Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiwa na Mgeni wake ambaye ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshugh...
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiwa na Mgeni wake
ambaye ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya
Afrika Bw. Makhtar Diop, wakiwa katika chumba cha kupumzikia wageni
maalumu katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere, Jijini
Dar es salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi
za Tanzania, Burundi, Somalia na Malawi Bi. Bella Bird.
Makamu
wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Makhtar
Diop, (wa pili kushoto aliyeshika dafu) alipowasili nchini, akiwa na
mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa
tatu kushoto) ambapo anatarajiwa kushiriki katika uzinduzi wa Mradi wa
mabasi yaendayo haraka BRT, Januari 25, 2017, na baadaye kufanya
mazungunzo na Waziri huyo alasiri.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop, (kushoto) akinywa maji ya dafu alipowasili
nchini, akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.
Philip Mpango (kulia) ambapo anatarajiwa kuungana na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, katika uzinduzi wa Mradi
wa mabasi yaendayo haraka BRT, Januari 25, 2017.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Mhe. Dkt. Philip Mpango,
akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi, baada ya mapokezi ya Makamu wa Rais
wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam
24. Januari 2017
Makamu
wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia masuala ya Kanda ya Afrika,
Bw. Makhtar Diop, amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu
ambapo pamoja na mambo mengine, anatarajia kushiriki uzinduzi wa Mradi
wa Mabasi yaendayo haraka tukio linalotarajiwa kufanywa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Jijini Dar es Salama kesho asubuhi.
Makamu
huyo wa Rais wa Benki ya Dunia, amelakiwa na Mwenyeji wake, Waziri wa
Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango kati Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo anayehudumu
katika Nchi za Tanzania, Burundi, Somalia na Malawi, Bi. Bella Bird.
Akiwa
nchini, Bw. Diop atakutana na kufanya mazungumzo pia Rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri wa Fedha na
Mipango Dkt. Philip Mpango, Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu, Sekta
Binafsi ambapo mazungumzo yao yanatarajiwa kujikita katika Miradi kadhaa
ya maendeleo inayofadhiliwa ama kugharamiwa na Benki hiyo kwa njia ya
ruzuku na mikopo yenye masharti nafuu ambayo mpaka sasa inakadiriwa
kufikia thamani ya Dola Bilioni 4 nukta 7 .
COMMENTS