalishaji wa pombe hizo kuanzia Machi 01, mwaka huu.
Heche amesema kuwa
operesheni hiyo pia inahusisha ukaguzi kutambua idadi ya pombe zilizobaki
katika maghala mbalimbali na kuzuia pombe hizo kutotolewa katika maghala hayo
mpaka hapo Serikali itakapotoa agizo ya namna ya kuziharibu pombe hizo.
Aidha amesema kuwa
agizo limetoka katika mipaka yote ya nchi kuzuia uingizaji wa pombe hizo na
kuzirudisha nchi zilizotoka kwa gharama za muhusika aliyesafirisha pombe hizo.
Kwa upande wake
Meneja Uendeshaji wa Kiwanda cha True Bell (T) Limited kilichopo Shekilango, Godwin Mungere amesema
kuwa kiwanda hicho bado kilikuwa katika majaribio lakini kutokana na agizo la
Serikali wamesitisha uzalishaji wa pombe za viroba ambapo wao walikuwa
wakizalisha viroba aina ya Bonanza na Suke.
Ameeleza kuwa akiba
ya pombe za viroba vilivyobaki katika ghala lao ni katoni 166 za viroba vya
Bonanza na katoni 165 za viroba vya Suke ambapo wanasubiri maelekezo kutoka
Serikalini namna ya kuharibu pombe hizo.
Nae, Mkurugenzi wa
Kibo Spirit kilichopo Sinza kwa Remmy Muhid Mwacha amesema kuwa kiwanda hicho
kilikuwa bado kipo kwenye majaribio ya kutengeneza viroba aina ya Double Panch
lakini kwa sasa hawaendelei na uzalishaji wa pombe hizo ila kiwanda hicho kwa
sasa kinazalisha maji ya kunywa ya Kibo Cool.
Operesheni ya viroba
ilianza rasmi jana kwa mkoa mzima wa Dar es Salaam ambapo ni utekelezaji wa
agizo la Serikali la kuzuia uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa pombe hizo kuanzia
Machi 1, mwaka huu. Adhabu ya kutumia, kusambaza au kuzalisha pombe hizo ni
faini inayoanzia shilingi elfu 50 mpaka milioni 5 na kifungo cha kuanzia miezi
3 mpaka miaka 3 jela.
Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Manchare Heche (kushoto) akikagua nyaraka toka kwa Msimamizi wa Kiwanda cha True Bell (T) Limited Bw. Godwin Mungere mapema leo hii jijini Dar es Salaam wakati wa siku ya pili ya operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.

Baadhi ya Maafisa wa Serikali wakikagua ghala la Kiwanda cha True Bell (T) Limited mapema hii leo Jijini Dar es Salaam wakati wa siku ya pili ya operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.

Msimamizi wa Kiwanda cha True Bell (T) Limited, Godwin Mungere (mwenye shati la njano) akionesha baadhi ya vifungashio vya pombe kali aina ya kiroba mapema hii leo Jijini Dar es Salaam wakati wa siku ya pili ya operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika, kulia ni Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Manchare Heche.

Baadhi ya shehena ya maboksi ya pombe ya viroba aina ya bonanza ikiwa imehifadhiwa katika ghala la kiwanda cha True Bell (T) Limited kilichopo Sinza Bamaga mapema leo hii jijini Dar es Salaam wakati wa siku ya pili ya opereshe
COMMENTS