Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga (kushoto), akimkabidhi tuzo, Mkurugenzi wa Uhusian...
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga (kushoto), akimkabidhi tuzo, Mkurugenzi wa Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Sarah Kibonde Msika,
kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Kituo cha
Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Januari
26, 2017. Mamlaka hiyo na ile ya Mapato, TRA zilikabidhiwa tuzo za
ubunifu na Umoja wa Afrika Nchini Ethiopia hivi karibuni.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga, akimkabidhi cheti Meneja wa Customs Automation wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania, (TRA), Bw. Tinasimile Felix.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAMLAKA
ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na Mamlaka ya
Mapato Tanzania, (TRA), zimetunukiwa tuzo za ubunifu katika utoaji huduma na
Umoja wa Nchi za Afrika (AU).
Akikabidhi
tuzo hizo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Msemaji wa wizara hiyo, Bi Mindi Kasiga, (pichani juu),
alisema Umoja wa Afrika umezitunuku Mamlaka hizo mbnili kutokana na ubunifu
katika utoaji huduma.
Akizunhgumzia
tuzo ambayo SSRA imekabidhiwa, Meneja Uhusiano wa SSRA, Bi. Sara Kibonde Msika
alisema, kupitia wataalamu wa nje na ndani Mamlaka ilibuni mfumo mtambuka ya
kupanua wigo wa Hifadhi ya Jamii kwa kutumia Tehama, ambapo ilianzisha mradi wa
Kanzi Data ya Taifa ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii (National Social Security
Collaborative Database Bridge (NSSCDB).
Alisema
takwimu za Sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini kwa kipindi kinachoishia Juni 2016,
Mifuko yote nchini ina jumla ya wanachama Milioni 2.46.
Naye
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu ya Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Nchini, (TRA),
Bw. Richard Kayombio alisema, TRA imekuwa ikiboresha huduma zake katika miaka
ya hivi karibuni ambapo utoaji wa huduma katika Mamlaka hiyo umekuwa ni wa
haraka na wenye manufaa makubwa.
Alisema,
kwa kiasi kikubwa TRA imekuwa ikitoa huduma zake kwa kutumia Tehama na hivyo
kupunguza usumbufu na muda mwingi uliokuwa ukitumiwa na wateja katika kufanya
malipo mbalimbali.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sara Kibonde Msika
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu ya Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Nchini, (TRA),
Bw. Richard Kayombio
Picha ya pamoja kati ya msemaji wa wizara, na maafisa wake na watunukiwa
Picha ya pamoja, msemaji wa wizara na watunukiwa wa TRA
Bi. Mindi Kasiga (kushoto), akimkabidhi cheti, Bi. Sara Kibonde Msika
COMMENTS