Na Mwandishi Wetu, Mkuranga KIJIJI cha Wasanii cha Mwanzega kimechaguliwa kuwemo kwenye orodha ya vijiji saba ambavyo vimepang...

Na Mwandishi Wetu, Mkuranga
KIJIJI
cha Wasanii cha Mwanzega kimechaguliwa kuwemo kwenye orodha ya vijiji
saba ambavyo vimepangiwa kupata umeme wa Serikali wa Mamlaka ya Umeme
Vijijini (REA).
Mtendaji
wa kijiji cha Mwanzega, Kitwana Kambangwa aliwaomba wanakijiji
wasipuuzie fursa hiyo kwa vile serikali imeona umuhimu wa kijiji hicho
kupata umeme ili kurahisisha maendeleo.
Akiwasomea
wananchi taarifa ya Mratibu wa Vijiji na Kata wa Utawala bora na
maboresho wa wilaya ya Mkuranga kuhusu mradi huo, Mtendaji wa kijiji,
Kambangwa alisema wananchi wewe tayari kutoa miti yao ya mazao na mimea
bila fidia ili kupisha kazi ya kupitisha nguzo za umeme wa REA.
'Ndugu
zangu Serikali ya Rais John Magufuli imetusikia kilio chetu sisi watu
wa vijijini, tunaletewa umeme ili tuwe na maendeleo kama wenzetu wa
mjini, tusiipuzie nafasi hii kubalini kupisha nguzo zipite bila
kulalamikia fidia' alisema Mtendaji Kambangwa.
Alisema
sambamba na kijiji cha Mwanzega, vijiji vingine vitakavyonufaika na
mradi wa REA ni Mbezi, Msorwa, Shungubweni, Boza, Kuruti na Mbonga
ambavyo mradi huo utapelekwa moja kwa moja kwenye shule za Msingi,
Zahanati, Viwanda na Shule za Sekondari.
Awali
wakichangia kuhusu mradi huo Dkt.Frederick Mwakibinga alisema umeme
ukishaingia kijijini baada ya muda mfupi kutakuwa na maendeleo ambayo
yatawanufaisha wananchi wote na kaongeza ajira kwa vijana.
Mwanakijiji
mwingine Ramadhani Mwanehekwa alisema wao wako tayari kuruhusu mazao
yao kukatwa bila kudai fidia lakini Serikali nayo iwakumbuke katika
kuwaletea wananchi huduma za jamii, kama zahanati, barabara, maji na
elimu.
Mkutano
huo uliohudhuriwa na wanakijiji wengi waume, wanawake na vijana, Ali
Ndambwe aliwashauri wanakijiji wenzake wasifikirie kulipwa fidia kwa
ajili ya mazao zitakapopita nguzo waangalie faida watakayoipata vijana
wao na majukuu baada ya kuingia umeme na kujengewa viwanda.
Mwenyekiti
wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Cassim Taalib aliwapongeza
wanakijiji wenzake kukubali kutoa mazao na mimea yao bure kwa wale ambao
mradi wa umeme utawapitia.
Katika
mkutano huo Mwenyekiti wa kijiji, Abdallah Mwangira aliwataarifu
wananchi hao kuwa serikali imewaandalia wananchi wa vijiji hivyo mambo
makubwa ya maendeleo ambayo aliahidi kuyasema kikao kijacho.
Kijiji
cha Mwanzega ndipo kilipo kijiji cha wasanii ambacho mpaka sasa
zimejengwa nyumba 250 za kisasa as wasanii ambazo zitaingia kwenye mradi
wa REA.
Mkazi wa Mwanzega Dkt. Frederick Mwakibinga akichangia mada kwa wanakijiji watakaonufaika na mradi huo baada ya kuukubali.

Wanakijiji
wa kijiji cha Wasanii Mwanzega Mkuranga wakiwa kwenye mkutano wa
kuidhinisha mradi wa Ilene wa REA kupita kijijini hali jana.
COMMENTS