MBUNGE WA JIMBO LA TANGA AMUANGUKIA WAZIRI MWIJAGE
HomeJamii

MBUNGE WA JIMBO LA TANGA AMUANGUKIA WAZIRI MWIJAGE

Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akizungumza na waandishi wa Habari ambao hawapo pichani kuhusiana na suala hilo. ...

RAIS MAGUFULI KUWA MGENI RASMI SIKU YA SHERIA NCHINI
SSRA, TRA ZAPEWA TUZO NA UMOJA WA AFRIKA, NI KUTOKANA NA UBUNIFU KATIKA UTOAJI HUDUMA
POLEPOLE ATEMBELEA MAGAZETI YA UHURU, MTANZANIA NA UHURU FM, LEO
MBUNGE WA JIMBO LA TANGA AMUANGUKIA WAZIRI MWIJAGE

Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akizungumza na waandishi wa Habari ambao hawapo pichani kuhusiana na suala hilo.

 Mkurugenzi Uzalishaji wa kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro, Vivek Pandey akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na shirika la viwango Tanzania (TBS) kutotoa kibali cha ubora unaohitajika na hivyo kusitisha uzalishaji.

Mkurugenzi Uzalishaji wa kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro, Vivek Pandey  kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na shirika la viwango Tanzania (TBS) kutokutoa kibali cha ubora unaohitajika wa kiwanda hicho na hivyo kusitisha uzalishaji. Kulia ni Msimamizi wa Kiwanda hicho, Paskal Dimelo
Msimamizi wa Kiwanda cha kuzalishaji Saruji
Mkoani Tanga cha Kilimanjaro, Paskal Dimelo akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusiana na shirika la viwango Tanzania (TBS) kutokutoa kibali cha ubora unaohitajika na hivyo kusitiza uzalishaji wake kushoto ni Mkurugenzi Uzalishaji wa kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro, Vivek Pandey.
MBUNGE wa Jimbo la Tanga kupitia Chama cha Wananchi CUF Alhaj Mussa Mbaruku amemuomba Waziri wa Viwanda na biashara Charles Mwijage kuingilia kati ucheleweshawajiwa wa cheti cha ubora wa viwango unaotolewa na shirika hilo la TBS na kusababisha zaidi ya watumishi 300 kupoteza ajira baada ya  kiwanda hicho kufungwa.

Ameyazungumza hayo jana baada ya siku kadhaa kutolewa taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa shirika hilo limechangia kwa kiasi kikubwa kupoteza ajira kwa zaidi ya watumishi 300 kutokana na agizo lao la kusitiza uzalishaji katika kiwanda hicho kwa madai ya kukosa ubora unaotakiwa.


Alionyesha masikitiko yake hayo juu ya hataua iliyochukuliwa na shirika hilo la Ubora wa viwango Tanzania (TBS) ya kukifungia kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro kilichopo Jijini Tanga kwa kudaiwahawajafikia ubora unatakiwa katika bidhaa hiyo bila ya kuangalia athari za mwekezaji huyo na ajira zilizopotea kiwandani hapo.

Aidha alisema ni jambo la kushangaza kwa viongozi wa mamlaka hiyo husika (TBS)ambapo kwa namna moja au nyingine wanaonekana wanaikwamisha Serikali katika mpango wake wa kukua katika uchumi wa viwanda ambavyo vinaweza kuwa mkombozi wa ajira hapa nchini.



“Serikali inapambana na uchumi wa viwanda vitakavyoweza kusaidia ajira kwa vijana wetu sasa kinachotokea katika kiwanda hiki kunaonekana kuna watu wachache wanataka kumkwamisha muwekezaji huyu,hivi wizara husika iko wapi?nini hatma ya mwekezaji huyu na kufanya hivi hatuoni kama tunawafukuza hawa wawekezaji?”Alihoji Alhaj Mbaruku.

Hatua ya kusitiza huduma ya uzalishaji wa kiwanda hicho licha ya kuathiri ajira za wafanyakazi hao lakini pia itasababisha serikali kukosa mapato yanayoweza kusaidia kukuza uchumi wa Taifa na Mkoa wa Tanga.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Vivek Pandey alisema kinachowaasumbua wao ni cheti bora kutoka kwa shirika la viwango cha kutambuliwa hivyo wanaomba suala hilo liingiliwe kati na mamlaka husika ikiwemo serikali ili waweze kuendelea na uzalishaji ambao utaweza kuongeza wigo wa ajira kwa vijana.

Alisema baada ya taarifa zao kutoka kwenye vyombo vya habari alifika mmoja kati ya wataalamu kutoka katika shirika hilo Jijini Dar es saalm na kuondoka na sampo ya bidhaa hiyo ambapo mpaka sasa bado hawajapata majibu sahihi ya hatma yao.

“Baada ya taarifa zetu kuruka kwenye vyombo vya habari siku ya pili tu alitumwa mtu kutoka makao makuu ya TBS Jijini Dar es salaam na niliondoka nae sambamba na sampo ya bidhaa hiyo nahii leo ja (jana)kwenda tena ili kuona hatua gani zimechukuliwa dhidi yetu”Alisema Pandey.

Aidha alisema hatua hiyo ya kusitisha uzalishaji mbali na kupoteza ajira kwa vijana lakini wamekisababisha hasara kiwanda kwa zaidi ya shilingi Milioni 200 ambazo zinatokana na tani elfu 11 zilizozalishwa kisha kuonekana zipo chini ya kiwango.


(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha).
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MBUNGE WA JIMBO LA TANGA AMUANGUKIA WAZIRI MWIJAGE
MBUNGE WA JIMBO LA TANGA AMUANGUKIA WAZIRI MWIJAGE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjCnJKhAJ_muQza3lA2XB0hmlg3ieGUTjZchynWBycioVIlaurZxf38Kc3EJBGGFc6WpxyGzMgWfou0JSVG0NYw5_uC63YMN_dMbXW_SmM6jxjq6BVCvJCnIWYO7jH7oKWaJniDsvuLh0VU/s640/POLE.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjCnJKhAJ_muQza3lA2XB0hmlg3ieGUTjZchynWBycioVIlaurZxf38Kc3EJBGGFc6WpxyGzMgWfou0JSVG0NYw5_uC63YMN_dMbXW_SmM6jxjq6BVCvJCnIWYO7jH7oKWaJniDsvuLh0VU/s72-c/POLE.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/03/mbunge-wa-jimbo-la-tanga-amuangukia.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/mbunge-wa-jimbo-la-tanga-amuangukia.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy